Nilirudi likizo nikiwa sijui kama nimejiwashia moto 😪..nilikaa likizo nyumbani nikiwa sina shaka kabisaaa na likizo ilipoisha nilirudi chuo lakini nilifikia hostel ya nnje maana ya chuo nilishahamisha vitu ila nilitangulia kwanza mama aliniambia atakuja baada ya siku mbili ili aje aonane na mkurugenzi,,, kweli baada ya siku mbili mama alikua na mimi ndo nikajiandaa kwenda chuo maana nilihofia kwenda kabla mama hajafika, tulifika chuo moja kwa moja offisi ya mkurugenzi tukamkuta akatukaribisha vizuri sana tukakaa tukasalimiana kisha mama akaeleza lililotupeleka ofisini kwake,mkurugenzi alitusikiliza kisha akasema,,,mama nisamehe sana sitamruhusu binti yako atoke nnje ya chuo maana ana makundi siyo mazuri hivyo ni kwa usalama wake...heeee mimi nikatoa macho 😲 nikamuangalia mama nae amenikazia macho...nikashangaa huyu mgurugenzi vipi tena makundi gani hayo wakati sikuwahi kua na makundi wala marafiki zaidi ya prisca sasa huyu ananiongelea mimi ama mwingine 🤔 niliwaza sikupata jibu nikabidi nimuulize, mkurugenzi mimi mbona sina makundi yoyote yale au umenifananisha??? Akasema mimi si mjinga taarifa zako ninazo...nashukuru mama yangu alikua ananiamini sanaaa hivyo akuyaamini maneno haraka akamwambia mkurugenzi mimi nina watoto wengi ninaosomesha hivyo nikaona huyu nimuamishie hostel ya nnje ili niweze kuendelea kulipa ada bila shida tofauti na hapo nitaelemewa naomba unielewe kwa hilo, kuhusu makundi huyu ni binti yangu nitaongea nae na kwakua ni mkubwa atanielewa ondoa shaka..mkurugenzi akajibu mimi maamuzi yangu ndo hayo hivyo mkiamua basi mmeamua nyinyi ila mimi silitambui hilo swala...dooh ikawa shidah mama akaona sio kesi akamjibu sawa tumekuelewa basi akaaga tukaondoka. Tulipofika nnje nikamuuliza mama sasa itakuaje? Akajibu wewe kakae hiyo hostel unayoitaka mimi nitalipia ada tu hapa sina kingine hawezi kukutalia wakati hakulipii ada au mnamahusiano 😲😲 haaa mama hapana mimi siwezi na sijawahi kufikiria hata kidogo...basi akanambia maamuzi yangu ndo hao...kweli mama halishikiria hilo basi siku hiyo hakurudi nililala nae hosteli kesho yake akaondoka...niakwa naenda chuo kama kawaida muda wa kutoka naenda hostel ya nnje,,,mgurugenzi hakuwahi niita offisin kwake na hata nikikutana nae nikimsalimia haitikii...ile hali iliniumiza sana ikabidi nimshirikishe prisca akashangaa tu hakua na la kusema zaidi ya kuniambia niachane nae nisimfatilie.....niliendelea kusoma chuo vizuri tu lakini shida ilikuja ilupofika siku ya kwenda field...ualim hualazima kufanya field mbili yaan mwaka wa kwanza na mwaka wa pili, ya mwaka wa kwanza nilipangwa na nikaenda ila ya mwaka wa pili nashangaa bado siku mbili kwenda field hua majina yanabandikwa na shule utakayoenda sasa nilipoenda kuangalia sikuona jina langu ikabidi nimuulize mkufunzi anaehusika akaniambia ambao hawajapangwa wanadaiwa ada nenda kaongee na mkurugenzi..duuh mkurugenzi tena!!! Akili ilinienda mbio maana sikuwa na maelewano nae ikabidi niende tu nafika officin kwake nae anatoka tukakutana mlangoni akanipiga jicho akanipita akaondoka ikabidi nikae nnje ya office yake nimsubiri lakini nilikaa muda mrefu hakurudi ilibidi niondoke nikijua kesho pia siku nitakuja lakini nilikosa raha....kesho yake pia hakua offisin ni kama alikua anajua tu nitaenda nikawaza ni ada ipi nadaiwa wakati mama amelipa hela ya ada yote daah nilijikuta nalia tu....siku zilisonga bila mafanikio mkurugenzi sikufanikiwa kumpata nikaambiwa amesafiri ameenda dar esaalam nisubiri hadi arudi hivyo niliishia kukaa tu hostel wenzangu wakiwa tayari wameenda field hivyo hostel vyumba vyote vilikua havina watu nilikua mwenyew tu huku sikuacha kwenda chuo kuangalia kama mkurugenzi amerudi...mama nilimpa taarifa alikua akimpigia mkurugenzi hila apokei sim....siku hiyo nilienda chuo nikakuta mwalim wa nidham yupo nikakaa nae kumueleza tukuo zima linalonikuta kwanza akacheka sanaaa nikamuuliza mbona unacheka akasema kwani hujui kwanini anakufanyia yote hayo nikasema sijui akasema ngoja nikwambie..........
ITAENDELEA
Tags:
CHOMBEZO