KIBUYU CHA BABU - 5 Mwishooo



sudy alitimua mbio hatimae akafika nyumbani kwao....kumbe mzee mkumbo alikuwa ameshazipata taarifa kichawi...sudy aliparamia mlango kisha akamueleza babu yake yale yaliyotokea huko shuleni kwao.. mzee mkumbo alirudi chumbani kwake... alichukua kibuyu chake...kisha akakinyanyua juu""" ghafla ilisikika sauti ikimpa maelekezo kwamba jinsi ya kuwarudisha misukule hao kwenye kibuyu...aliambiwa aende kwenye mto unaitwa MWADOVYA mto huo ni wa KICHAWI KUTOKA KUZIMU akatumbukize kibuyu kile kisha achote maji hayo.... atakapokutana na misukule awamwagie maji yale na baada ya hapo nafsi za misukule wale zitarudi ndani ya kibuyu...
baada ya kupata maelekezo hayo kutoka kuzimu.. alijipanga kuelekea kwenye mto MWADOVYA... alipofika tu kwenye mto huo alikutana uso kwa uso na yule mganga maziku"""kumbe mganga maziku alikwenda kutibiwa ni baada ya kushambuliwa na nguvu za kichawi za mzee mkumbo kisha akaungua mwili mzima.... pia aliomba kuongezewa nguvu ili apambane na mzee mkumbo... awaokowe wanakijiji cha jirani...
mganga maziku aliongezewa nguvu za ajabu... mara ghafla...

mara ghafla mzee mkumbo aliingiwa na wasiwasi.. alijiuliza mganga maziku kapajuaje huko na kaenda kutafuta nini... mzee mkumbo hakuweza kufanya chochote kwa sababu alijua ni mwiko kuleta vita eneo lile.. hata mganga maziku alijua kuwa haitakiwi kufanya vurugu au mapambano katika eneo hilo kisha mganga maziku aliyayuka na kupotea kichawi""" mzee mkumbo aliusogelea mto ule kisha akasujudu na kuchota maji ya mto ule kwa kutumia kibuyu chake... wakati anayachota maji hayo alikuwa akiwaza sana juu ya mganga maziku... hivi huyu ni nani ambae anafuatilia mambo yangu inamaana hakomi tu??? alijisemea moyoni mzee mkumbo...
baada ya kumaliza kuchota maji hayo alinyanyuka na kupotea kichawi.. ni kitendo cha sekunde ghafla alifika nyumbani kwake... alijitokeza ndani ya chumba chake cha kulala.. kisha akainama na kutoa ungo wake wa kichawi chini ya uvungu.. akaanza kuandaa mikakati jinsi ya kunasa nafsi za misukule waliotoka ndani ya kibuyu baada ya mjukuu wake sudy kuiba kibuyu na kukidodosha chini kikafunguka na nafsi za misukule wale zikatoka ndani ya kibuyu kile....
baada ya kufika majira ya saa sita usiku mzee mkumbo alijipanga kwa ajili ya kuizungukia mitaa ya kijiji hicho ili kuwanasa misukule wale na kuwarudisha kwenye kibuyu... punde alipotea kichawi ni kitendo cha sekunde aliingia kwenye mitaa ya kijiji hicho.....alianza kunasa mmoja baada ya mwingine....

*************

kule kwenye kijiji cha jirani alionekana mganga maziku naye akijipanga kwenda kumkabili mzee mkumbo.... ilipofika majira ya saa nane(8) usiku mzee mkumbo alikuwa ameisharudisha robotatu ya misukule wale ndani ya kibuyu chake.. alifurahi sana.... ghafla alihisi harufu ya hatari... tena hatari ya leo ilikuwa ni kubwa kuliko... alistuka... bila shaka ni yule mwanaharamu anayefuatilia mambo yangu sasa leo nitaondoa uhai wake. wakati mzee mkumbo akiwaza hivyo mara ghafla alipigwa na nguvu za ajabu alistahajabu... kidogo akimbie....kisha mganga maziku akajitokeza akasema leo ndio mwisho wa maisha yako kisha akarusha nguvu za kichawi zilimrusha mbali mzee mkumbo... eeeh mzee mkumbo alipo ona mambo yamekuwa magumu aliamua kupaa na ungo wake...punde mganga maziku alimfuata hukohuko juu aisee ilikuwa vita ya ajabu walipigana kwa nguvu za kichawi huko juu angani.... lakini ilionekana uchawi wa mzee mkumbo ulikuwa ni moto wa kuotea mbali... mapigo aliyokuwa anayatumia kurusha nguvu za kichawi.. yalimuogopesha mganga maziku....alizidiwa nguvu na kuamua kutimka kuelekea kijijini kwao mzee mkumbo alipandwa na hasira za hali ya juu... uso wake ulibadilika rangi na kuwa mweusi kama mkaa macho yakawa mekundu... hii iliashiria hasira za hali ya juu.... wakati mganga maziku anamkimbia mzee mkumbo.... alipogeuka nyuma aliogopa baada ya kuona uso wa mzee mkumbo umekuwa mweusi na macho yake kuwa mekundu.... ghafla alipigwa na skadi iliyotoka kwenye kibuyu cha mzee mkumbo mganga maziku alidondoka kutoka angani mpaka chini....kisha mzee mkumbo alijisemea shaabashi mimi sio mtu wa mchezo mchezo...hii ni fundisho kwa wengine watakaoendelea kunifatilia.... kisha akarudi nyumbani kwake.. hakutaka tena kuendelea kuwarudisha misukule wale usiku huo. aliamua akapumzike...kisha ataendelea na kazi hiyo kesho... ni kitendo cha sekunde alikuwa tayari kafika nyumbani kwake..... akapanda kitandani akalala...

*************

asubuhi palipo kucha sudy akiwa anafanya usafi nje ya nyumba kutokana siku hiyo ilikuwa jumamosi hivyo ni siku ya mapumziko sudy hakwenda shule siku hiyo... alidamka mapema na kuanza kufanya usafi wa mazingira yanayoizunguka nyumba yao... mara ghafla aliona mwanamke mzee akija upande wa nyumba yao... bibi huyo alipofika alimuulizia mzee mkumbo... sudy hakusita akaenda kumuamsha babu yake... mzee mkumbo alimkaribisha bibi huyo sebuleni..
kisha bibi huyo alimpa taarifa kuwa mtoto wako amefariki... usiku wa kuamkia leo....
kumbe mzee mkumbo alimbebesha mimba bibi huyo miaka 40 iliyopita na kumtelekeza bibi huyo aliamua kukimbilia kijiji cha jirani ili kuficha aibu ya kubeba mimba bila kuolewa kipindi hicho alikuwa na miaka 19.. mzee mkumbo hakuwahi kumuona huyo mwanae wa nje.. kwa hiyo yule aliyekuwa akipambana nae usiku wa jana na kuondoa uhai wake.. kumbe alikuwa ni mtoto wake wa damu. ....
bibi yule alitoa picha ya huyo mtoto wake na kumuonesha mzee mkumbo....
mzeee mkumbo alistahajabu sana kuona ile picha si mwingine alikuwa mganga maziku.

Mzee mkumbo macho yalimtoka baada ya kusikia taarifa hiyo...... alisikitika na kujutia sana......baada ya lisaa limoja kupita bibi yule aliondoka... sudy alistahajabu kumuona babu yake akiwa katika hali ya majonzi alipojaribu kuuliza mzee mkumbo hakujibu kitu chochote alibaki kimya.... taratibu za mazishi zilifanyika...... mzee mkumbo alifunga safari kuelekea kule kijiji cha jirani ili kumzika mwanae mganga maziku.......alipofika huko taratibu za mazishi ziliendelea... mzee maziku alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu..alijuwa wazi kuwa nafsi ya mganga maziku ipo mule ndani ya kibuyu...na akirudisha nafsi ile ili iungane na mwili wa maziku inamaana atabainika kwamba yeye ndiye mchawi aliekuwa akiwauwa wanakijiji kichawi na kuzifungia nafsi zao ndani ya kibuyu ili watu wale wageuke misukule na kumtumikia katika shughuli zake mbalimbali... aliingiwa na wasiwasi kisha akajisemea moyoni natamani dana urudi tena katika uhai lakini wananzengo watanitenga na kunifukuza kijijini endapo nitakapotoa nafsi yako ndani ya kibuyu nafsi nyingine pia zitatoka...
ilipofika majira ya saa saba mchana wanakijiji wa hicho kijiji cha jirani waliuaga mwili wa marehemu mganga maziku... watu walikuwa wengi karibia kijiji kizima walimpenda aliwasaidia kwa mambo mengi pia alikuwa mpenda haki.... hakika mganga maziku alikuwa kipenzi cha watu. walijiandaa kuelekea makaburini ili kumzika mganga maziku"""mzee mkumbo ..

*****************

kule nyumbani kwa mzee mkumbo... sudy aliona huo ndio muda sahihi wakufungua kibuyu kile ili zile nafsi zilizotoka siku ile alipo dondosha kibuyu zirudi ndani ya kibuyu"""" sudy alifanya hivyo huenda babu yake akafurahi baada ya kukuta nafsi hizo zimerudi ndani ya kibuyu... kwa sababu hawaongei vizuri yeye na babu yake kama zamani... sudy alizoea kumuona babu yake akifurahi muda wote pia alipenda hadithi za babu yake lakini sikuhizi hasimuliwi tena.. sudy aliamua kuingia chumbani kwa babu yake...alivuta ungo uliokuwa chini ya uvungu wa kitanda anacholalia babu yake.... alikiona kibuyu alikichukua kwa ujasiri siku hii hakuogopa wala hakuwa na wasiwasi wowote... hata yeye alijishangaa kuwa katika hali hiyo... alikinyanyua kibuyu kisha akaanza kufungua kile kipande cha kaniki nyeusi kilichokuwa kimefungwa upande wa juu ya kibuyu hicho...... kabla hajamaliza kukifungua kibuyu kile kilimponyoka na kudondoka chini kikapasuka vipande viwili!!!! ikawa ndivyo sivyo alivyokuwa amekusudia...... moshi ulianza kutanda ndani ya chumba kile huku vimvuli vya binadamu vikitokea pale chini kibuyu kilipodondokea na kupasuka"" sudy aliogopa alitoka chumbani akaelekea upande wa nje..... baada ya muda kidogo moshi ule ulikatika...ghafla walianza kuonekana watu wakitoka nje kupitia mlango wa mzee mkumbo.... watu hao walionekana kuwa na makucha marefu na nywele ndefu..... watu hao walitoka mfululizo aisee walikuwa ni wengi sana na kila mtu alipotoka nje alistahajabu kujiona katika hali ile ya kuwa na makucha marefu na nywele mdefu.... watu hao walipata fahamu baada ya kibuyu kuvunjika.... baada ya lisaa limoja mfululizo watu wale waliacha kutoka nje kutokea upande wa ndani ya nyumba ya mzee mzee mkumbo......wanakijiji walijazana kuizunguka nyumba ya mzee mkumbo walistahajabu sana kumbe mchawi alikuwa ni mzee mkumbo.... mbona alionesha ushirikiano kwa kila jambo hapa kijijini loh!! ((UMDHANIAYE NDIYE KUMBE SIYE)) alisikika mama mmoja wa wanakijiji akisema hivyo....mwenyekiti wa kitongoji alimuhoji sudy""" sudy hakutaka kudanganya alimueleza kila kitu... wanakijiji walimuonea huruma sudy pia walimpongeza kwa sababu bila yeye wasingeweza kuwaona ndugu zao waliofariki miaka mingi iliyopita""" kumbe mzee mkumbo aliwauwa kichawi na kuzifungia nafsi zao ndani ya kibuyu ili misukule hao wamtumikie kwenye shughuli zake...

*********

kule makaburini walipotaka tu kuliweka jeneza ndani ya kaburi walisikia mganga maziku akigongagonga jeneza huku akitoa sauti nifungulieni"" watu waliogopa walikimbia kila mtu njia yake wengine wakisema maiti imefufuka... lakini mzee mkumbo alibaki hakukimbia yeye pamoja na mama yake mzazi mganga maziku.
mzee mkumbo alistahajabu sana akajisemea moyoni haiwezekani lazima kunakitu hapa hakijaenda sawa kule nyumbani kwangu.... mzee mkumbo aliingiwa na wasiwasi wa hali ya juu.. alilikaribia jeneza na kulifungua......kumbe mganga maziku alirudi katika uhai baada ya nafsi yake kuungana na mwili ni baada ya kibuyu kuvunjika nafsi yake ilikuwa huru angani ikitafuta kiwiliwili cha mganga maziku ........mganga maziku alistahajabu kumuona adui yake kafungua jeneza alipotoka ndani ya jeneza alistahajabu kumuona mama yake mzazi..... kisha bibi yule alimwambia mganga maziku mwanangu huyu ndiye baba yako wa damu"""" maziku hakuwa na namna ilibidi awe mpole.... alimsamehe baba yake wakakumbatiana huku machozi yakimtoka mganga maziku.. waliondoka makaburini hapo.. kisha maziku na mama yake walikwenda nyumbani..
mzee mkumbo aliondoka na kurudi kwake... alipofika jirani na nyumbani alistahajabu kuona mkusanyiko wa watu nyumbani kwake... akiwa anatahamaki mara ghafla wanaume wawili walimnasa na kumpeleka pale kwenye mkusanyiko wa watu nyumbani kwake... mwenyekiti wa kitongoji aliamuru mzee mkumbo atengwe na afukuzwe kijijini hapo kisha wakaichoma moto nyumba ya mzee mkumbo.....baada ya mzee mkumbo kuona hivyo presha ilimpanda akadondoka chini na kupoteza maisha..... sudy alichukuliwa na mwenyekiti wa kitongoji akawa anamlea na kumsomesha....

*MWISHO WA SIMULIZI YA KIBUYU CHA BABU* 

Post a Comment

Previous Post Next Post