SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA 2

Mlango ulifunguliwa nilitoa macho kujua ni nani, alikua ni mwenzangu ntakaekua nalala nae kwenye chumba hicho, yaani kuingia tu alinipokea na tabasam ziito daah nikajikuta natabasam, karibu dear alinikaribisha nami nikaitikia asante mpnz nishakaribia,,,alikua ni mdada mnene mwenye umbo zuri tu yaani mwili wake uliendana nae na ulimpendeza hasa na hakua mwenye majivuno yaan alikua mkarimu kupita kiasi na mpole sana asiyependa makuu,,,tulitambulishana pale tulipotokea na kunitajia jina lake kua anaitwa prisca nilifurahi kwakweli kupata mtu msaharabu wa kuishi nae....maisha ya chuo yalianza na wala sikua na shida na kama mnavyojua maisha ya chuo kidogo watu wanakua na akili za utuuzima,,,,siku zilienda na hatimae nikamaliza mwaka wa kwanza bado mwaka mmoja nimalize maana ualim ni miaka miwili....lakini pamoja na yote maisha ya chuo sikuyapenda maana tulikua tunafanywa kama wanafunzi wa secondary yaani vyuo vya ualim vina sheria sana muda mwingine hadi inakera....kilichokua kinanikera sana mnapangiwa mda wa kula,kulala na kusoma na ikifika muda wa kula ni mwendo wa kupanga foleni kupokea chakula unaeza kuta unakaa foleni mda mrefu mpaka muda wa kuingia kusoma unakukuta hujala inabidi uailishe hasa wakati wa usiku na vyakula vilikua haviridhishi ni kama wanafunzi wa secondary wanavyokula na huruhusiwi kujipikia na hapo ada ni kubwa sana nikaona hii sitawezana nayo baada ya kumaliza mwaka wa kwanza ikabidi nimshauri mama nihamie hostel za nje bei ilikua nafuu sana na niliipenda pia maana ilikua karibu na chuo na ilikua ni ya wanawake tu wanaume hawaruhusiwi kuingia hivyo usalama ulikuwepo na ilikua unakuta chumba kina kila kitu yaan kitanda,godoro,meza na kiti ila unajitegemea chakula na unaruhusiwa kuweka vitu vyako kama unavyo yaani unaishi kama nyumbani ila ni wanawake tu....nilimshawishi mama na akaridhia maana alikua anasomesha watoto kama wa nne wakiwemo na watoto wa ndugu zake, hivyo ni kama ilikua inampunguzia gharama kidogo..akaniambia unatakiwa uombe ruhusa kua utatoka hostel ya chuo nikaona si shida maana wengi hua wanahama hostel za chuo wanakaa nnje na wanaruhusiwa na wapo wanaokaa kwao alafu wanakuja chuo kusoma na kuondoka....basi baada ya kufunga chuo kabla ya kuondoka nilienda office ya mkurugenzi kuomba ruhusa ya kutoka nnje ya chuo lakini cha ajabu mkurugenzi akakataa 😲 nilishangaa nikamuuliza kwanini unanikatalia akasema mama yako alinikabidhisha kwangu hivyo sitoruhusu utoke hostel,,nikamwambia lakini mbona mama ameridhia ngoja nimpigie uongee nae, akasema hata ukipiga sitokubari utoke nnje ya chuo...aisee nilishikwa butwaa kwani shidah iko wapi maana wengine wamepewa ruhusa kutoka ila mimi nakataliwa shidah iko wapi sikujua,nilimbembeleza sana mkurugenzi lakini alikataa na akanifukuza nitoke offisin kwake duuh sikua na namna nilitoka kinyonge huku nikiwa sina jibu kwa nini kanikatalia,, nilipofika nnje ya office nilimpigia mama na kumweleza kila kitu mama akasema, sikia mwanangu mimi ndo ninaelipa ada hivyo kama hiyo hostel ya nnje inanafasi nenda unipe niongee na muhusika kisha ulipie alafu urudi nyumbani ukifungua chuo nitakuja kuonana na mkurugenzi...kweli nilifanya kama nilivyoelekezwa na mama na nilifanikiwa kupata chumba kwenye hostel ya nnje na mama alituma hela nikafanya malipo kabisa na kuhamishia mabegi yangu hostel kisha nikarudi morogoro likizo nikiwa na furaha zooote 💃🏼 bila kujua kua najiingiza matatizoni kutoka nnje ya chuo bila mkurugenzi kupitisha.....
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post