SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA. 6

Nilimtaarifu babe kua nishapanda basi yaan mapenzi yakiyawa yanaanza bhana raha mtaitana kila aina ya majina.,,,,tuendendelee
  Mida ya saa mbili safari ilianza hapo nawaza sijui naenda kukutana na mtu wa aina gani woga ukaanza kuniingia kwa mbali ila nikawa najipa matumaini kua hatonifanya kitu kibaya...safari iliendelea tulipofika morogoro stand msamvu yaan hata nnje nilikua siangaliii maana nilikaa dirisha niliogopa asije niona mtu naefahamiana nae taarifa zikamfikia mama yaan tena nililaza kichwa kwenye siti ya mbele yangu, tulivyopita msamvu nikainua kichwa safari ikaendelea ilipofika saa Kumi na mbili jion tulikua tunaingia ubungo maana tulikutana na foleni kimara hivyo ilituchelewesha kidogo hapo nishamwambia sylivester kua nimepanda gari gani na No ya gari hivyo alikua ubungo tu ananisubiri,,basi liliingia likapaki abiria tukaanza kushuka, ghafla sim ikaita kuangalia mama uwiii amejua nini? Nikapokea haloo mama ikabidi nikae kwanza maana nje ya gari kelele nyingi,,hujambo! Sijambo mama shikamooo,,,,marhaba,uko wapi mwanangu? Mmh nilishtuka nikamjibu nipo mjini kuna vitu nimekuja kununua,,,akasema okay sawa usikawie kurudi hostel na uwe makini sanaa nilikua nakujulia hali tu,sawa mama nashukuru, akakata sim,,,niliwaza kahisi nini mbona hivi? Ila nikajua hajajua maana kwa ukali wake angekua anajua asingenibembelezaa hivyo moto ungewaka hapohapo,watu walikua wanamalizikia kushuka nami nikashuka nikawa nataka nimpigie sylivester nijue yuko wapi ila ghafla nilishikwa mkono.,,nikashtuka kugeuka nakutana na mkaka mwenye mwili wake yaan kama alivyo jayb yule mwigizaji uwiii nini nani huyu nikashtuka akaniwahi samahani ww ni winie nikatikisa kichwa maana niliduwaa akanihag wao karibu mpnzi karibu sana na pole na safari akanipokea kibegi maana nilibeba pochi tu ambayo niliweka nguo za siku mbili tu sikua na mizigo mingi,,,nikajichaangamsha kidogo nikasema asante sanaa nishapoa akanishika mkono akaniambia twende tukapande gari,,,,tukatoka nje ubungo tukafika kituoni gari ikaja tukapanda tukiwa kweye gari nawaza sasa mbona mkubwa hivi uwiii yaani si kwamba alikua ni mtu mzima hapana ni kijana tu ila mwili jamani mmmh na ukiniangalia mimi kipindi hicho sikua na mwili mkubwa nilikua mwembamba tu japo si sana ila kwa mwili wake hatukuendana hata kidogo, njia nzima anafurahi tuuu amenishika mkono tu,, hapo mimi macho yapo nnje tu kushangaa mitaa tunayopita maana ilikua ndo mara ya kwanza kufika dar esaalam,,,,ilituchukua muda mrefu kidogo lakini tulifika na tukashuka,, tulivyoshuka tu nikaanza kusikia vijana wa pale wanamuita huku wakimtania kama mnavyojua wanaume,, naye alikua akiwaitikia huku anacheka tu nikamuuliza unaonekana unajulikana sana akasema yah najulikana mpnz kutokana na kazi ya baba angu kipindi cha kampeni niliongozana nae sana alafu mimi nimezaliwa hapa na kukulia hapa hivyo wengi wananijua maana wengi tumekua wote japo wengine ni wageni huku...nikamjibu okay sawa,,,sasa nikawa nawaza diwan ni mtu mwenye hela zake kidogo sasa hata usafiri hawana mbona tunatembea tu hata basi hata tax tukodishe maana tumetembea muda mrefu na nilishaanza kuchoka nikakumbuka nina akiba nikamwambia love kwani bado mbali sana maana nishachoka au tuchukue usafiri akasema tushafika malkia wangu nilitaka unyooshe miguu maana umekaa sana nikamjibu sawa....ilituchukua kama dk saba hivi tukafika akaniambia ni hapa babe karibu,,,,uwiiii 😲😲😲 hicho kijumba jamani yaani ni nyumba zile zinazojengwa ili kulinda kiwanjwa nadhani mnazijua japo majirani walikua na nyumba kubwa kubwa tu na nzuri hatari ila pale ilikua ni vyumba vinne kimoja kimeisha na vingine havijaisha wameezeka tu ila havina mlango wala madirisha dooh niliduwaaa kimoyomiyo nikamuangalia machoni nikamwambia love hapa ndo mnapoishi? Akanijibu hapana mpenzi sisi tunaishi hapo mbele tu nitakupeleka utapaona ila kwa sasa tutakaa kwanza hapa nikifanya mazingira mengine sawa mama ingia basi ndani upumzike,,,sikutaka kumuonyesha kua sijapendezwa na yale mazingira niliitikia tukaingia ndani nikakaa kwenye kitanda yeye akaweka pochi akaniambia nakuja love naenda kukuletea chakula nikajibu sawa,,,,yaani kile chumba kilikua na kitanda na godoro na godoro lenyew lilikua limeisha japo ukikalia haliumizi,pembani ya kitanda kulikua na baiskeli zike za mkulima na ilishaharibika kwa mwonekano,,pia kulikua na kochi la watu watatu la mbao ila halina mito ya kukalia na kulikua na kabati la kawaida tu la nguo, jiko la mchina na madumu ya maji dooh nilibaki nimeshangaa tu inawezekanaje na hapa ni kwa nani? Maana kama viela alikua akinitumiatumia sasa alishindwaje kuchukua hata guest akalipia tukakaa hizo siku mbili kuliko hapa,,,wakati bado natafakari mlango ulifunguliwa aliingia pole mpenzi nimekuacha peke yako, huku chakula unasubiria sana maana nilikuta foleni,,,nikamwambia usijali love niko sawa..............
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post