MREMBO MCHARUKO-5 - 6

 


MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

Mwahija yule shogayangu akanisogelea,
"Wewe Lisa umecheza hadi kanga imevuka huna habari hii hapa niliokota mie nikaishika"
Alisema nilimshukuru sana.
"Mwezangu sijui ningeendaje nyumbani asante mwaya"
Basi akanipatia tatizo giza lishaingia kurudi mbali nikamuomba kama anabuku aniazime nitamlipa nipande bodaboda.
"Hata sikuazimi chukua tu shogayangu"
Nilimshukuru zaidi tukaagana nikasogea mbele kidogo kijiweni, nikapanda bodaboda moja ikanipeleka karibu na nyumbani nikashuka nakutembea kidogo nikaingia ndani hapo moyo unanidunda balaa najua kipigo leo lazima.
Basi ile kuingia tu nikakutana na baba sebuleni kavimba balaa alinisogelea nakuanza kunitandika na mkanda wake wa kijeshi nilipiga kelele nililia hadi mama akatokea kunigombelezea.
"Utaua baba Lisa msamehe mtoto"
"Acha afe shenzi huyu mtoto asikii kama kalambishwa mavi sijui ameniona narudi kanipita mbio kaenda kucheza ngoma muone ananuka jasho balaa hapo Lisa utanipa kesi nakwambia nitakuua wewe"
Nilitoka mbio nikaingia chumbani nakujifungia nalia huku baba alizidi kufoka tu Mama akamtuliza nakuingia chumbani.
Nililia hadi nilipotosheka nikaenda kuoga nilipomaliza nilisikia njaa inauma sana, Mara Ghafla mlango wangu ukagongwa
"Nani wewe?"
Niliuliza kabla sijaenda kufungua.
"Mimi Leah"
Nikamfungulia namuona kabeba sahani ya chakula.
"Lisa mdogo wangu pole chakula hiki kula mwaya"
Mwenyewe alikuwa anahuruma namimi nikamshukuru nakuanza kula uku amekaa ananitizama.
"Wewe huendi kulala kwani?"
Nikamuuliza.
"Nakungoja wewe umalize nibebe vyombo"
Nikamuangalia sikumjibu nilikula hadi nilipomaliza nikampa vyombo.
"Lakini mdogo'angu punguza mcharuko ona kilasiku baba anakupiga"
akajifanya ananipa ushauri.
"Bibi wee koma ushauri pelaka Angaza tafadhari sijakuita hapa kunipa chakula isiwe nongwa nitakitapika chote uondoke nacho unajifanya mwema ngoja ugeuzwe msukule"
nilimpa maneno mabaya hadi alikoma mara mama nae akaingia chumbani.
"Nimekusikia mtoto unamaneno machafu wewe lione kama zimwi"
Mama naye yumo kwa maneno nikabaki namtizama sijui nimjibu nini.
"Wewe Leah ungeliacha lilale na njaa hili halina shukrani kabisa"
Mama aliongea huyo hadi basi Leah akatoka zake nakumuacha.
"Halafu mimi naisi kweli mliniiba hospitali si mtoto wenu mimi maana hamnipendi kabisa naishi kama nipo utumwani na nitajiua mbaki wenyewe"
Nilimwambia mama akashtuka na maneno yangu.
"Lisa mimi ndo mamayako mzazi niliekuweka tumboni miezi tisa nakukuzaa kwa uchungu unaanzaje kusema nimekuiba sisi tunakuchukia tabia zako mbaya" Mama alisema.
"Tabia mbaya nimejikojolea kitandani?"
Nilishtukia kofi la uso nimepigwa, mama akatoka nje nakuniacha nikafunga mlango nakulala.
Asubuhi ilifika sikuamka hadi mchana nikaunganisha kulala hiyo siku ilikuwa wikiendi wote wapo nyumbani wakashangaa kwanini nimelala sana wakaja kugonga mlango ndo nikashtuka saa nane mchana mwili wote unauma kwa kipigo cha jana. Mama ndio alikuja kuniamsha nakuniuliza najisikiaje nilipomambia naumwa akaniletea dawa yakupunguza maumivu ila nikaenda kula kwanza.
***
Siku sikazidi kusonga hadi majibu yalipotoka nikaonekana nimefaulu hakuna alieamini kama Lisa mie nimefaulu kuingia secondari.
Tatizo likaja nimechaguliwa shule mbali Tegeta uko nilichukia sana.
"Bora ningefeli tu ndo nini kupelekwa kijinini huko?"
"Lazima ukasome huko huko kwanza sijui kama ujawapa rushwa wakufaulishe"
Baba akaingilia.
"Mimi nina wazo mumewangu tumuamishe Lisa shule anayosoma kakayake"
Mama akasema nakumfanya baba achukie sana.
"Unasemaje? Yani nitoe pesa zangu kwaajili ya huyu kichaa nina wazimu au?" Alifoka kwa hasira nakuinuka akaondoka nakutuacha.
"Ngoja nitakufanyia mpango nikupeleke hata Yusuph Makamba ukasome hapo"
Alisema Mama hiyo shule ipo karibu na kwetu basi nikamkubalia, nikiwa pekeyangu nililaani kufaulu nilitamani nifeli tu basi nilichukia.
Hatimae siku yakuanza masomo ikafika Mama akafatilia uhamisho hadi yalipokamilika nikapelekwa shuleni kuanza. Basi siku ya kwanza tu kufika nikapigana na mwezangu ambaye alikaa kwenye kiti changu nilimdunda hadi akatoka damu puani alikuwa msichana anaitwa Mwantumu.
Basi tangu siku hiyo shule nzima nikajulikana Lisa ni nani nikapata mashoga wengi micharuko wenzangu hadi nyumbani wakawa wanakuja tunapiga stori mwisho wanaondoka.
Kaka Gedion akanichongea kwa baba ambaye alipogundua naleta marafiki zangu akanipiga stop kuwaleta nyumbani alinikera.
"Halafu huyu atakuwa si babayangu sio bure"
Nilijisemea nikapanga nimuulize mama vizuri ambapo aliporudi tu nikamuwahi bila salamu.
"Mama kanionyeshe babayangu mzazi alipo"
Nilimwambia akashtuka kwanza nakusema.
"Babayako wakutokea wapi tena na huyu unaeishi naye hapa ninani?"
"Huyu si babayangu namtaka babayangu wa kweli nasema"
Nilichachamaa nikimlazimisha anionyeshe babayangu.
"Wewe mpuuzi usinisumbue mimi nimechoka"
Mama alisema akanipuuza nakuondoka.
Asubuhi ilifika kama kawaida nikajiandaa kuelekea shuleni sikuacha mcharuko wangu nilizidisha hadi nilipofika kidato cha pili siku moja tunatoka shule rafiki zangu wawili wakanifuata.
"Shosti leo ijumaa twende zetu Coco beach wikiendi ishaanza hivyo"
Alisema Salma na mwezake Diana akadakia.
"Ndio twende mwezangu tukaogelee"
Mimi niliogopa tutachelewa kurudi na baba namjua atanipa kipigo nikawakatalia.
"Twende Lisa hatuchelewi bwana wendo mrembo wetu tunakutegemea"
Alinishawishi Diana basi nikakubali tukaondoka nakupanda gari la Msasani, tulishuka macho tukachukua bodaboda hadi Coco.
Ilikuwa bado mapema shule tulitoka saa sita hakukuwa na foreni saa saba na nusu tukawa Coco tayari.
Basi wezangu walikuwa na pesa tukakodisha nguo zakuogelea hapo kila mmoja akachagua yake tukavaa nakuvua nguo za shule tukaogelea hadi tulipochoka tukaanza kukimbizana kwenye michanga tulifurahi siku hiyo hadi saa kumi jioni tukaanza kujiandaa kuondoka. Mara nikasikia naitwa na mwanaume nikageuka nimsikilize ni mbaba mkubwa.
"Hujambo Mrembo?"
"Sijambo shikamoo"
"Asante"
Alijibu huku anatabasamu alinichefua sana nikataka nianze kumchamba maana sicheleweshangi ghafla wakaja mashoga zangu nakumsalimia kwa furaha yule mbaba.
Kumbe wenzangu walikuwa na mabwana tayari mie ndo nilikuwa mgeni sina mpenzi na mwanaume akinitokea nampa matusi hadi anakoma.
"Sisi tunaelekea ubungo tupeleke basi"
Salma akamwambia yule baba akakubali basi tukajiandaa nakuvaa nguo zetu za shule tukapanda gari lake nakuanza kutupeleka
"Nimempenda sana Lisa natamani awe mpenzi wangu"
Alisema huyo mwanaume ambaye alitwambia anaitwa Mr Antony.
"Lisa muoga huyu ila usijali utampata tu"
Diana alidakia kusema nikataka kuongea akaniwahi kuniziba mdomo maana ananijua nipoje.
Basi alipitia njia ya Shekilango akakatiza makaburi ya Ufi nakutokea Shungashunga ndo maeneo ya kwetu walianza kunipeleka mimi kwanza lakini hatukifika nyumbani ila tulipo nyumba yetu inaonekana basi nikaagana nao nakutelemka ile nashuka tu kwenye gari nikaona gari la baba limesimama pembeni akatelemka nakuja nilipo hata kabla lile gari halijaondoka akanifikia.
Itaendelea.
MREMBO MCHARUKO-6
MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

Baba alipofika akaninasa kofi moja bila kuongea akasogea hadi kwenye gari nakugonga kioo.
"Fungua mlango toka nje" alimwambia yule mwanaume aliyekuwa ndani ya gari, ambaye alifungua kioo kumsikiliza baba aliyekuwa amevaa magwanda yake yakijeshi nilijua muda huo ndo alikuwa anatoka huko kambini kwake Lugalo.
"Habari yako muheshimiwa?"
Alianza kusalimia Mr Antony,
"Salama, samahani nimeona binti yangu akishuka kwenye gari lako unaweza kuniambia umemtoa wapi leo ijumaa shuleni wanatoka saa sita mchana na sasa hivi ni saa kumi na moja niambie umetoka nae wapi" aliongea baba akiwa siriasi zaidi alikuwa anakunja mikono ya nguo yake yakijeshi nakuifanya iwe fupi mikononi akionyesha hana masihara anaweza kumpiga huyo mwanaume anaeongea naye nilipomuangalia alionyesha anauoga kwa mbali ila alijitahidi kujikaza.
"Oh kumbe ni binti yako mimi nilimkuta coco beach akiwa na rafiki zake wawili wapo humu kwenye gari ngoja niwaite"
Akawaita wale mashoga zangu ambao waliteremka wakatoka nje nakumuona baba alivyo uoga uliwajaa walitetemeka hovyo.
"Ndo hawa marafiki zake niliwaona coco nikawachukulia kama watoto wangu nikaamua kuwasaidia niwapeleke majumbani kwao ndio nimeanza na huyo ulosema binti yako bado ninasafari yakuwapeleka hawa wengine majumbani kwao"
Alijitetea Mr Antony nakumfanya baba awageukie wale wenzangu Diana na Salma.
"Aliyosema huyu baba ni kweli au?"
Aliwauliza akiwakazia macho wote wakatingisha kichwa kukubali,
"Mlipoenda uko coco mlitoa ruhusa majumbani kwenu na wewe Lisa unaanzaje kwenda bila kuaga nyumbani mlifuata wanaume uko eeh?"
Baba aliwauliza akawashushia makofi wezangu wote waliobaki wanalia kisha akamwambia yule mwanaume awapeleke kwao kesi ikabaki kwangu sasa alinibutua hadi tunafika nyumbani
"Ole wako siku nyingine utoke bila kuaga shenzi wewe"
Yani nilikuwa napigwa sana ila sikomi nikaingia chumbani nikalia nakumlaani baba bora afe kabisa.
Mama aliporudi akaambiwa hata hakuniuliza yeye alishachoka kuongea.
Basi siku zikazidi kusonga hadi nikaingia kidato cha tatu bado niliendelea kuwa mtukutu baba ananipiga tu hadi nikamaliza kidato cha nne nilishukuru Mungu hapo nikajiona nishamaliza masomo tena nilizidi kutanuka nakuwa mkubwa nilifikisha miaka kumi na nane basi nilijiona mtu mzima kabisa, sifai kupigwa sikutaka hata kungojea majibu nikaomba nipelekwe kwa bibiyangu Songea nikakae nimkimbie baba maana shule nimemaliza ningekuwa nazurura kilasiku ningedundwa na baba muhimu kuondoka kwake.
Siku moja usiku tunakula nikaanza maongezi.
"Nimemkumbuka bibi yangu mimi nataka nikamuone tena nikakae huko hadi majibu yakitoka"
Niliongea kiunyonge mwenyewe.
"Ila bora ukakae kijijini labda utajua kazi umelegea kama mlenda vile" Mama alisema baba akaniangalia.
"Najua unanikimbia sawa nenda kule kuna babayako mdogo nitamwambia akulinde ukitoka tu akupige"
Nilichukia maisha gani yakupigwa kilasiku nikajikuta namchukia babayangu kuliko shetani nilimuangalia nikatamani nimuwekee sumu afe.
"Sawa anipige tu nishazoea si mnanifanya mie ngoma"
Nilimjibu baba
"Katulie mwanangu hatokupiga babayako mdogo usijali"
Mama alisema sikumjibu nayeye nikainuka nakuelekea chumbani kwangu.
"Jiandae kesho safari Asubuhi na mapema"
Baba alisema nikaondoka zangu nimenuna.
Basi nilifika nikapanga nguo zangu vizuri nakuweka nikaingia kulala.
***
Asubuhi kulikucha nikajiandaa nakutoka nikawaaga wote baba ndie alinipeleka hadi standi ya mkoa ubungo akaniacha nimepanda gari nayeye kuondoka.
Basi saa mbili Asubuhi safari ikaanza nilikuwa na simu hapo tayari mama alininunulia, nikaanza kuchat na mashoga zangu nikiwaaga naenda kijijini
"Loh shosti umeishiwa na urembo wote ukaishi kijijini aibu"
Alinambia Nasra.
"Mwezangu babayangu kazidi kunipiga nimeona niondoke tu"
Nikachat hadi saa nane sijui tumefika wapi pale nilichoka nakulala zangu kwenye kiti.
Nikaja kushtuka imefika saa kumi na mbili giza limeanza kuingia.
Ghafla tukatokea porini barabara haionekani kila mtu akashangaa
"Tumefikaje huku wewe dereva vipi?"
Watu wote walishangaa tukamsogelea dereva tumuulize tukamkuta amelala huku damu zinamtoka na kondakta hajulikani wapi alipo hapo wote tulijawa uoga kila mtu akatoka kwenye gari nakukimbia hovyo mie begi lilikuwa zito nilitupa huko nakutoka mbio nisijue wapi naelekea, kila mmoja alikimbia njia yake gari likabaki na dereva aliyekufa tu.
Usiku ulishaingia, nilikimbia nikiwa pekeyangu nikatokea porini zaidi kunatisha huku milio ya wadudu inasikika.
"Mama wee nakufa mimi uuuhh"
Nikaanza kulia giza limetanda sioni mbele wala nyuma natetemeka kwa uoga nikasogea kwenye mti mkubwa nakukaa chini nimejikunyata hapo hofu imenijaa sina tumaini lolote.
"Mungu ipokee roho yangu"
Hapo ndo nilikumbuka kuna Mungu kumbe wakati mama alipokuwa ananiambia niende kanisani nilikuwa nagoma leo yamenikuta sasa nilijuta bora ningebaki tu nyumbani safari yakijijini imekuwa ndo mwisho wangu.
"Nakufa mimi leo"
Nilizidi kutetemeka mara kwa mbali nikaona miale ya moto watu wanaimba nakuja kule nilipo nikatamani nikimbie ila nguvu nilikuwa sina hatimaye wakanisogelea wakinishangaa sana walikuwa wanatisha niliisi wachawi walivaa kaniki chini juu vifua wazi ni wanaume watatu.

Elfu moja mwendelezo hadi mwisho.
Voda 0763361677
Tigo 0719618409
Jina Lisa Ntanga. Ukilipa nitumie muamala wasap.

Post a Comment

Previous Post Next Post