MOYO WANGU 31---32---33

Mida ya saa tatu asubuhi maeneo ya karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya ya kigamboni maeneo ya geza ulole, watu walikuwa wamejikusanya katika mfumo wa duara kuonyesha kwamba kuna kitu walikuwa wamekizunguka…. “Eti kaka kuna nini hapa mbona watu wengi halafu pale inaonekana kama kuna kitu wamekizunguka?” alikua ni dada mmoja akimuuliza jamaa mmoja “Aaa inasemekana hapo kuna jamaa wanne wamekutwa wamekufa nab ado haijajulikana kama walishambuliwa na majambazi au la na inavyosemekana kulikua na usafiri ambao walikuwa wakiutumia umeibiwa muda sio mrefu” alijibu yule jamaa “Jamani mbona watu hawana utu yani angalia vijana wa watu walivyopendeza na wanaoekana bado wadogo kabisa lakini wamewaua bila hata huruma” ilisikika sauti ya mama mmoja kutoka katika lile kundi la watu, haikupita muda polisi walifika eneo la tukio na kukuta waandishi wahabari wakiendelea kuchukua video na picha mbali mbali za tukio hilo, polisi waliwasogeza watu na haikupita hata dakika moja ambulance mbili zilifika na kuzichukua maiti zile na kuzipeleka hospitali ya taifa ya muhimbili huku wakiwaacha polisi wakijaribu kuchukua maelezo kwa wananchi wale waliokuwa wamefika wakwanza katika eneo lile la tukio…

Siku hiyo sheby aliwahi mapema na kumuaga mpenzi wake warda ambae hakutaka tena kufanya kazi na alimuambia sheby kuwa anataka awe mama wa nyumbani tuu haitaji tena kufanya kazi, na sheby kwa kua alikua akimpenda sana alikubaliana nae jinsi anavyotaka, basi alimuaga mpenzi wake na kuingia ndani ya gari lake aina ya prado na kuelekea eneo ambalo alikuwa anafanyia kazi, ilipofika mida ya saa nne wafanyakazi hukutana sehemu moja na kupumzika kwa muda wa nusu saa huku wakiangalia taarifa mbali mbali za habari, mr yusufu alipofika eneo lile alichukua rimoti na kuweka TBC (Tanzania broadcasting company yani shirika la habari la Tanzania) ambapo walikuta kuna kipindi kinaishia na hazikupita hata dakika mbili walisikia… “Breaking newz, watu wanne wakutwa wameuwawa maeneo ya karibia na geza ulole huku miili yao ikionekana kutokujeruhiwa, muandishi wetu steven moyo anataarifa zaidi, steven…” “

#itaendelea 

Breaking newz, watu wanne wakutwa wameuwawa maeneo ya karibia na ofisi ya mkuu wa wilaya geza ulole huku miili yao ikionekana kutokujeruhiwa, muandishi wetu steven moyo anataarifa zaidi, steven…” “Katika hali ya kushangaza kabisa maeneo haya ya geza ulole miili mine ya watu imekutwa ikiwa haina uhai na inavyosemekana ni kwamba huenda kabla ya marehemu hao wakati wakiwa bado hai walivamiwa na watu wasiojulikana na kuwakatisha maisha yao, lakini katika hali ya kustaajabisha zaidi miili hiyo inaonekana kutokuwa na jeraha la aina yeyote kama inavyoonekana hapa na tukio hilo linahusishwa na masuala ya kishirikina, aliongea steven moyo huku picha za marehemu hao zikioneshwa, lakini hata hivyo miili hiyo imepelekwa hospitali ya taifa ya muhimbili kwaajili ya uchunguzi zaidi, nikiripoti kutoka eneo la tukio, mimi ni steven moyo wa TBC” bwana steven alimaliza kuripoti taarifa hiyo… John alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuona picha za vijana aliyewatuma kumuua sheby wakiwa hawana uhai lakini alilificha hilo bila kujua kua sheby alishamuona jinsi alivyopatwa na mshtuko, sheby alitabasamu na kujisemea moyoni “Pole john kwakua choo ulichoingia ni choo cha kike kwani ni sawa utumbukie katika bwawa ambalo limejaa mamba wenye njaa na ukajipa matumaini kuwa utatoka salama” na hapo aliamka na kuelekea ofisini kwake kuendelea na kazi… sheby aliendelea na kazi zake kama kawaida na baadae muda wa kutoka ofisini ulifika, sheby alifunga makabrasha yake na kuyaweka sehemu husika na baada ya hapo alirudishia mlango wake vizuri, sheby alitoka ofisini na kuelekea sehemu ambayo alipaki gari lake aina ya Mercedez benz nyeusi lakini kabla hajafika maeneo ya parking alisikia mtu akimuita, alipogeuka alimuona John akija kwa kasi eneo lile alilokuwepo na ilionekana dhahiri kwamba john alikua akija kwaajili ya shari hali iliyomfanya sheby atabasamu na kujiandaa vyema kwa jambo lolote ambalo lingetokea, lakini John baada ya kufika eneo alilokuwepo sheby alitabasamu kwa tabasamu feki na kabla hajaongea kitu sheby alimsabahi….

#itaendelea 

Mambo vipi john?alizungumza sheby “Poa tuu nambie muuwaji?” aliongea John kwa sauti iliyochanganyikana na ghadhabu ya hali ya juu “Hahaha!! Angalia bwana mdogo kauli zako zisije zikakuponza na kukugharimu” alizungumza sheby kumuambia John katika hali ya ustaarabu na umakini wa hali ya juu sana “Acha kunitisha kunguni wewe, kwani utanifanya nini mbw….” Alizungumza John lakini kabla hajamalizia kauli, ngumi nzito na yenye ujazo kutoka kwa sheby ilitua vyema katika shavu lake na kusababisha moja kati ya jino lake kudondoka kutokana na uzito wa ngumi ile.. “Huwa sipendi kubishana na watoto wa mama ambao wanajua kula na kunywa na kunya tuu, hawajui kingine chochote..” alizungumza sheby na kumuambia John na baada ya hapo alifungua mlango wa gari lake na kuingia ndani, alifunga mkanda na kuwasha gari lake na safari ya kuelekea nyumbani kwake ilianza huku akimuacha John akigugumia maumivu ya kung’ooka kwa jino pasipo ridhaa yake jambo ambalo alilisababisha mwenyewe kutokana na kauli zake chafu kwa mtu asimfahamu undani wake, hakika john hakuamini kama ile ngumi amepigwa na sheby… “Au ameshika jiwe akanipiga nalo nini? lakini mbona sikumuona akichukua hilo jiwe, au jamaa atakua mchawi nini?” ni mambo ambayo alikuwa akiyawaza John kotokana na uzito wa ile ngumi ya sheby, alihisi huenda ile ngumi amepigwa na mpiganaji maarufu wa mieleka bwana John Cena, hakika alipagawa na alikua kwenye maumivu makali mno, ilimbidi aondoke na kuelekea kwake maeneo ya mnazi mmoja ili angalau akanunuepanadol ili akapunguze maumivu ambaye alikua akiyasikia..
***************
 Mida ya saa moja kasoro usiku sheby akiwa ndani ya gari lake aina ya Mercedez benz nyeusi alikua mbele ya geti kubwa jeusi, geti hilo lilikua la kisasa kweli kwani lilikua likifunguliwa na kufufungwa kwa remote, Sheby alitoa kirimote kidogo na kukibonyeza ambapo geti hilo lilifunguka, aliingiza gari ndani na kulifunga geti lile, baada ya kuliweka gari katika maeneo ya parking yaliyopo mle ndani, sheby alishuka katika gari na kuelekea ndani ambapo alilakiwa na harufu nzuri ya chakula ambacho warda kwa muda huo ndo alikuwa anakitenga mezani… “Waooow!! Husband huyoo”

Post a Comment

Previous Post Next Post