MOYO WANGU 28---29---30

Sheby alifungua boneti la gari lake akajifanya kuzuga kama gari lake limeharibika na alifanya hivyo ili kuwatega wale jamaa na mida hiyo ilikuwa yapata saa moja kasoro na giza lilikua limeshaanza kuchukua nafasi yake, na kweli alifanikiwa kwani wale jamaa walikuja na kupaki nyuma ya gari lake na hapo wakashuka jamaa wawili na wawili wakabaki kwenye gari, jamaa wale walimuona sheby ni mzembe na ndio maana waliwaacha wenzao wawili washuke peke yao wakiamini kwamba watakamilisha kazi ya kumuondoa sheby duniani, jamaa wale wawili walisogea mpaka eneo alilokuwa sheby na kujifanya kumuuliza alikuwa amepatwa na nini.. “Vipi kaka gari lako limepatwa na tatizo gani?” mmoja wa jamaa wale alimuuliza sheby swali.. “Kwani niliwapiga mkono gari lenu na kuwaambia kuwa nataka masaada, mnaweza mkaendelea na safari yenu kwani sihitaji msaada kwa mtu yeyote” alijibu sheby kwa utaratibu huku akijifanya kuonesha hali ya uoga ili kuwateka kisaikolojia wale jamaa, na alifanikiwa kwa asilimia tisini “Hahahahaha safi sana kijana, sawa kama hutaki msaada wetu sisi tunataka roho yako” alicheka jamaa mmoja kisha kufuatishia na maneno yake ya kifedhuli
 “M..na..see…ma m.. m..nataka roho yangu?” aliongea sheby kwa sauti kuigiza ya kitetemeshi na kuigiza hali ya wasiwasi “Unajifanya unajua sana kufanya kazi sasa siku zako za kuishi zimeisha na sasa tumekuja kuichukua roho yako” waliongea wale jamaa utadhani wao ndio malaika mtoa roho.. “Nani kawatuma jamani mje mniue na nimewakosea nini?” aliuliza sheby kwa hali ya kudadisi na kupata uhakika zaidi kama kweli ni john ndie aliyewatuma, na bila kujua kua lile lilikuwa ni swali la mtego jamaa mmoja akajibu “Ndio john katutuma yule muhasibu msaidizi, sema kama unalingine” alijibu jamaa mmoja kwa kejeli bila kujua kuwa ameshaharibu mambo “Sawa mnaweza kufanya mlichokusudia” alizungumza sheby kwa utulivu huku akisimama kwa umakini wa hali ya juu… Jamaa mmoja alikuja kichwa kichwa kuja kumvaa sheby lakini sheby alimuona vyema, wakati jamaa amemkaribia sheby, alimkwepa jamaa na kumsukumizia konde moja zito katika tumbo lake hali iliyopelekea jamaa kusimama 

#itaendelea 

Sheby alimkwepa jamaa na kumsukumizia konde moja zito katika tumbo lake hali iliyopelekea jamaa kusimama na kabla hajakaa vizuri konde jingine zito lilitua katika shingo yake na jamaa alianguka chini na mwili pamoja na roho vilitengana na jamaa akafa papo hapo bila kelele, naam hilo lilikua pigo maridhawa kwaajili ya kuua, sheby alipompiga jamaa konde la tumbo alisababisha utumbo wa jamaa upande juu na wakati huo alisababisha mishipa ya shingo ya jamaa kusimama na kukaza na alipomalizia kwa konde la shingo hapo aliipasua mishipa hiyo ya shingo na baada ya hapo kinachofuata huwa ni kifo cha kimya kimya na huwezi hata kupiga kelele au yowe la maumivu, na ndivyo ilivyokuwa kwa jamaa yule kwani alikufa bila kufurukuta wala kupiga kele ya aina yeyote… Yule boya mwingine baada ya kuona mwenzake ameanguka chini bila kujua kuwa mwenzake tayari alikua ameshakufa, nae alikuja kwa papara kwaajili ya kumvaa, sheby alimuona vyema na alipomkaribia, sheby aliruka juu na kutanua miguu yake na wakati anashuka chini pigo moja aina ya flight kick lilitua vyema katika shingo ya yule boya ambae alipiga yowe la maumivu na kutua chini huku mwili ukiwa hauna uhai,sheby aliamua kumpiga jamaa yule pigo la flight kick ili kuwafanya wale waliokuwa wako ndari ya gari waweze kushuka wote, na kweli ukelele alioutoa yule jamaa kabla ya kufa ulisababisha wale jamaa washuke kwenye gari ili kwenda kushuhudia ni nini kimetokea, walipofika eneo ambalo miili ya wenzao ilikua imelala wakahamaki na kusimama juu kwa haraka, ni kama sheby alikua akisubiri jamaa wale wafanye vile kwa aliruka juu na kuachia mapigo mawili aina ya double kick ambayo yalitua vyema katika vifua vya wale jamaa na kuwapeleka chini,

#itaendelea 
wakati wakijianda kuamka sheby afyatuka kama mshale na kuruka juu na wakati anashuka chini alikua ametanguliza goti lake ambo lilitua vyema shingoni mwa jamaa mmoja na kilichosikika hapo ni mlio wa shingo kumaanisha kuwa ilikua imevunjika, wakati jamaa mwingine akitahamaki kwa kile kilichotokea, sheby aliruka serekasi maridhawa na alipotua tua chini alitua huku amechuchumaa na wakati huo guu lake la kulia lilikua mbele pigo hilo lilitua vyema katika taya za yule jamaa na kusababisha ateme meno kumi na mbili chini, wakati bado jamaa akiugulia maumivu ya kuvunjwa meno, sheby alivirika kama tairi na kutua nyuma ya yule jamaa hapo alifyatua mikono yake na kuvunja shingo ya yule jamaa na habari yake ikawa imeishia pale, ndani ya dakika kumi na tano tayari sheby alikuwa ashakatisha uhai wa vijana wanne ambao walitumwa na john, sheby aliwasachi wale vijana na alifanikiwa kupata simu, aliangalia simu ya mwisho kutoka na hapo aliona jina lililoseviwa joo de boss, alibonyesha kitufe cha kuruhusu simu itoke na kuiweka sikioni na baada ya muda simu ilipokelewa upande wa pili… “Not easy like that, am not of that kind so take care” aliongea sheby na kukata simu bila ksubiria majibu na maneno aliyozungumza sheby alimaanisha kuwa “Sio kirahisi hivyo, mimi sio wa aina hiyo hivyo kuwa mwangalifu” John alibaki kujiuliza maswali huyu aliyempigia simu ni nani, aliwaza huenda wale jamaa watakuwa wamemgeuka na wamemuibia pesa zake bila kujua kuwa jamaa wale walikuwa washapoteza maisha, alijaribu kupiga ile simu lakini alikutana na sauti nyororo ya mwanadada ikimwambia samahani namba unayopiga kwa sasa haipatikani tafadhali jaribu tena baadae, hakika alichanganyikiwa…. Sheby baada ya kumaliza kuongea na ile simu aliitupa chini na kusababisha betri kutoka katika ile simu, alirudi katika gari lake na kufunga boneti na baada ya hapo aliingia ndani ya gari na kuligeuza na safari ya kuelea kwake ilianza

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post