SI KILA MAHUSIANO YA KUYAVUMILIA 5

Nilitoka nnje nikanunua chakula nikarudi ndani kula,,,maisha yaliendelea yale yale ya upweke na mawasiliano na sylivester yalishamiri hasa na kunoga mwisho tukawa wapenzi na kipindi hicho sikua na simu ya touch nilikua na sim ya kawaida tu hivyo tulikua tunachart sana na kuongea na simu muda mwingi yaan tulikua tunakesha nilikua nasoma ikifika saa tano usiku tunaongea hadi alfajiri jamani mapenzi haya 😂 achenu tu..sikuacha kwenda chuo kumuangalia mkurugenzi kama amerudi ila inavyoonekana alienda likizo kabisaaa maana haikua kawaida na mama alimtafuta sana lakini hakua akijibu sim na muda mwingine alikua hapatikani hivyo akamuacha akaniambia akirudi tu chuo nimwambie ili aje aonane nae...na hatukuweza kwenda sehem yoyote maana hakikua chuo cha serikali ni private hivyo ilibidi tu niwe mpole....na si kwamba ni mimi tu ndo sijaenda field hapana ni wengi ila hao wengine kweli walikua wanadaiwa ada ila mimi aliniingiza tu kwenye kundi lisilonihusu na yeye ndo alikua na maamuzi ya mwisho hivyo ilitakiwa awepo ndo anielekeze vizuri hiyo ada nayodaiwa ni ada gani maani hadi kwa secretaary wa chuo nilimfata lakini aliniambia yeye hayo majina amepewa na mkurugenzi kwa hiyo nisubiri akirudi nimfate, sikua na namna ilibidi nivumilie tu japo nilikua naumia lakini sikua na namna na ukizingatia field ya pili ndo inayojazwa kwenye mtihani wa mwisho sasa usipoifanya inamaana italeta shida....
   Siku moja nikiwa tunaongea na sylivester akaniambia anaomba niende dar hata wiki tu alafu nirudi maana nilimdanganya kua nipo likizo sikumwambia ukweli sikutaka ajue hivyo alijua nipo likizo ila sijarudi nyumbani nimebaki kujisomea. Mmmh nikamjibu naanzaje kuja na mimi sasa hivi aipo vizuri akaniuliza kivipi nikamwambia sina hela wala nauli ya kunifikisha dar, na si kwamba sikua nayo hapana ila tu nilikua najaribu kumkwepa maana nilikua najua kwanini sitaki kwenda kwa muda huo, alilalamika sana akanambia nauli si shidah mimi nitakutumia hela ya nauli nataka tu kukuona nakuomba sana mamie usinikatalie hata ukikaa siku mbili ni sawa zitatosha tu lengo nikuone tu alafu na mimi hapa nipo chuo kama unavyojua na tunakaribia mihani ko siwezi kutoka la sivyo mimi ningekuja,,,katika utambulisho aliniambia kua anasoma chuo UDSM ila hakuniambiaga anasomea nini na aliniambia baba yake ni diwani wa kawe na jinsi alivyokua akiongea huezi bisha hata kidogo,,maneno yaliniingia na hivi nilikua natamani kumuona nikaona si shida acha niende siku mbili si nyingi nikamkubaria kua nitaenda anipe siku moja nijiandae kisha niende..alifurahi nikapigwa makiss kama yote 🥰🥰😂 wanaume wakitaka yao kama watu 😂,,,,tukaongea sana kama kawaida hadi alfajili basi siku iliyofuata nilichelewa kuamka maana hua nachelewa kulala nilivyoamka tu mida ya saa sita nikakutana na msg kama zote kutoka kwa syliveater mara mkewangu hujaamka tu, mara umeamkaje, nyungine nakupenda sana malkia wangu, amka basi nisikie sauti yako,,,jamani wanaume mungu anawaona....nikaamka pale mwenyew nasikia rahaaa nikatabasam nikamtext nimeshaamka love...woi muda huo huo simu ikaingia umeamkaje malkia wangu,,,mie tena salama love wewe je, akajibu nimeamka poa mpnz amka basi uoge unywe chai ufanye maandalizi yako si unajua kesho unakuja,,,nikamwambia sawa naamka sasa hivi basi akasema nakutumia hela ukasuke na nyingine ufanye nauli ya kuja kesho nikamjibu sawa asante sanaaa love...akakata simu na dk kama kumi hivi muamala ukasoma amenitumia elfu 80 na ikumbukwe nauli ya kwenda daa kipindi hicho ilikua 6000...nikamtumia msg ya asante kisha nikaamka nikaoga niakenda saloon kusuka mida ya saa moja hivi usiku nikarudi hostel hapo simu muda wote yaani kama kesho ndo tunaoana hivi🤣🤣🤣🤣.....lakini nikakumbuka kua natakiwa kuongea na madam wa nidham kua natoka maana nilikua na no yake na tulikua tunawasiliana alikua kama dada yangu,,,nikampigia nikamtaarifu kua naenda nyumbani mara moja mama ameniita hivyo kama mkurugenzi akirudi naomba anitaarifu akasema sawa hakuna shida ila usikawie kurudi nikamwambia sawa,,,kisha nikampigia prisca nae nikamwambia kama nilivyomwambia madam sikutaka kuweka wazi sana mambo yangu ndivyo nilivyo basi nae akanambia poa dear usijali tutawasiliana...hapo nikawa na amani najua kuna watu wawili nawaacha hivyo chochote kikitokea nitapewa taarifa ila mama yangu sikumwambia kama nasafiri yeye alijua bado nipo chuo...siku ikapita hatimae kukakucha jamani nilipigiwa sim saa kumi na moja alfajiri nijiandae maana usiku wake hatukukesha kuongea na sim ili nipumzike sababu ya safari,,,nikaamka nikajiandaa nilikua nishampanga dereva,kuna dereva alikua na tax nikampanga kua asubuhi anichukue aniepele stand kweli nilivyomaliza kujiandaa nilimpigia akanifata akanipeleka stendi nikashuka nikamlipa akaondoka nami nikaenda kukata ticket nikaingia kwenye basi mida ya saa moja asubuhi na basi lilikua linaondoka saa mbili asubuhi...hapo nishamtaaribu babe 😍 kua nishapanda basi nawaza tu sijui naenda kukutana na mtu wa aina gani..
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post