Mr Yusufu alipigwa na butwaa baada ya kusikia kua dokta hashimu alisimamia gharama zote za yeye kutibiwa kwani hakuamini kama katika dunia hii bado kulikua na watu wenye moyo kama dokta hashimu, hii ni kutokana na kuona jinsi dunia inavyoenda, watu hawasaidiani, watu wanachukiana, watu wanadharauliana, watu wanauana, wenye pesa wanawadharau masikini kwa kuwaona hawapaswi kuishi, sasa alishangaa kuona mtu mwenye moyo kama ule kuwepo katika kizazi hiki cha nyoka…
“Nashukuru sana dokta Mungu akubariki na akuzidishie kipato chako kaka yangu” Mr Yusufu alijikuta akizungumza maneno hayo huku machozi yakimtoka, hakika alijiona ni mwenye bahati sana, ingawa alikua ana fedha za kutosha kama pasinge tokea mtu ambae angejitolea kumsimamia mpaka hapo alipofikia, angeshakua marehemu kwani pesa alikuwa nazo sawa lakini nani akijua kwamba pesa za kujilipia matibabu alikuwa nazo ilihali yeye alikuwa kapoteza fahamu kwa muda wa miezi miwili?, hakika kama dokta hashimu asingejitolea kumlipia matibabu yake basi toka siku nyingi jina lake lingeshabadilika kutoka Mr Yusufu mpaka kuitwa marehemu,angeshakua mfu na kwa kipindi hiki pengine wadudu kama funza na wengine wangekuwa washautoboa toboa na kuuharibu mwili wake vibaya kipindi ambacho angekuwa yupo kaburini, hakika alifarijika sana na kumshukuru mungu na kumuombea dokta hashimu na wenzake wote waliomsaidia waishi maisha marefu na kama wakija kupoteza maisha basi mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, Mr Yusufu alishindwa hata amshukuru mungu kwa kiasi gani kutokana na ukuu aliomtendea…
“Oooh ahsante Mungu kwa kila jambo” aliongea Mr Yusufu kukamilisha shukrani zake kwa Mungu…
“Daa asee kweli bana hapo Mungu alikutendea muujiza” alizungumza Sheby huku akishusha pumzi ndefu..
“Ndo hivyo mwanangu Mungu alinitendea miujiza” alizungumza Mr Yusufu kuthibisha alichokisema Sheby
“Enhee baada ya hapo ikawaje?” aliuliza tena sheby na baada ya swali hilo Mr Yusufu aliendelea kusimulia yale yaliyomsibu mpaka kufika hapo alipofika…
“Basi baada ya kumshukuru Dr hashim, ndipo alipovunja ukimwa tena kwa mara nyingine na kuniambia….
#itaendelea
“Aaaa samahani mr Yusufu kuna tatizo limetokea ila kwa kua wewe ni mwanaume naamini utavumilia na kujikaza kiume” alizungumza dokta hashimu kumuambia mr yusufu
“Tatizo gani tena dokta? Nimekua kilema nini sitaweza kutembea tena katika maisha yangu?” alizungumza Mr yusufu katika hali ya hamaniko…
“Hapana mr yusufu haujawa kilema ila yakupasa usikilize kwa umakini sana kwani ukija kukiuka utakayoambiwa unaweza ukajisababishia matatizo makubwa sana katika maisha yako” alizungumza dokta hashimu katika hali ya utulivu wa hali ya juu sana
“Jamani kiyu gani hicho tena mbona unanitisha dokta?” Mr yusufu aliuliza kwa hali ya uoga sana
“Yakupasa utulie na utilize hofu yako, na yakupasa kuwa mtulivu na msikivu sana katika hili mr yusufu” alizungumza dokta hashimu na baada ya hapo alimrusu dokta razaq ambae alikua amebobea katika masuala ya psychology(saikolojia) na masula ya kizazi kuzungumza juu ya jambo hilo.
Kitendo cha dokta hashimu kumruhusu dokta razaq kuzungumza juu ya tatizo ambalo limemkuta mr yusufu, kengele ya hatari iligonga kichwani mwa mr yusufu alishaelewa maana yake nini kwa alishafahamu kuwa dokta razaq ni mtaalamu wa masuala ya saikologia pamoja na masuala ya kizazi hivyo alijua fika kama hatokua na tatizo la kisaikolojia basi atakua na tatizo la kizazi, na ingawa alijua fika kuwa lazima atakuwa na tatizo moja kati ya hilo aidha la kisaikolojia au linalohusu kizazi alijitahidi kumuomba mungu amuepushie na hayo matatizo, alikatishwa katika dimbwi la mawazo baada ya dokta razaq kuanza kuzungumza na hapo aliweka umakini na utulivu wa hali ya juu katika kumsikiliza ni kitu gani dokta razaq alikua akitaka kumuambia…
“Mr Yusufu kwanza pole kwa yaliyokukuta, japo kuwa ni makubwa yakupasa umshukuru mungu kwa kila jambo kwani binaadamu ndio sisi na haya matatizo tumeumbiwa pia sisi wanaadamu,
#itaendelea
Mr Yusufu kwanza pole kwa yaliyokukuta, japo kuwa ni makubwa yakupasa umshukuru mungu kwa kila jambo kwani binaadamu ndio sisi na haya matatizo tumeumbiwa pia sisi wanaadamu, hivyo katika hali yeyote ile litakapo kufika jambo aidha liwe jambo zuri au baya, lakusikitisha au lakuhuzunisha, lakufurahisha au lakuliza, yakupasa umshukuru mungu wako kwani yeye ndiye mpangaji wa kila jambo, hakuna jambo ambalo linashindikana kwake, yeye nduye mpangaji wa kila jambo linalotokea, yeye ndiye anayeamua leo litokee hili au leo lisitokee hili, hivyo yakupasa umshukuru mungu wako kwa kila jambo, pia kaa ukitambua na kujua ya kuwa kila neno limeshaandikwa kinachosubiriwa ni andiko litimie tuu, yakupasa ukubaliane na kila jambo ambalo tayari limeshatokea katika maisha yako, yakupasa usimame kiume na ukabiliane na changamoto ambazo utakumbana nazo katika maisha yako” yalikua na maneno ya faraja na kutia moyo ambayo alikuwa akizungumza mtaalam wa masuala ya saikolojia pamoja na kizazi dokta razaq…
“Sawa dokta nimekuelewa na nashukuru kwa maneno yako kwani yamenitia moyo na faraja pia, mungu akubariki dokta” alizungumza mr yusufu
“Usijali na karibu, ila pasina kupoteza muda kwani unahitajika kupumzika, nikwamba wakati ulipopata ajali kuna vipande vidogo vidogo vya kioo ambavyo vilifanikiwa kupenyezza katika suruali yako ambayo kwa kipindi ajali ilipotokea suruali hiyo ilichanika kwa kiwango kikubwa hivyo kusababisha eneo kubwa la mwili wako kubaki wazi, baada ya kufanya uchunguzi wa kina ndipo nilipogundua kuwa vipande hivyo vilifanikiwa kuingia katika ngozi ya korodani zako ukizingatia ngozi hiyo huwa ni laini sana hasa katika kipindi cha joto kali kama hichi, vichupa hivyo viliweza kuathiri kwa kiasi kikubwa vimirija ambavyo huwa vinatunza shahawa wa muda ambavyo vimirija hivyo vinajulikana kwa kitaalamu kama(seminiferous tubules), nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu na nilifanikiwa kuvitoa vipisi hivyo vya kioo ambavyo vilikuwa vimeathiri vimirija hivyo, licha ya kuvitoa tayari kuna madhara ambayo yalishatokea baada ya vipande hivyo kupenyeza katika ngozi ya korodani zako,
#itaendelea
Tags:
CHOMBEZO