SI KILA MAHUSIANO YA KUYAVUMILIA 4

 Akaniuliza kwani hujui kwanini anakufanyia yote hayo nikamjibu sijui akasema ngoja nikwambie.....mkurugenzi anakutaka....unasemaje madam nilimuuliza kwa mshangao pamoja na kwamba wanachuo tulikua tunajua tabia za mkurugenzi kua anapenda na wanachuo na si mmoja yaani karibia wanne na tulikua tunajua kua ni muathirika maana story zilikua zimetapakaa sana hivyo kutaka mwanafunzi hakikunishangaza ila kunitaka mimi hapo ndo nilishangaa maana sikuwahi kua na mazoea nae hata ya bahati mbaya maana kuna wanachuo walikua wamezoeana nae sanaaa hadi unakuta wapo offisin kwake wanapiga story tu ila mimi sikuwahi na hivi tulikua hatupatani hivyo sikujiangaisha nae sanaaa...na alikua na asili ya kihindi ila ni mtanzania yaani amechanganyika...aisee nilishtuka nikamwambia madam hilo haliwezekani akasema ndo nakwambia hivyo mara nyingi hua akimtaka mwanacho hua anamfanyia vitimbi sana ili akija kumwambia shida yake isiwe ngumu kukubariwa...aisee nilibaki nimeduwaaa nikamwambia madam kwahiyo unanishauri nifanyaje!!!! Akasema wewe ni kama mdogo angu sikushauri uingie kwenye mkumbo wa wenzio nimekuona hauna makuu na umetulia sana ndo maana nakuambia hivi....muache afanye anavyotaka ila sikushauri ufanye ujinga wowote wa kukubari kua nae kama ikitokea atakutamkia,,mungu anasiri kubwa na maisha yako hivyo usijiaribie sawa,,,nilimshukuru madam na kumuahidi kufanyia kazi ushauri wake sikutaka kukaa tena maana alishanivuruga nilimuaga na kuondoka kurudi hostel...nilifikiria sana lakini sikupata....upweke ulinizidi ni kawa sina wa kuongea nae hosteli nipo mwenyew nilikua nampigia prisca naongea nae ila hili sikuweza kumshirikisha mimi ni msiri sana kuna mambo mengine hua mgumu sana kumwambia mtu hivyo nilikaa nalo moyoni..
  Wiki tatu zilikatika bila mafanikio ya kuonana na mkurugenzi na field ilikua miezi mitatu niliendelea kujipa moyo tu kua bado siku zipo maana ukaguzi hua ni wiki za mwezi wa mwisho hivyo nilijua muda bado niano....siku hiyo nilikua nilikua nachezea sim yangu akili ikaniijia ngoja nijaribujaribu no alafu nipige nikisikia sauti ya kaka mzuri niongee nae..huo wote upeke tu na akili za kiuanafunzi jamani msinishangae,na si kwamba sikuwahi kuwa kwenye mahusiano hapana nilishawahi kuwa ila ya kisiri sana maana mama alikua mkali sana hivyo mwanaume niliekua nae kipindi hicho hakuweza kunivumilia maana hakua akipata muda wa kua nami muda mwingi nabanwa hivyo tuliachana japo nilimpendaga ila sikua na namna tuliachana na ndo aliyenitoa usichana wangu...mama alijua kutubana watoto wake wakike namshukuru kwa hilo maana ukali wake ulitusaidia tulikua makini sanaaa....basi nikawa najaribisha no nyingine zinaita hazipokelewi nyingine zinapokelewa na wanawake na nyingine wanaume ila sauti mbayaaaa nikawa nasema tu sorry nimekosea no nakata...basi kuna no moja nikabahatisha akapokea kama anasauti nzuriiiii uwiiiii nikaamka kwanza nikakaa maana nilikua nimejilaza chini...hello,hello ,hello nani mwenzangu duh kaka aliita mara tatu mimi moyo unaenda mbio nikamjibu hellow samahani naongea na vicky dooh yote kuzuga 😂 akati najua ni mwanaume akasema hapana kwani wewe ni nani na unatokea wapi??? Sauti nzuri jamaniii uwiiii nikamjibu kwa pozi lote sauti nimeitoa ile ya pangoni 👌👌👌 naitwa winie nipo dodoma,,,akajibu oooh akay,dodoma unaishi au unasoma? Hapana siishi huku nipo chuo nasoma naishi morogoro,,, nilimjibu kwa bashasha.akanijibu okay sawa nimefurahi kukufahamu,mimi naitwa sylivester nipo dar esaalam changanyikeni....uwiii kusikia dar esalaam tena nikasema hapa ndo napopataka nikamjibu okay sawa nimefurahi kukufaham pia na samahani kama nimekusumbua maana niliekua namtafuta nimekosea no,,, hapo najishaua tu kuzuga 😂😂😂 akasema usijali winie mungu ana makusudi yake hadi ukakosea na kunipigia,kwani huyo vicky ni nani yako? Nikamjibu ni rafiki yangu tu tulipotezana mda tangu tukiwa shule alinipaga no yake sasa leo nimemmisi nikasema ngoja nimtafute bahati mbaya ndo nikakosea ikaja kwako....aaah usijali winie tena nimefurahi kusikia sauti nzuri ya mtu aliyekisea no na naimani utakua mrembo sana kama sauti yako...uwiii alizidi kunivuruga na hivi muda mrefu sikua na mahusiano basi tukaongea kidogo kisha akaomba tuwe tunawasiliana basi sim ikakatwa...daah nikajihisi upweke tena maana kidogo alinichangamsha...nikaanza kumtafakari kupitia sauti yake nikajua atakua handsome hatare maana si kwa sauti ile,,,njaa ikaanza kuniuma ikabidi niamke nikatafute chakula...nilitoka nnje nikanunua nikarudi ndani,,
 ITAENDELEA........... 

Post a Comment

Previous Post Next Post