JIRANI 01👯



( watoto mtupishe kidogo)

Nyumba yangu upande wa nyuma ilikuwa na dirisha kubwa liliniwezesha kuziona nyumba zote za majirani vizuri.Nyumba zote zilizonizunguka zilikuwa na Fensi ya tofali, lakini kutokana na urefu wa nyumba yangu kwenda juu sana, niliweza kuangalia ndani ya fensi ya nyumba zilizonyuma yangu.

Nilikuwa nyumbani kwangu kwa karibu mwezi mmoja ndipo nilipogundua nyumba ya jirani iliyokuwa inauzwa kuna familia mpya inahamia. Nikiwa dirishani niliwashuhudia wakiingiza vitu ndani.

“ Ni busara kwenda kuwasalimia wageni.” Nilijiambia.

Nilitoka chumbani kwangu na kuelekea dukani. Nilinunua mkate mkubwa wa elfu mbili na kuelekea nao kwa majirani zangu wapya waliokuwa wanahamia.

“ Karibuni sana.” Niliwasalimia nikinyosha mkono wangu. Mwanamke aliyekuwa anashusha vitu kwenye gari aliupokea na kujitambulisha.

“ Ahsante kwakutukaribisha. Naitwa Jenifer.” Aliniambia.

“ Naitwa zakia.” Nilimjibu.

“Mtaa wenu umetulia sana.” Alianzisha mazungumzo.

“ Ni kweli, Mtaa huu wanakaa watu waliostaharabika. Hakuna kelele wala vurugu zisikokuwa na msingi.” Nilimwambia. Tukiongea hayo, mlango mkubwa ulifunguliwa, alitoka mkaka ambaye nazani alikuwa Mume wa jenifer.

Nilimsogelea na kumpa mkono wa kumsalimia.

“ Karibuni sana shemeji.” Nilimwambia.

“ Mmmmh! kwanini umemuita shemeji?” Aliniuliza Jenifer. Alitembea kuja tulipo.

“ Huyu sio shemeji yako, mimi na yeye tumezaa mtoto mmoja ambaye ni huyu hapa anaitwa Enock. Lakini hatuishi pamoja, hata hapa anahamia yeye tu! Mimi nimekuja kumsaidia kuweka mambo sawa.” Aliongea Jenifer huku akisogea kwenye gari kushusha vitu. Tembea ya Jenifer haikuwa kawaida, ni kama aliteguka kiuno.

“ Naitwa Michael, kama Jenifer alivyokueleza. Nitakuwa naishi hapa na mwanangu Toddy.” Aliniambia huku akimshika kichwa mwanae.

“ Ok sawa, karibu sana. Niliona nije niwasalimia mara moja, kama nilivyojitambulisha kwa Jenifer, mimi naitwa Zakia. Nakaa kwenye nyumba ile pale. Mimi ni mwenyeji hapa, mkiwa nashida yoyote mnitaarifu.” Niliwaambia.

“ Ahsante.” Walinijibu. Nilipiga hatua kutaka kuondoka, lakini hali ya Jenifer jinsi alivyotembea ilinipa shida. Niliamua kumuuliza.

“ Jenifer upo sawa! Hiko kiuno vipi?” Nilimuuliza.

Jenifer badala ya kunijibu alimtazama Michael, tena hakumtazama usoni, alimtazama Michael chini ya kiuno.

“ Mmmmh!” Niliguna.

“ Utanisamehe! Tumekutana leo, halafu nakuwa na maswali yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Samahani sana.” Nilimwambia.

“ Usijali, ni jambo la kawaida. Sio wewe tu wengi wananiuliza kuhusu kiuno changu. Ila ukweli naujua mwenyewe. Hali hii ndio chanzo cha mimi kuachana na Michael.” Aliniambia.

“ Eeeeh!’ Nilishtuka. Haraka niligeuka kumtazama Michael.

“ Acha kuwachanganya watu. Inakuwaje kiuno chako ndio chanzo cha mimi na wewe kauchana?” Aliuliza Michael.

“ mmmmh! jamani msilumbane kwa ajaili yangu.” Niliwaambia. Niliwaga na kuondoka. Nikiondoka Jenifer macho yake yote yalikuwa kwenye suruali ya Michael, hali iliyonifanya na mimi nitembee huku nikiingalia Suruali ya michael.

……………………….

Siku ya pili, majira ya saa kumi alasiri nilichungulia dirishani nikamuona Michael akiwa kwenye bwawa la kuogelea lilikouwa nyuma ya nyumba yake, Sura yake nzuri, kifua kilichojazia na misuli iliyojaa vilinifutia, nilijikuta nameza mate.

“ Mkaka mzuri yule.” Nilitamka.

“ Lakini si yupo single! Acha nikajaribu bahati yangu.” Nilijiambia. Nilivaa nguo ya uchokozi kisha nikatoka nje. Nilienda getini kwake na kugonga mlango.

“ Nani! Ni zakia au?’ Aliniuliza.

“ Ndio ni mimi.” Nilimjibu.

Sekunde kadhaa mbele , geti lilifunguliwa na michael akiwa kifua wazi na tight tu kwa chini. Nilipoitazama taiti yake, moyo ulipiga.

“ Paaaa…paaaa…paaaa…” Moyo ulipiga kasi. Kwa haraka sana nikajikuta nimegundua sababu ya Jenifer kushindwa kutembea vizuri. Kiherehere changu kikaisha pale pale, niligeuza kutaka kuondoka, lakini Michael aliniwahi, alinishika mkono na kunivutia ndani.

Itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post