MOYO WANGU 01

Ilikua siku ya jumamosi ambapo yalikua majira ya saa kumi jioni ambapo wingu jepesi lilikua likijikusanya taratibu katika anga la jiji la Dar es salaam huku kukiwa na kajua kwa mbali kakiangaza katika jiji hilo, wananchi wengi waliifurahia hali hiyo kwani wingu lile lilikuwa limeambatana na hali ya ubaridi, hali hiyo ilipunguza kadhia ya joto ambayo ilikua imewapata wananchi wa jiji hilo muda mfupi kabla ya hali hiyo ya wingu nene yenye dalili za mvua kutokea. Wakati hali hiyo ikiendelea, hali ilkua tofauti kidogo katika jumba moja lililopo maeneo ya kigamboni, katika jumba hilo kijana ambae alikua na makadirio kati ya miaka 24 mpaka 30 alikua katika bwawa la kuogelea(swimming pool) akiogelea pamoja na kurushiana maji na mwanadada ambae nae kwa makadirio alikua na umri kati ya miaka 22 hadi 25, kwa kuwaangalia tuu kwa haraka walionekana ni mtu na mpenzi wake, naam hawakua wengine bali ni Sheby na mpenzi wake Warda, walikua wapo katika jumba la Sheby ambalo alizawadiwa na uongozi wa TRA hasa kutokana na utendaji wake na uhodari wake katika utendaji wa kazi katika idara hiyo, Sheby aliajiriwa TRA kipindi akiwa na miaka 20 ambapo alikua amehitimu shahada yake ya kwanza ya IT katika chuo cha Udsm kilichopo katika jiji hilo la Dar es salaam, kutokana na kuibuka kinara katika masomo yake katika chuo hicho ndipo mkurugenzi wa TRA Mr Yusufu alipoamua kumuajiri katika idara hiyo pia ni kutokana na umaarufu wa baba ake ambaye alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani aliyestaafu Mr Husein Bahi, baada ya kufanya kazi kwa takribani miaka miwili, ndipo Uongozi wa TRA ulipomzawadia jumba hilo lililopo Kigamboni alizawadiwa hivyo kutokana na utendaji wake pamoja na uaminifu wake kazini, Warda ambae alikua ndio mpenzi wake Sheby, yeye alikua ni secretary katika ofisi za GSm Mikocheni, Warda na Sheby walikutana coco beach ambapo kila mtu alikua amekwenda maeneo hayo sababu ya kurefresh pamoja na kuogelea, hapo kila mtu alivutiwa na mwenzake na hapo ndio ikawa mwanzo wa mahusiano yao, sheby yeye hakua na ndugu yeyote yule kwasababu yeye alizaliwa pekee yake kwao na baba ake alikuwa ameshafariki, upande wa warda yeye alikuwa na familia yake katika jiji la arusha

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post