*MWANAMKE*, akilala na hali mumewe *amemkasirikia*, basi hulaaniwa na Malaika *usikukucha*.
💞Lakini sikujuwa kua *kuna na kinyume chake*.
.. Ilitokea katika khutba ya Ijumaa, lilitokea jambo ambalo si lakawaida, jamaa mmoja alimshitaki mkewe kwa Shekhe wa msikiti mbele ya watu..
SHEKHE akamjibu kua mwanamke hubeba jukumu kubwa la nyumbani kwake... na kuyavumilia mambo mengi kumshinda mwanamume, kwa mara zaidi ya mia na mia, na hata lau angekua huyo mwanamume ana misiba au matatizo mengi na akasubiri, lakini subira za mwanamke ni *kubwa zaidi*..
HAPO hata sauti ya huyo Shekhe ilianza kubadilika alipokuwa anamsemesha huyo mwanamume alomshitaki mkewe na kumwambia:
*Mkeo amebeba mambo yako na ya watoto wako*, na anasimama kwa miguu yake *kuwatengezea chakula chenu*. Na Mtume (s.a.w.) ameshausia hivo..
*Jee kwani hana haki yeye ya kuheshimiwa* ? *Na ya kuthaminiwa*? Bila ya kumpunguzia chakula au kitu chochote anacho kihitaji?
BASI naapa Wallahi *lau mwanamume anamkasirisha mkewe*, *akamgeukia* na *kumpa kichogo* akatoka nyumba kumwacha mkewe na *huzuni*, basi Mwenyezi-Mungu anamlaani kwa kila khatwa anapokwenda, na *kumyimia rizki yake*, na kumpunguzia *afya yake*, na *kumuandikia kwa kila chozi moja linalotoka machoni mwa mkewake huyo*..
makaa ya moto elfu moja kila siku, nusu yake duniyani, na nusu kesho akheera..
*NATAMANI* maneno haya yawafikie wanaume wengi walokwisha *OWA*...
*Machozi mangapi mengi yashamtoka mke wako na wewe hata hujali kabisa*, wala huna *hamu ya kitu chochote*, wala *hutaki kujua habari yake*..
Musiyawache maneno haya *kubakia moyoni mwenu tu*, bali kila mtu awatumie *walokwisha owa*. Na *ambao hawaja owa* wahifadhi maneno haya kwa umakini kabisa kama hakiba ya kesho inshaaaallah watakapo owa..
AMESEMA Amiir Talaal Ar-Rashiid, Mungu amrehemu,:
(( .. *Kama aliumbwa mwanamke kuwa ndege angekuwa ni*
"Tausi", *الطاووس*
na kama aliumbwa kuwa *mnyama angekuwa* ni
"Paa" (Ghazala), *غزالة*
na kama aliumbwa kuwa mdudu angekuwa ni
"Kipepeo" (Butterfly), *الفراش*
lakini ameumbwa kuwa *MTU*, kwa hivo yeye ndiye *Mpenzi*, na ndiye *Mke*, na ndiye *Mama bora*, *Mtunza siri zako , Mshauri mwenzako , Mama wa Wanao , Yeye ndio Shamba yako Panda utakavyo na vuna ulivyopanda na ndiye Neema nzuri kabisa ya mwanamume katika *ULIMWENGU*
Hakika nimependezewa na Mwanamke kwa kuwa:
"Ni kiumbe ambaye *unaweza*wewe Mwanaume kuishi naye kwa urahisi na vilevile kwa vigumu kabisa, unaweza *kumridhisha* kwa ua moja la waridi, na unaweza *kumuuwa* kwa neno moja..
*JITAHADHARI* ewe mwanamme ujue kuwa mwanamke *ameumbwa* kwa *mfupa wa ubavu wako* si *kwa mguu wako hata umkanyage*...wala si kwa *kichwa chako hata umpandie juu ya kichwa* chake, lakini *ameumbwa kwa mfupa wa mbavu zako ili umueke ubavuni mwako*, na ni kwa mfupa ulioko karibu na *moyo* wako ili upate *kumpenda*..
Mwanamke ni kiumbe bora kabisa...
Katika utoto wake *humfungulia babake mlango Peponi*...
Na katika *UWARI WAKE* wake humtimizia mumewe dini yake...
Na anapokuwa *MAMA*, Pepo huwa chini ya miguu yake...
Maneno mazuri kabisa.....
Nampa salamu na pongezi kila ambaye ni *Mwanamke* mwenye sifa njema...
Shukran kwa kila atakaye yasoma maneno haya, na kila *atakaye yatuma kwao wanawake* na *akaingiza furaha katika moyo wa kila msichana*, na kila *ndugu wa kike*, na kila *mke*, na kila *mama*...
*NAKUOMBA MTUMIE KILA YANAYOMHUSU* .
Tags:
KUNGWI WA MAPENZI