MOYO WANGU 25---26----27

“Daaa aisee inasisimua sana baba” alizungumza sheby
“Ndo hivyo mwanangu” alizungumza mr Yusufu na kumsihi sheby amalizie chakula kwa muda wa chakula cha mchana ulikuwa unakaribia kuisha, hivyo wafanye haraka ili wakaendelee na kazi…

Wakati sheby na Mr Yusufu wakiwa wanamalizia chakula ili wawahi kuendelea na kazi, upande wa pili katika mgahawa ule ule alikuwepo John ambae alikua ni muhasibu msaidizi akiwa kazungukwa na vijana wanne ambao miili yao ilikuwa mikubwa na imejengeka kwa mazoezi, john pamoja na vijana hao walikuwa wakipanga mikakati ya kumuondoa sheby duniani….
“Mnamuona yule jamaa ambae amevaa shati la mikono mirefu la rangi nyeupe na suruali nyeusi?” alizungumza john kuwauliza wale jamaa ambao alikuwa amekaa nao..
“Ndio si yule pale kwenye ile meza ambayo wamekaa wawili tuu” wale jamaa walijibu kwa pamoja huku wakionesha meza ambayo alikuwa amekaa sheby na mr Yusufu “Ndio huyo huyo, huyo ndiye sheby ambae nataka mumpoteze duniani, tayari nimeshawaandalia gari pamoja na kiasi cha milioni mia moja kama mkikamilisha zoezi hilo na pia hii ni advance na mkimaliza zoezi hilo nitawamalizia kiasi kilichobaki” aliongea john huku akiwakabidhi wale jamaa bahasha ya kaki ambayo ilikuwa na kiasi cha shilingi milioni arobaini (dollar elfu 20) “Sawa boss tumekuelewa, na tunakuhakikishia kuwa huyo jamaa hatoliona jua la kesho asubuhi” waliongea jamaa wale na kumuhakikishia john kuwa mpaka kufikia siku ya kesho asubuhi kazi yake itakuwa imeshakamilika hivyo aandae kitita kilichobakia kiwe tayari. Baada ya kumaliza mazungumzo hayo, john alitoka katika mgahawa huo na kuelekea ofisini kuendelea na kazi huku akiwaacha wale jamaa wakiendelea kumsomea ramani sheby…Wakati sheby alipokuwa akiendelea kula kuna muda aligeuka upande wake wa kulia na kumuona john akiwa na wale jamaa wanne, hapo sheby machale yalimcheza na alihisi kuna kitu kibaya john alikua akitaka kumfanyia kutokana na muonekano wa wale jamaa,

#itaendelea 

Sheby baada ya kuwaona aliamua kukaa kimya na kujifanya kama yuko bize anaongea na mr yusufu, na mara kwa mara alikuwa akiibia kuwaangalia kina john walikuwa wanafanya nini mpaka pale john alipoondoka nay eye ndipo alipomalizia chakula chake haraka na baada ya kumaliza aliondoka na mr yusufu kuelekea ofisini ili kuendelea na majukumu ya kulijenga taifa, baada ya kufika ofisini mr yusufu alielekea sehemu anayofanyia kazi na sheby alipitia katika ofisi ambayo john huwa anakaa, aligonga na kuruhusiwa kuingia, john alipomuona sheby alipendezesha uso wake kwa tabasamu feki huku akisema kimoyomoyo
“we jifanye tuu tutaona kama kesho utaliona jua la asubuhi”… “Habari yako bwana john?” alianza kusabahi sheby kumwambia john “Salama tuu sijui nikusaidie nini mkuu?” alijibu john kwa kejeli “Unajua bana ukitaka kumjua mtu upande wake wa pili jaribu kuingilia na kufuatilia mienendo yake na hapo ndipo utakapo jua undani wake na upande wake wa pili upoje” alizungumza sheby kwa hali ya utulivu na umakini wa hali ya juu “Unamaanisha nini rafiki yangu sheby?” aliuliza john kinafki hali ya kuwa hakujua kuwa shebt tayari ameshaelewa kwamba kuna kitu kibaya alitaka kumfanyia… “I mean take care and watch out your steps because it will cost you” aliongea sheby kumwambia john akimaanisha kuwa “john awe muangalifu na nyendo zake kwani zinaweza kumgharimu” “Okay thank you for your advice but its too late” alizungumza john kwa hali ya dharau kumwambia sheby akimaanisha kuwa “Nashukuru kwa ushauri wako lakini umechelewa sana” “Okay we shall see” alijibu sheby akimaanisha “Sawa tutaona” na baada ya hapo hakutaka kusubiri neno bali alitoka katika ofisi ya john na kuelekea katika ofisi yake huku akiwa amechukia kupita kiasi… “We subiri mpuuzi huyu si ananichukulia mimi maandazi sana, ananichukulia mimi mtoto wa kishua mchele mchele, hajanijua vyema kuwa nilikuwa muhuni niliyeshindikana sasa subiri nitamuonesha kwamba mimi ndiye sheby nilie kulia tandale uswazi” aliwaza sheby wakati akiwa ameketi katika kiti chake ndani ya ofisi anayofanyia kazi,

#itaendelea 

baada ya kuwaza sana aliendelea na kazi zake mpaka muda wa kutoka ofisini ulipofika ambapo alitoka na kufunga vizuri sehemu anayofanyia kazi na baada ya kumaliza alielekea katika ofisi ya mr Yusufu na kumuaga, alipomaliza kumuaga alitoka mpaka katika parking ya magari ambapo aliingia kwenye gari lake na safari ya kuelekea kwake ikianza… Wakati sheby akiingia katika gari lake kwaajili ya kuondoka, wale jamaa wanne ambao waliagizwa na john kuhakikisha kuwa sheby anapoteza maisha siku hiyo walikuwa wamepaki gari yao aina ya corolla wakimfatilia sheby kwa ukaribu na wakati michael alipokuwa anaondoka nawenyewe waliondoa gari lao na kuanza kumfatilia sheby nyuma nyuma bila kustukiwa, sheby wakati anaendesha gari lake aliweza kugundua kuwa kuna gari ilikua ikimfuatilia na ili kuthibisha hilo alipunguza mwendo na kuwasha hindcator kuruhusu gari hilo lipite lakini gari hilo nalo lilipunguza mwendo pia na dereva aliekuwa akiendesha hakutaka kumpita sheby na hapo ndipo sheby alipothibitisha kwa asilimia mia moja kuwa atakuwa anafuatiliwa... ************* ********** ********** Katika maisha yake siku zote sheby hakuwa mzembe, alishapigana sana ngumi mtaani hadi akafanikiwa kupata udhamini na kupelekwa nchini china katika jiji la hong kong ili kupata mafunzo zaidi na alifanikiwa kuhitimu mpaka mafunzo ya uninja ndipo aliporejea nchini Tanzania na kuendele na masomo yake… Vijana wale wanne waliokuwa wamejazia miili yao kutokana na mazoezi walizidi kumfatilia sheby bila kujua kuwa walikua wanajiingiza kwenye hatari ambayo hakuna hata mmoja wao ambae anaweza akafika salama, sheby aliendesha gari lake na alipofika karibia na anapoishi alipapita na kuendelea kwenda kama vile anaenda geza ulole, alifanya hivyo ili kuepusha mpenzi wake warda asije akapatwa na matatizo, baada ya kufika eneo ambalo lilikua halina watu na palikuwa na utulivu mkubwa sheby alipaki gari lake pembeni ya barabara na kushuka ambapo alienda mpaka sehemu ya mbele na kufungua boneti la gari lake akajifanya kuzuga kama gari lake limeharibika na alifanya hivyo ili kuwatega wale jamaa na mida hiyo ilikuwa yapata saa moja kasoro 

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post