pia nilijitahidi kukabiliana na madhara hayo ili yasije yakaendelea kutokea na nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia madhara hayo ambayo endapo yangetokea yangesababisha wewe kupata hali ya utasa ya kutoweza kumpa ujauzito mwanamke yeyote yule kwa kitaalam tunaita(infertility), sambamba na jitihada hizo pia ya kupasa kuacha kushiriki tendo la ndoa kwa muda wa miezi saba ili sehemu ambazo tulizifanyia matibabu katika vimirija hivyo viweze kupona kabisa, ila kama utakiuka hilo basi hautokuja kupata mtoto katika maisha yako yote, nafikiri utakuwa umenielewa vyema” dokta razaq aliweka nukta na kumeza funda la mate baada ya kutoa maelezo hayo marefu na yakueleweka pia…
“Ndio dokta nimekuelewa” alijibu mr Yusufu…
Mr Yusufu aliendelea kumsimulia sheby kuwa baada ya maelezo hayo ya dokta razaq, jopo lile la madaktari lilitoka na kumuacha yeye akipumzika na hapo alitafakari mambo mengi sana ambayo yalitokea katika maisha yake, mwisho wa yote alimshukuru mungu kwa kila lililotokea katika maisha yake…
“Pole sana baba, enhe baada ya hapo ikawaje?” alizungumza sheby na kumuuliza swali jingine mr Yusufu
“Niliweza kukaa hospitali kwa muda wa miezi sita ndipo hali yangu ilipotengemaa na hapo niliruhusiwa kuendelea na shughuli zangu, lakini kabla sijatoka hapo hospitali nilipitia ofisini kwa dokta hashimu ili kwenda kumpa shukrani pamoja na kumuaga, lakini nilipofika ofisini dokta hashimu alitaka nimsimulie maisha yangu kwa ufupi, niliweza kumsimulia na baada ya kumaliza simulizi hiyo dokta hashimu aliniambia haina haja ya kurudi nchini uingereza nibaki tuu Tanzania na nitaishi nae nyumbani kwake na pia atanisaidia kupata kazi ukizingatia vyeti vyangu vilikuwa na ufaulu wa hali ya juu, kwakua dokta hashimu alinibembeleza sana ukizingatia wema alionitendea niliamua kukubaliana nae na hapo nikaanza kuishi nyumbani kwa dokta hashimu maeneo ya kariakoo, wakati nikiwa nimemaliza wiki mbili tangu muda ambao niliambiwa na daktari nisishiriki tendo la ndoa, siku moja nilikua natembea tembea katika mitaa ya kariakoo,
#itaendelea
lakini nikiwa katika matembezi hayo nilikutana na msichana mmoja mrembo sana aliejitambulisha kwa jina la mery, ingawa ndio tulionana kwa mara ya kwanza kila mtu alivutiwa na mwenzake na kuanzia siku hiyo tukawa wapenzi, baada ya wiki mbili tangu tuanze mahusiano na mery, nakumbuka ilikua siku ya juma5 siku ambayo tulipanga na mery kukutana katika gesti moja iliyopo maeneo yale ya kariakoo ili tuweze kushiriki tendo la ndoa, siku hiyo nilimuaga dokta hashimu kuwa mida ya saa tisa nitatoka na kwenda kwa rafiki yangu na kwamba nitalala huko huko mpaka kesho yake ambapo dokta hashimu aliniruhusu bila ya kipingamizi ukizingatia tayari nilishakua mwenyeji katika maeneo hayo, basi siku hiyo mida ya saa tisa niliweza kukutana na mery katika gesti tuliyopanga kukutana na hapo tulishiriki tendo la ndoa na kutokana na papara zangu za kutokufanya tendo la ndoa muda mrefu, nilijikuta nikishiriki tendo la ndoa na mery pasipo kuvaa kinga(condom)” baada ya kufikia hapo Mr Yusufu alidondosha machozi kuonesha kuna jambo ambalo nilibaya lilimkuta hasa baada ya kushiriki tendo la ndoa na mery pasina kutumia kinga(condom)…
“Pole baba usilie, kwani ulipatwa na nini baada ya kufanya mapenzi na mery?” Sheby alimpa pole Mr Yusufu na kumtupia swali jingine
“Basi mwanangu baada ya kushiriki nae tendo lile asubuhi ya siku iliyofuata ambayo ilikua siku ya alhamisi niliweza kuacha na mery na kila mtu akaelekea eneo ambalo alikua akiishi, nilikaa kwa muda wa wiki mbili tu huku nikiwa nawasiliana na mery kupitia kwenye simu, kwa muda huo wa wiki mbili tangu niliposhiriki tendo la ndoa na mery nilianza kuona mabadiliko katika maumbile yangu ya kiume, kwani wakati nilikua nikienda haja ndogo nilikua napata maumivu makali sana, maumivu hayo yalizidi na ikafikia kipindi nikawa nikienda haja ndogo basi haja ndogo ilikua ikichanganyikana na damu, hali hiyo iliniogopesha na nilimueleza dokta hashimu mwanzo mpaka mwisho, dokta hashimu alinichukua na kunipeleka hospitali ambapo alinipima mwenyewe na hapo nilikutwa na gonjwa la ngono lijulikanalo kama kaswende, basi alinianzishia dozi na baada ya kumaliza dozi nilimleta na mery ambae nae alikutwa na gonjwa hilo ambalo kwake lilikuwa sugu
#itaendelea
baada ya kumaliza dozi nilimleta na mery ambae nae alikutwa na gonjwa hilo ambalo kwake lilikuwa sugu hali iliyosababisha kizazi chake kuharibika na hapo madaktari hawakuwa na jinsi zaidi ya kumtoa mery kizazi na kuanzia hapo mery alianza kuishi maisha ya utasa, licha ya mery kuwa tasa nilimpenda sana na nilipanga siku nitakapo pata kazi basi nitamuoa na kuwa mke wangu kabisa, nilipomwambia mery kuhusu hilo alinikatalia na kuniambia nitafute mwanamke mwingine ambae angeishi na mimi na kunizalia watoto, hali hiyo ilinikosesha raha kabisa, sikuwa tayari kumpoteza mery hivyo nilipanga lazima nitafunga ndoa na mery, baada ya kumshauri mery kwa muda mrefu huku mery akionyesha kusuasua ndipo nilipoamua kwenda hospitali kupima kama naweza kumpa mwanamke ujauzito, majibu yaliyotoka yaliniacha kinywa wazi kwani niliambiwa kuwa sina uwezo wa kumpa mwanamke mjamzito na tatizo langu limetokea hasa baada ya kuugua ugonjwa wa kaswende, basi nilitoka hospitalini hapo na kuelekea moja kwa moja sehemu ambayo alikua akiishi mery, nilimuonesha mery majibu yale na mery alionesha kushtuka lakini alinifariji na kunitia moyo, hapo pia niliamua kumdokeza tena kuhusu suala la ndoa ambapo mery alikubali nimuoe kwakua wote tulikua hatuna uwezo wa kupata mtoto, baada ya mwezi mmoja dokta hashimu aliweza kunitafutia kazi katika benki hii ya CRDB ambapo nilipata na kutokana na vyeti vyangu kuwa vizuri niliweza kuajiriwa kama maneja msaidizi(assistance maneger), baada ya kupita miezi miwili tangu niajiriwe ndipo nilipofunga ndoa na mery na kuanzia siku hiyo nilihama nyumbani kwa dokta hashimu na kuhamia katika nyumba yangu ambayo nilizawadiwa na uongozi wa benki hiyo na nyumba hiyo ilikuwa maeneo ya kigamboni na hapo ndipo nilipoamishiwa katika tawi la posta na kuwa maneger kwa kuwa kutoka kigamboni mpaka posta kulikua hamna umbali na Baada Ya CRDB kufanya vizur sifa zangu zilitapaka ndipo Raisi alinichagua kuwa mkurugenzi wa TRA. Mr Yusuf alimaliza simulizi yake ambayo alikuwa akimuhadithia sheby…
#itaendelea
Tags:
CHOMBEZO