MSIBANI TANGA 09

Jun 20, 2021
Nilitembea kwa mwendo wa haraka haraka kuelekea sehemu nisiyoijua, ilikuwa saa nne na ushee.



Kwa bahati nzuri niliona pikipiki inapita kwa mbali nikapiga kelele



"Oyaaa......Boda bodaa......oiii" Nilisema na kupiga miluzi ya nguvu "Fyyuuuuuu.......fyuuuu" Ndo nikaona pikipiki imepunguza kasi nikajua amenisikia



Kweli aliendesha mpaka nilipokuwa, akafika pale 

"Oi kaka" Nilisema huku nikihema



"Vipi?" Alisema huku akinikagua



"Poa, nataka kwenda kigongoi kaka" Nilisema



"Kigongoi? mbona mbali usiku huu babu?" aliniuliza



"Nifanyie wepesi kaka"



"Nipe mwekundu nikupeleke" Aliniambia



"Nina minane kaka nipeleke basi"



"Ok, kwea twenzetu" Aliniambia



"Poa poa" Nilisema huku nikipanda pikipiki akaigeuza na safari ikaanza kueleka Kigongoi



Aisee nilijuta, tamaa za mwili ziliniponza, baadaye nilifika salama, nilipofika sikuamini, nilimlipa huku nikiapa kwamba kesho yake lazima niende zangu Dar siwezi mimi kukutana na magumu kiasi hicho bado niendelee kutaka kukaa tanga



Msibani watu hawakuwepo wengi walikuwa ni wachache sana, ambapo Aziz hakuwepo pia



Nilienda hadi nyumbani kabisa na kuulizia



"Samahani ninaweza kumpata Aziza hapa?" Niliuliza nikaona mama mmoja amenishangaa



"Aziza?" aliuliza huku akishika kiuno



"Ndio"



"Kwani wewe nani?.....nakuuliza wewe nani?" Alianza uswahili mama yule



"Mimi rafiki yake, nilikuwa nataka nimuombe aniwekee simu chaji maana imezimika" nilisema



"Ok, hayupo, labda uende kwake huko sio hapa halafu mimi ni mama yake huyu binti yangu ameanza kuwa na urafiki uliokithiri na wanaume, pumbavu" alisema kwa hasira mwanamke yule.



Niliondoka kwa uoga nikaenda hadi kule nilipolala jana yake ambapo alikuwa akiishi Aziza na mdogo wake Ilham, niligonga mlango ngo ngo ngo



Ghafla akafungua yule rafiki yake Ilham, "Mambo" Alinipa salamu



"Safi hujambo?"



"Sijambo karibu" Alisema kwa tabasamu ndipo nikauliza



"Aziza yupo humu?" niliuliza



"Hapana nipo mwenyewe" Aliniambia, lakini kwa haraka haraka nilipofikiria huyo hata sina mazoea naye hata jina simjui, nisingeweza kumuachia simu



"Ok" Nilisema



"Ila kwao ni nyumba ya tatu tu hapo mbele nafikiri anaweza akawa kwa mama yake" alisema akinionyeshea njia ya kwenda kwao ndipo nikaondoka nikiuliza



Nilipofika nlibisha hodi mara tatu lakini hakuna aliyeitika, ikabidi nigeuke kurudi kule nilipotokea ila nilipogeuka tu hivi nikakutana uso kwa uso na yule mwanamke ambaye alisema ni mama yake



"Eeeh.....umenishtua!" nilisema



"Samahani" Alisema mama yule "Umemkuta?" Aliniuliza



"Hapana mama, sijui yuko wapi.....naomba uniwekee simu chaji basi" Nilimuambia



"Una chaja?" aliniuliza



"Hapana sijabeba ila ni chaja yoyote ya simu janja (Smartphone) inaweza kuchaji hapa" nilisema



"Embu" Aliniambia nimpatia simu halafu akafungua mlango na kuingia ndani "Ngoja niangalie kama ya kwangu itachaji" alisema na kuelekea ndani



Nilibaki nje nikisubiri majibu, kweli baada ya dakika moja alirudi mlangoni na kunitazama



"Inapeleka?" Nilimuuliza akatikisa kichwa kwa ishara ya kukubali "Asante" Nilisema huku nikigeuka kuondoka



"Unaitwa nani?" Aliniuliza mwanamke yule



"Jawabu" Nilitaja jina



"Ndo jina lako, Jawabu au?"



"Ndio"



"Ok.....aamhhh....Karibu ndani" Aliniambia



"Aam...mh hapana" Nilisema



"Njoo ule bhana.....chakula kipo au ushakula?" Aliniuliza, nikawaza ni kweli nina njaa ila sasa nisingeweza kula maana nilikuwa simjui



"Karibu unaogopa nini au unaenda kulala wapi mbona unaonekana kama vile mgeni huku?" Aliniuliza na mimi nikaanza kushawishika kweli kwa sababu nje kuna mbu halafu mwenyewe nina njaa, halafu daaah Aziz sijui alipo



"Baba mwenye nyumba yupo?" Niliuliza



"Ahaha.....acha mambo yako bwana mimi sina mume nimejenga hii peke yangu embu njoo mbona unakuwa muoga au hautaki kula" aliniuliza



"Aamh....ni kweli nina njaa ila mmh"



Mama yule alitoka akanishika mkono na kuanza kunivuta kwa nguvu "Njoo basi mbona muoga sana jamani huku ni Tanga hupaswi kuwa muoga njoo ule vyakula vyote"



Nilijafanya kukaza kaza lakini mwisho wa siku tuliingia ndani, na aliniketisha na kufunga mlango. Nilihema kwa uoga



"Umesema unaitwa Jaribu?" aliniuliza



"Haha....hapana ni Jawabu"



"Ok wait nikupakulie chakula ule sawa?" Aliniambia mi nikatikisa kichwa.



Baada ya dakika tano alirudi akiwa na sahani iliyojaa wali na nyama za kutosha juu huku mkono wa kushoto ameshikilia blauri ya maziwa halafu kilichonishangaza zaidi ni kwamba alikuwa ameshavua lile dera na kujifunga khanga nyepesi halafu alipofika alipiga magoti na kuniwekea mezani



"Karibu mwanangu.... Kula hiki chakula halafu mimi naenda kuoga ili uje ule chakula maalum" alinipa sentensi yenye utata nikabaki nashangaa.....ITAENDELEAAAA

Je ni chakula gani hicho maalum?... Usikose 

Post a Comment

Previous Post Next Post