MOYO WANGU 13---14-----15

“Nakumbuka ilikua mwaka 1988 ambapo nilimaliza elimu yangu ya juu katika chuo cha Oxford kilichopo nchini marekani”
“Ngoja kwanza baba kabla hujaendelea, huko oxford ulikua unasomea nini?”
“Nilikua nasomea masomo haya haya ya uhasibu, lakini kule nilienda kuchukua phd(philosophical doctor)(degree ya tatu) ya uhasibu, kwani stashahada yangu ya kwanza(first degree) niliipata katika chuo cha cambrige ambapo pia kutokana na kufaulu vizuri masomoyangu waliamua kunidhani na nikapata stashahada yangu ya pili katika chuo hiko hiko, kutokana na kuendelea kufaulu vizuri masomo yangu nilidhaminiwa na chuo kwenda kuongeza elimu yangu na hapo niliambiwa nichague chuo ambacho nakipenda ili niende kusoma degree yangu ya tatu yani phd, hapo ndipo nilipochagua chuo cha oxford kwani ndio chuo ambacho nilikua nakitamani tangu nikiwa mdogo, nilisoma hapo na baaada ya kuhitimu masomo yangu niliweza kufaulu kwa kiwango cha juu sana ambacho hakijawahi kutokea tangu chuo kianzishwe na hapo ndipo nilipoitwa na uongozi wa chuo cha Cambridge wakinitaka niwe muhadhiri(lecturer) wa chuo hicho katika masomo hayo ya biashara” mr Yusufu aliweka kituo na kupiga funda moja la juisi ya embe ambayo alikua akiitumia kwa muda huo..
“Haa kumbe ulishawahi kuwa muhadhiri wa chuo kikuu cha Cambridge?” Sheby alimtupia kiswali cha uzushi mr Yusufu..
“Ndio tena nilifundisha kwa takribani miaka mine na baada ya hapo ndipo nilipoamua kuja nchini kwangu Tanzania kwaajili ya kuja kuwasalimu wazazi wangu kwani ni muda mrefu tangu niondoke na wao walikua kijijini huko Mtwara na wakati huo simu hizi zilikua bado hazijaenea” aliongea mr Yusufu
“Enhee ikawaje sasa baada ya kuamua kuja nchini?” aliuliza sheby kwa staili ya kudadisi..
“Ndo hivyo mwanangu, nilienda kwa mkuu wa chuo ( Chancellor ) na kumueleza jambo hilo na bila hiyana aliniruhusu na alinipa likizo ya miezi mitatu, basi nilikata tiketi ya ndege na baada ya hapo kesho yake nikapanda ndege na kuja nchini Tanzania, baada ya kufika nchini Tanzania nilienda moja kwa moja kijijini kwetu Mtwara na hapo sikuweza kuamini nilichokikuta” aliongea mr Yusufu huku akionekana kulengwa lengwa na machozi…

#itaendelea 


mr yusufu aliongea akionekana kulengwa lengwa na machozi…
“Mbona kama unataka kulia baba kwani ulikuta nini nyumbani?” aliuliza sheby huku akimuangalia mr yusufu kwa umakini wa hali ya juu…
“Kutokana na kwetu kuwa kijijini tena ndani ndani kabisa, kiasi kwamba kutoka nyumbani mpaka kwa jirani unaweza kutumia dakika kumi mpaka kumi na tano, basi baada ya kufika huku nikiwa na zawadi zangu mkononi na wakati huo nilikua nimekodi tax kutoka mtwara mjini, sikuamini pale nilipowaona chatu wakubwa wawili wakiwa wanamalizia kuwameza wazazi wangu, hakika ilikua ni picha ya kutisha kweli, nilipiga ukulele wa uchungu na hasira pia, kwakua nilikua na bastola, nilishuka katika tax ile huku nikikimbia kuelekea eneo ambalo walikuwepo wale chatu ambao kwa wakati huo walikuwa hawawezi kutembea kutokana na kumeza viumbe wakubwa ambao walikua ni wazazi wangu, yule dereva tax alikua akinipigia ukulele kuwa nirudi kwani ilikua ni hatari kutokana na kua nilikua peke yangu tena nikiwa naonekana na umbo dogo kwani alihofia kwamba chatu wale wanaweza wakanidhuru, licha ya dereva tax yule kunipigia ukulele, sikuweza kusimama wala kumsikiliza, niliendelea kukimbia upande ule ambao ndipo walipokuwa chatu waliowameza wazazi wangu huku nikiwa na hasira na uchungu mkubwa, lakini kitu kingine ambacho kilinisukuma kufanya hivyo ni kwamba nilikua na matumaini kwamba nitawakuta wazazi wangu wakiwa ni wazima kutoka na kushuhudia tukio la kumezwa kwao, basi wakati nimewakaribia wale chatu ghafla mbele yangu umbali wa kama mita tatu walitokea chatu wengine pamoja na nyoka mkubwa aina ya kobra wakiwa wanaonekana kuja sehemu ambayo nilikua nimesimama kwasababu ya kupigwa na butwaa, na viumbe wale walionekana kabisa walikua wanania ya kunidhuru, yule dereva tax alinipigia makelele kuwa nirudi kwenye gari haraka lakini kutokana na kupigwa na bumbuwazi sikuweza kumsikia na wala sikujua nifanye nini kwa wakati huo…Wakati nikiwa katika hali hiyo ya bumbuwazi nilipatwa na mshtuko baada ya kuona viumbe wale wakizidi kuongezeka kila baada ya sekunde kadhaa,

#itaendelea 

Wakati nikiwa katika hali hiyo ya bumbuwazi nilipatwa na mshtuko baada ya kuona viumbe wale wakizidi kuongezeka kila baada ya sekunde kadhaa, ni kama vile mshtuko ule ulinigutua katika bumbuwazi lile na hapo ndipo nilipo usikia vyema ukulele wa yule dereva tax akiniita kwa nguvu kuwa nirudi kwenye gari ili tuweze kuondoka kwa eneo lile halikua salama kuendelea kubaki, ilifika muda yule dereva tax akashuka katika gari ili aje anivute tuingie kwenye gari, hapo niligeuka haraka baada ya kusikia ukulele mkubwa ambao aliutoa yule dereva tax kuonesha kwamba alikua katika hatari kubwa, na kweli nilipogeuka niliona chatu mwingine mkubwa kiasi akiwa anaanza kujiviringisha katika mwili wa dereva tax yule ambae alikua akipiga makelele ya uoga ili aweze kummeza, hapo nilitoka mbio mbio mpaka eneo alilokuwepo yule chatu ambae alikua anajiviringisha katika mwili wa dereva tax, hapo niliitoa pistol(bastola) yangu kisha nikaikoki vyema na kilichofuata nilisambaratisha kichwa cha yule chatu ambae alikua akijiandaa kummeza yule dereva tax, hapo nilimsaidia kujitoa kwa chatu yule ambae tayari alikua ameshapoteza uhai wake na kwakua yule dereva tax hakuwa sawa nimsaidia kumuingiza kwenye gari, hapo nilikaa sehemu ya usukani na kuliondoa gari kwa kasi ya ajabu kwani wale chatu wengine walikua wakija kwa kasi eneo lile ambalo tulikuwepo kwa lengo la kutudhuru, kutokana na mwendokasi ambao nilikua nikiutumia niliweza kufika mtwara mjini kwa kutumia dakika kumi tuu,spidi niliyoingia nayo katika barabara ya lami kila mtu aliyekuwepo barabarani aliweka mikono kichwani na wengi walitabiri kwamba tutapata ajali kwa mwendo ule, wengine walidhani kuwa huenda sisi ni majambazi tumetoka kupora mahali…

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post