SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA. 1



Paulina mpendwa naomba wafikishie wamama story yangu fupi tu najua kuna watakachojifunza......
    Naitwa winie ( si jina halisi) nina umri wa miaka 31, ni mtoto wa sita kuzaliwa kati ya watoto saba na katika familia yetu wazazi wetu walijaliwa kupata watoto wakike wawili tu mimi na dada yangu ambaye ni wa nne kuzaliwa wengine watano ni wakiume,,,ambapo kaka yetu wa kwanza na wapili wameshatangulia mbele za haki na mdogo wetu wa mwisho ambae ni wa kiume amepotea katika mazingira ya kutatanisha hatujui ameenda wapi tumeshatafuta sana na kuhangaika ila hatujafanikiwa kupata taarifa yake yotote na aliondoka tu nyumbani akiwa na umri wa miaka 15 hadi hivi leo ni miaka tisa sasa hatujui alipo tunaimani mungu anamlinda kwa ajili yetu....hivyo kwa sasa tumebaki watoto wa nne ndio tupo karibu na tuna mawasiliano.... Wazazi wetu walitengana mda sana ko kiufupi sisi wa mwisho tumelelewa na na mama tu ila hao wa kwanza walibahatika kulelewa na baba na mama. 
    Mama yetu alitulea malezi mazuri sana namshukuru mungu alikua ni mpambanaji alikua ameajiliwa selikarini hivyo maisha yalikua mazuri tu hatukuwahi kukosa kitu na tulisoma shule nzuri tu za kulipia,,wakati huo tulikua tunaishi morogoro....pamoja na malezi mazuri aliyotulea mama yetu lakini alikua ni mama mkali sana yaani huezi muingia kirahisi akakuelewa ni mama ambae kupiga ama kukufokea siku mbili mfululizo ilikua ni kitu cha kawaida hivyo tulitamani mama aende kazini kila siku maana akiwa nyumban lazima mtu atapigwa ama kugombezwa, haikutusumbua sana maana tulimzoea ikafika kipindi tukaona ni kawaida tu. Nilifanikiwa kusoma hadi form six ila sikufanikiwa kupata alama za kutosha kunipeleka chuo kikuu ila nilipata alama za kuweza kusomea collage, hivyo mama alinipeleka kusomea ualim ngazi ya diploma dodoma maana kwa kipindi hicho nilikua napenda sana ualimu.. Ntaeleza kwa ufupi ili tufike kwa lengo la story hii...
  Basi mama alifanya process zote na nikafanikiwa kupata nafasi katika chuo cha ualim kilichopo dodoma na siku ya kwenda chuo alinipeleka chuo na tulupokelewa vizuri na uongozi wa chuo,,lakini kitu ambacho nahisi mama labda alikikosea ni kunikabidhisha kwa mkuu wa chuo,, 
Alimwambia: nakukabidhi mwamangu naomba umwangilia kwa kila jambo ikitokea tatizo lolote naomba unijulishe...mama alitoa maelezo hayo kwa mgurugenzi naye akamjibu; usijali mama yupo mikono salama na hutakiwi kuwa na wasiwasi...basi mama akafanya malipo ya awali na kisha kuondoka na kuniacha. Mkurugenzi alimuita mwanachuo mwenzangu ambae alikua na uongozi akanikabidhisha na kumwambia anipeleke hostel,, alikua ni mdada tu mwenye mwili wake na kwa haraka haraka ukimtazama utajua tu ni wale wadada wakorofi yaan wababe fulani hivi ukiingia kwenye kumi na nane zake,,,,alinibebea mizigo yangu tukaongozana hadi hostel zilikua humohumo ndani ya chuo,,,tukafika hadi chumba nitakachokua nalala,kilikua kidogo tu na kilikua na deka moja hivyo tunalala wawili yaan zile hostel vyumba watu wana kaa watu wawili wawili tu vichache sana watu walikua wanakaa watatu ama wanne....daah niliingia nikamshukuru akaondoka nikajisemea naanza maisha ya chuo sasa,,hapo nnaekaa nae alikua yupo darasani maana nilifika muda wa mchana, nikawa naomba tu nitakaekua nakaa nae awe mstaharabu maana maugomvi siyawezi napenda sana amani....ghafla mlango ulifunguliwa nilitoa macho kujua ni nani......
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post