GEORGE; NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA 05


(ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Salma anarudi kwa George baada ya kusikia ana mwanamke mwingine, wanagombana mpaka anataka kujiua lakini anapona. Jack anakuja wanagombana na George anamfukuza Salma, ila anakua na hasira ambazo anazihamishia kwa Jack, anampiga na kumfungia ndani, akijua kuwa ameshamuua basi anarudi ili kwenda kumtupa. ENDELEA….)

Nilifika nyumbani nikiamini kuwa Jack atakua ameshafariki dunia, nilijua nishaua hivyo natakiwa kutafuta sehemu ya kumtupa. Nilifungua milango taratibu mpaka chooni, bado alikua amelala chini palepale nilipokua nimemuacha. Niliiinama harakaharaka ili kumbeba, wakati nahangaika naye nilisikia sutiti yake.
“Usinipige tena, utamuua mtoto wako George….” Ilikua ni sauti ambayo ilinishtua kwani nilijua kuwa nimeshika maiti. Lakini haikua hivyo, Jack alikua mzima kabisa ingawa alikua kachoka sana nilishangaa alikua na nguvu kidogo.

“Upo hai! Upo hai mke wangu! Upo hai mke wangu nisamehe!” Nilianza kupiga kelele huku nikimnyanyua harakaharaka, sijui nilipata wapi nguvu lakini nilimbeba kama karatasi mpaka kitandani. Hapo nilimkalisha lakini alishindwa kukaa, alilala kitandani huku akijitahidi kuongea kunisisitiza kuwa nisimpige tena kwaajili ya mtoto.
“Usijali, siwezi kukupiga, nakuahidi kabisa kwua siwezi kukupiga, kaa utulie. Nakupenda sana mke wangu, nakupenda siwezi kukupiga tena, niamini alikua ni shetani!”

Nilimuambia huku nikimchunguza mwili wake ambao ulikua umevimba sana, alikua kaumia karibu kila sehemu yaani alikua hatazamiki. Kwa kumuangalia niliona kama ni mtu mpya kwangu, ilikua kama nimemuokota akiwa vile akiwa kapigwa na mtu mwingine.
“Hivi mtu atafanyaje unyama wa namna hii? Huyu sio mimi atakua ni shetani tu, sio mimi!”
Kwa akili yangu na namna alivyokua ameumia ilikua ngumu kwangu kukubali kuwa mimi ndiyo nilikua niemfanya vile.

“Nisameha mke wangu, nisame sana, yaani sijui ni kitu gani kimeniingia akilini kwangu lakini nisamehe….” Niliomba msamaha sana lakini yeye ni kama hakunisikia.
“Mwanangu hachezi kabisa, kaacha kupigapiga, sijui kuna nini George, nipeleke hospitalini, najihisi siko sawa, sioni kama mwanangu yuko sawa….” Alizidi kuniambia, niliona ni sawa, nilimsaidia kunyanyuka, nilitaka abaidlishe nguo lakini alikataa, bado alikua ana nguvunguvu ingawa nilimuacha muda mrefu nikiwa nimemfungia ndani bila chakula wala nini?

“Upate chakula kwanza, usiende hivi Hospitalini…” nilimuambia lakini bado alikataa.
“Nimeshakula, mimi niko sawa kabisa, sitaki chochote, nilikua nakunywa maji ya chooni na niemshiba ninachotaka sasa hivi ni kujua hali ya mwanangu tumboni. Nataka sana mtoto na najua unamtaka sana, kama sitakua imara huyu mtoto atafia tumboni.” Kusema kweli alikua anajikaza, kwa namna alivyokua kavimba, mwili mzima umevimbia damu hata mimi kumshika ilikua shida, kila nikimgusa niliona kama namuumiza lakini yeye wala hakujali. Alikua akimuwazia mtoto wetu tu.

Nilimbeba mpaka kwenye gari ili kumpeleka hospitalini, hapo akili yangu ilikua haiwzi kitu zaidi ya mtoto, kama vile si mimi niliyempiga nilihisi kama kafanyiwa unyama flani hivi na mtu mwingine. Lakini nikiwa njiani nakaribia kufika Hospitalini akili ilianza kuzinduka na kufanya kazi vizuri.
“Watauliza kafanya nini? Kwa hali yake hii ni lazima watataka PF3. Nilijikuta nasita.
“Hivi hatanitaja kweli kuwa mimi ndiyo nimefnanyia hivi?” Niliwaza huku nikipunguza mwendo mpaka nikasimama.

“Vipi mbona umesimama?” Aliniuliza, nilizima gari na kumgeukia.
“Tunaenda kusema nini tukifika huko?” Nilimuuliza swali ambalo nadhani hakulitarajia.
“Kusema nini hukusu nini?” Aliniuliza, nilijaribu kumuelewesha kuwa kwa hali yake aliyokua naye hospitalini wasingekubali kumtibu mpaka wapiti Polisi.

“Mimi sipo tayari kufungwa, na kama umeshanisamehe sioni kama kuna haja ya kushirikisha Polisi….” Nilimuambia kwa sauti ya ukali kidogo.
“Hata mimi sitaki mambo ya Polisi, nitawaambia kuwa nimeondoka kwenye ngazi…” Aliniambia, nilikaa na kufikiria kwa muda nikasema hapana, huu ni ujinga, hakuna mtu anayedondoka kwenye ngazi akang’oka nywele, huyu lazima atanifunga!” Niliwaza huku nikifungua mlango wa gari na kutoka, nilirudi mpaka siti ya nyuma alipokua amelala. Nikafungua mlango kisha nikamuamuru atoke nnje. Mwanzo alikataa lakini nilipomtishia alitoka.

Nilirudi upande wa dereva nikazima taa za gari, nikamshika mkono na kumsogeza pembezoni kabisa mwa Barabara ambapo kulikua na mtaro mkubwa bila kuwaza mara mbili nilimsukumia huko.
“Watu watakuokota na kujua umepigwa kwakua ulikua umelewa.” Nilimuambia akiwa kule chini ambapo alianza kupiga kelele.

Nilikumbuka chupa za pombe ambazo nilikua nazo kwenye gari, nilizichukua ili nikitupa maiti yake nimmwagie mwili mzima ili ionekane kama vile alikua kalewa wahuni wakamvamia. Nilizichukua na kuzifungua kisha nikaanza kumwagia akiwa pale chini, moja niliivunja kisha nikaondoka eneo lile.

“Piga kelele watu watakuja kukuokota….” Nilimuambia wakati nawasha gari na kuondoka kwa kasi. Ile sehemu ilikua haijajificha sana na kwa usiku ule nilijua lazima kuna watu watapita hivyo kama akipiga kelele basi itakua rahisi kupata msaada. Sikutaka hata kusubiri, niliondoka moja kwa moja mpaka nyumbani, niliingia chumbani na kupanga vitu vizuri, nikaingia bafuni na kufuta damu zilizokua zimegandiana sakafuni kisha nikapanda kitandani kusubiria simu kuwa mke wangu kaokotwa.

Nilijua ni lazima atanitaja lakini kwa hali ilivyokua na namna nilivyokua mstaraabu, mtu wa Kanisani, kila mtu ananipenda nilijua moja kwa moja kuwa hata akisema ni mimi nimempiga hakuna mtu wa kumuamini. Nilisubiri simu mpaka asubuhi lakini sikusikia simu ya yeye kupatinaka, zaidi simu nilizokua napigiwa zilikua ni ndugu zake nao wakiulizia yuko wapi, hali hiyo ilizidi kunichanganya zaidi kwani nilihisi labda atakua kaumia sana au nilivyomsukuma alijigonga sehemu na kufia hapohapo.

Mpaka subuhi bado nilikua macho, sikupata hata lepe la usingizi. Asubuhi nilipigiwa simu na Mama yake, nilijua labda naye ananiulizia lakini hapana, alikua Hospitalini aliniambia kuwa mke wangu ameokotwa mtaroni.
“Najua unaenda kazini Baba lakini nimeamua kukuambia ili usipate wasiwasi, hali yake ni mbaya lakini Mungu atasaidia.” Mama yake aliniambia huku akilia.

“Mama mbona unalia, ni kitu gani kimempata mke wangu, naimbie….” Nilimuuliza nikionyesha kama nimepaniki, Mama mkweli alijaribu kunisihi nisipaniki na kuniambia kuwa yuko salama lakini name sikutaka kukubali.
“Mama mbona unaongea kama unalia?” Nilimuuliza. “Niambie mke wangu ni mzima?”
Nilimuuliza, alisisitiza kuwa ni mzima lakini nilipomuulizia kuhusu ujauzito nikamuulizia kuhusu mtoto wangu hapo alikaa kimya.

“Mama kuna nini? Ni kitu gani kimempata mwanangu?” Niliuliza kwa masikitiko, kusema kweli pamoja na unyama nilikua nimemfanyia lakini bado nilikua naumia, nilijua kuwa matendo yangu inawezekana yakaharibu maisha yangu yote nilikua na hamu sana na mtoto na sikujua ni kwanini nilimpiga mke wangu.
“Mwanangu, kila kitu kiko sawa wewe nenda tu kazini, nenda tu Baba hata ukija hapa hakuna kitu unaweza ku….” Mama mkwe alijaribu kuongea lakini alishindwa, alianza kulia hivyo nikaanza kazi ya kumbembeleza.

Nilimuomba anielekeze hospitali aliyokuepo lakini aligoma akiniambia hataki niende.
“Naona aibu mimi mwanangu, naona aibu sana, naona aibu….” Aliongea, alijikaza sana kutokulia lakini alishindwa alianza tena kulia. Hapo ndipo nilimlazimisha sana mpaka akakubali kuniambia alipokua. Nilikua napajua na hakukua mbali sana na kwangu, sehemu niyomuacha nilijua lazima watakao muokota watampeleka pale.

Niliwasha gari na kwenda kumuona Mama mkwe, alikua kakaa nnje kwenye chumba cha upasuaji.
“Kuna nini Mama?” Nilimuuliza, alianza kulia huku akiniomba msamaha, aliniomba sana msamaha huku akimlaumu binti yake.
“Mwanangu, kumbe wakati tunangaika na kumtafuta yeye anafanya starehe zake, yaani hajionei hata huruma. Karudia tabia zake za chuo amerudi tena kunywa pombe. Amepona lakini kaniulia mjukuu wangu. Mwanangu mwanao hayupo tena, mwanangu kamuua mwanao, nisamehe mimi kwakua ndiyo nilishindwa kumlea vizuri, nisamehe Mama!”

Mama alikua anaongea kama charahani huku akilia. Niliona kabisa kuwa msala aumemgeukia Jack. Mama yake alianza kufunguka tabia zake kipindi akiwa chuo, hata hazikua tabia mbaya sana ni mambo ambayo hata mimi niliyafanya lakini kwakua Mama yake alikua ni mtu wa dini walikua wanagombana sana.

Kwanza ilikua ni kuhusu kuvaa kwake na pili alikua anakunywa pombe kitu ambacho Mama yake alikua hapendi kabisa. Ingwa niliumia sana kumpoteza mwanangu lakini angalau nilipata ka ahueni kidogo kuwa msala hauwezi kunigeukia.
“Nisamehe mimi mwanangu, yaani sijui hata hii aibu naipeleka wapi? Baba zake nitawaambia nini, alishaniabisha kubeba mimba sasa hivi tena wakijua kuwa imetoka tena amepigwa na wahuni huko aklifanya umalaya na kunywa mipombe yake si nitaaibika mimi?

Kanisani mimi ni kiongozi, nawasema mabinti wa watu lakini wakwangu ndiyo hivi, kaniaibisha sijui nitafanya nini jamani….” Mama aliongea kwa uchungu sana, alikua anaumia kiasi kwamba nilijikuta na mimi machozi yananitoka.
“Pole kijana wangu, hivi kwanini wanawake tunakua hivi, mtu unapata kijana mzuri kama huyu lakini bado hatulii, ana kazi nzuri lakini hatulii, sijui nina laana gani mimi jamani, daaa!”

Aliendelea kulalamika, alikua anaongea kwa uchungu yeye ndiyo mtu wa kwanza kupigiwa na alikua hajamuambia mtu mwingine yoyote, alikua anaona aibu hata kuwaambia Kaka zake na Jack, alikua anaona kama kadhalilishwa yeye.
“Mama huyu ni mke wangu, nilikuja kwako kujitambulisha kwa heshima baada ya yeye kubeba ujauzito wangu, nilimuambia kuwa nitamuoa na kweli nitamuoa. Akitoka hapa nataka aje kwangu, nitamuuguza mimi mwenyewe kama mke wangu na sitamuambia mtu yoyote. Huyu ni mke wangu, kazi ya mume ni kumfichia mke wake aibu zake kwani ni aibu zangu mimi nitamhudumia mimi mwenyewe na kama mtu akiuliza basi alipata ajali ndiyo akawa hivyo. Mama mimi ndiyo nilimpa huu ujauzito na kukuaibisha sitakubali uaibike tena Mama.”

Nilimuambia Mama mkwe, nilijua kabisa kuwa, kama nikiziteka akili za Mama mkwe basi hakuna kitu ambacho angesema na kuaminika. Kwa namana Mama yake alivyokua anaongea nilijua kabisa kuwa hajamuambia kitu chochote. Nilijifanya mwema sana mpaka Mama mkwe alishangaa. Lengo langu halikua kumuoa bali nilijua kama nikimuacha akahudumiwa na ndugu zake basi ni rahisi yeye kuongea ukweli na kuniharibia sifa yangu.

****

Alikaa hospitalini kwa wiki mbili, alifanyiwa upasuaji mara mbili ndani ya hizo wiki mbili kwani kuna matatizo yalitokea wakati akifanyiwaupasuaji wa kwanza ambao ulikua ni mdogo tu ila huu wapili ulilazimika kufanyika mkubwa. Kilikua ni kipindi kigumu sana kwangu kwani nilikua sijielewei, nilikua na mawazo sana kila nikimuangalia hali yake nikiona kuwa mimi ndiyo nilikua nimemfanyia vile haikuingia akilini kabisa.

Hakua amemuambia mtuyeyote kitu chochote kilichokua kimetokea, nadhani alikatishwa tamaa na maneno ya Mama yake ambayo alimuambia baada tu ya kupata nafuu.
“Umenivua nguo mwanangu, najuta hata wewe kuwa mtoto wangu, kwa ulivyonidhalilisha natamani hata hao uliokua unakunywa nao wangekuua kabisa nikazika.”

Wakati Mama yake anamuambia hivyo nilikua nipo hapo, nilimuona kanyong’onyea akashindwa hata kuongea. Hali yake haikua mbaya sana lakini baada ya Mama yake kumuombea kifo niliona kama moyo wake umepooza. Alibadilika, akabaki kimya, ni kama alikua kafungwa mdomo. Wakati wa kutoka hospitalini alitaka kwenda kwa kaka yake, wifi yake alikuja na kutaka kumchukua ili akamhudumie lakini Mama yake alikataa.

“Unataka akakuvunjie na ndoa yako? Huyu ana mwanaume wake, muache akaishi maisha yake!” Mama yake alimuambia, alikua na hasira iliyojaa chuki. Nilimuelewa kwani alikua akiamini kuwa binti yake alikua katoroka usiku kwenda kunywa pombe na huko akavamiwa na wanaume wakampiga mpaka mimba kutoka, alimuona mwanae kama mnyama na hakumpa muda wa kuongea. Ingawa kesi ilishafika Polisi kwani waliomuokota waliripoti lakini aligoma kuongea kitu chochote, aliwaambia alikua hakumbuki kitu.

Naamini baadaya kumsikia Mama yake akiongea vile alimuacha aamini alivyokua anaamini. Nilijifanya msamaria mwema nikamchukua na kuanza kuishi naye, hakusema kitu chochote, ingawa kila dakika nilikua namuomba msamaha lakini hakujibu kitu. Alikua ni mtu wa kulala tu, haongei na hafanyi chochote, kwa kumuangalia ni kama alikua kashakua taahira flani, sijui ni mawazo au mshituko lakini alikua anaboa na kutia hasira kuishi naye.

“Utakaa hivi mpaka lini, umeshapona unatakiwa kurudi kazini!” Nilimuambia, mwezi mmoja baada ya lile tukio alikua hajaongea kitu chochote. Ingawa nilishajitutumua na kumuambia kila mtu kuwa ninamuoa lakini niliogopa kwani alikua haongei kitu, haonyeshi hasira wala kuniambia kitu chochote. Alishapona lakini alikua hataki kurudi kazini, walishamuita zaidi ya mara tatu lakini aligoma.

“Siwezi kuishi na wewe hivi, kama huwezi kubadilika basi ondoka kwangu!” Nilimuambia kama kumtishia, lakini siku hiyo natoka kazini nilikuta kachukua kila kitu chake na kuondoka. Kesho yake nafika kazini naambiwa kaandika barua ya kuacha kazi.
“Nimempa likizo, naona hayuko sawa ila ongea naye, hii ofisi si yangu hivyo siwezi kumbeba muda mrefu!” Afisa utumishi aliniambia, nilijisikia vibaya kwani moja kwa moja niliona kama mimi ndiyo nimeyaharibu maisha yake.

Akili zilisharudi hivyo niliamua kwenda kuomba msamaha tena.
“Ndio kosa gani hili ambalo halisameheki tena?” Nilijiuliza bila majibu, nakumbuka ilikua ni usiku, niliamua kwenda kwake, nilijua bado alikua hajahama na kweli nilimkuta. Alinikaribisha vizuri tofauti na mwanzo, alionekana kuchangamka flani hivi, nilifika pale na kuanza kuongea.

Nilimpa risala ndefu nikijaribu kumuambia kuwa hana haja ya kukasirika vile na kuacha kazi, mimi niko tayari kumuoa.
“Shukuru Mungu uko salama, najua umempoteza mtoto wako kwa makosa yangu lakini niamini nikimuambia nimejifunza na nimeamua kubadilika. Kama ni ishu ya mtoto tutapata mwingine tena sasa hivi tukiwa ndani ya ndoa.” Nilimuambia lakini ndiyo kama nilikua nimeupalia mkaa, alianza kulia kama mtoto hivyo nikapata kazi ya kuanza kumbembeleza tena.

“Wewe utaoata mwingine lakini mmimi siwezi kuapta mtoto mwingine tena.” Aliniambia hukua kiendelea kulia.
“Kuna haja gani ya kuendelea kuishi kama siwezi kwua Mama tena, sina haja ya kufanya kazi, ni bora kufa. Kila mtu ananiona malaya, Mama yangu hanitaki anatamani ningekufa siku ile sasa kwanini nihangaike tena… hapana.” Aliongea kwa uchungu, sikumuelewa kabisa kwanini alikua anasema hivyo.

Kwanini umekata tamaa, kama ni mtoto tutahangaika na tutapata mwingine.” Nilimuambia, alinyanyuka kwa hasira na kubadilika ghafla, mwili wake ulikua mwekundu mpaka nikahisi anaweza kunidhuru, alikua kavimba.
“Tutapataje mwingine wakati walinitoa kizazi?” Aliniambia, nilikua sijui hilo hivyo nilibaki nauliza uliza.
“Unamaanisha nini kusema hivyo?” Nilimuuliza.
“Namaanisha umeharibu maisha yangu, kwenye oparesheni ya pili walinitoa na kizazi hivyo siwezi kuzaa tena na sitamani kuishi tena, sina sababu hata ya kufanya kazi.”

Hakikisha unafuatilia ukurasa wetu @

ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post