MOYO WANGU 16---17----18

Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, kama jinsi watu walivyotabiri kuwa tutapata ajali ndivyo ilivyokua, kipindi nakanyaga mafuta mpaka mwisho sikuweza kugundua kuwa mbele palikua na bamsi nah ii ni kutokana na kutokujua vyema barabara ile, ni kitendo cha ghafla tuu na kutahamaki tayari nikawa nimelifikia bamsi lile, nilijaribu kufunga breki za ghafla lakini breki zilifeli, hapo nikalivaa bamsi lile ambapo tax ile niliyokua naendesha wakati huo tukiwa wawili tuu kwenye tax ile, tax ile irushwa juu na baada ya kutua iliviringika mara tano mfululizo, yule dereva tax nilokuwa nipo nae nilishuhudia akikata roho wakati bado hatujatolewa katika gari ile na baada ya kushuhudia tukio la kukata roho kwa yule dereva tax sikujua tena kilichoendelea kwani nilipoteza fahamu” alizungumza Mr Yusufu huku machozi yakimtoka, alitoa handkerchief(hengach­ifu/leso) yake katika moja ya mfuko wa koti la suti ambalo alikua amelivaa na kujifuta machozi…
“Daaa aise pole sana baba kwa yaliyokukuta” alizungumza sheby katika hali ya huzuni kubwa na kuumia moyoni
“Nashukuru mwanangu nimeshapoa” alijibu Mr Yusufu
“Enhe baada ya hapo ikawaje baba” aliuliza tena sheby na kufanya Mr Yusufu kuendelea kusimulia kilichomkuta baada ya ajali ile mbaya kuwahi kutokea katika maisha yake..
“Basi nilipokuja kupata fahamu nilijikuta nipo hospitalini ambapo nilikuja kugundua kuwa ilikua ni hospitali baada ya kuwauliza wahudumu ambao walikua wakipishana kuingia katika chumba ambacho nilikua nimelazwa, nilijaribu kuamka na hapo nilikumbana na maumivu makali sana ambayo yalinifanya nitoe ukulele hafifu na baada ya hapo nilipoteza tena fahamu, siku ambayo nilikuja kupata fahamu nilisikia mchakacho wa kama mtu akikimbia na baada ya hapo nikisikia sauti ya kike ikisema kwa nguvu..
“Doktaa ameamkaaa”

#itaendelea 

Hazikupita hata sekunde tano liliingia jopo la madaktari wapatao watano ambapo walipoingia walitabasamu baada ya kuona nimefungua macho, hapo nilitolewa mashine ya (Oxygen) oksijeni ambayo nafikiri ndiyo iliyokua ikinisaidia kupumua kipindi ambacho nilikua nimepoteza fahamu, baada ya mashine ile kutolewa ndipo nilipoanza kuangaza macho huku na huko, nilijaribu kuvuta kumbukumbu jinsi ilivyokua na hapo niljikuta machozi yakinitoka baada ya kukumbuka matukio yote niliyokutana nayo ambayo yalipelekea mimi kuwa hapo hospitali ya taifa ya muhimbili kwa kipindi hicho, niligeuka upande ule ambao ulikuwa na jopo la madaktari, niliwaangalia kwa awamu na hapo niliwauliza nipo wapi maana chumba ambacho nilikuwepo mara ya kwanza kilikua ni tofauti na chumba ambacho nilikuwepo kwa muda huo…
“Tulia Mr Yusufu kwanza pole kwa yaliyokukuta” alizungumza mmoja wa madaktari ambaye alionekana ndiye mkubwa wa jopo lile la madaktari waliokuwepo mule ndani, muda huo nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kichwani, kwanza nilijiuliza wamejuaje jina langu na nipokumbuka kwamba nilikuwa na vitambulisho pamoja na vyeti vyangu basi nilijikuta mawazo hayo yakiisha na hapo ndipo nilipokumbuka kuwa kuna dokta alikua ananiondelesha, basi nilianza kumjibu yule dokta maswali ambayo alikua akiniuliza…
“Pole sana Mr Yusufu kwa yaliyokukuta” alizungumza daktari yule ambae alikua akizungumza kwa umakini wa hali ya juu..
“Nashukuru sana dokta…”
“Sawa naitwa dokta Hashim, wenzangu hapo ni dokta jack, dokta john,dokta abdul na dokta Razaq” alitambulisha dokta hashimu na baada ya hapo aliendelea..
“Mimi nahusika na masuala ya mwili kwa ujumla lakini nimebobea katika kutibu magonjwa ya moyo, ini pamoja na figo, huyo dokta jack yeye amebobea katika maswala ya mifupa, dokta abdul yeye amebobea katika maswala ya ubongo na mshtuko na dokta razaq yeye amebobea katika maswala ya psychology(saikolojia) pamoja na maswala ya kizazi(reproductive issues as general)” dokta hashimu aliweka nukta na kumeza funda la mate kabla hajaendelea…

#itaendelea 

Nashukuru kwa utambulisho dokta, samahani kwa swali hili ambalo nataka kukuuliza” aliongea Mr Yusufu
“Bila samahani, unavyotuona hapa tupo kwaajili ya kukujibu maswali ambayo yatakuwa yanakutatiza” alijibu dokta hashim na kumtoa wasiwasi Mr Yusufu
“Tangu nimeletwa hapa nina mda gani?” Mr Yusufu aliuliza
“Ulifikishwa hapa muhimbili miezi miwili iliyopita, lakini mwezi mmoja kabla ya kuingizwa katika chumba hiki cha wagonjwa mahututi(ICU) ulipata fahamu lakini manesi ambao walikua zamu siku hiyo wanasema ulivyopata fahamu ulipiga ukulele na baada ya hapo ulipoteza tena fahamu, kesho yake ndipo tukakuleta huku katika wodi ya wagonjwa mahututi na hapo kwakuwa mapigo yako ya moyo yalikuwa chini tulijaribu kuyastua ambapo yalipanda kidogo na hapo ndipo tulipokuwekea mashine hiyo ya kupumulia ambayo tumekutolea muda sio mrefu, na ulidumu katika hali hiyo ya kupoteza fahamu huku ukiwa unapumulia mashine kwa muda usiopungua takribani wiki nne kasoro mpaka siku hii ya leo ambayo ndo umepata fahamu” dokta hashimu alimaliza maelezo yake aliyoyatoa kwa kirefu ambapo Mr Yusufu alimuelewa vema…
“Na vipi kuhusu gharama na huduma ambazo mlikuwa mnanipatia, ni nani ambae alikua anashughulika na hili?” Mr Yusufu aliuliza tena kwani alizijua vyema hospitali za bongo, huwezi kutibiwa kama utakuwa huna pesa…
“Usijali gharama zote nilizitoa mimi mpaka kufikia leo hii, nah ii nimeifanya kwa moyo kwani nilipatwa na huruma sana baada ya kuona mwili wako ukiwa katika hali mbaya, hapo nimuomba Mungu anisaidie niweze kupambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba unarudi katika hali yako ya kawaida, na ninamshukuru Mungu kwa kutenda muujiza mpaka wewe unapumua kwa wakati huu” alizungumza dokta hashim.

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post