MREMBO MCHARUKO-7 -8



MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

Walizidi kunishangaa huku wakinimulika na ile miale ya moto usoni, hatimae mmoja akaongea nakuniuliza.
"Unaitwa nani?"
"Naitwa Lisa"
"Umetoka wapi umefuata nini huku kwenye ufalme wa Odinya?"
Aliuliza lakini sikumuelewa.
"Mimi nimetoka Dar es salaam nilikuwa naelekea Songea kwa bibi yangu kuna sehemu tulifika ni porini hakuna aliejua tupo wapi tukamsogelea dereva tumuulize tumemkuta amekufa wote kwenye gari tukatoka nakukimbia ndio mimi nimefika hapa"
Nilijielezea nakuangua kilio kikubwa wale wanaume wakaangaliana nakusema wanisaidie
"Tumpeleke kwa Mfalme huyu" Wakasema nilishtuka nikajua napelekwa kuzimu sasa.
"Kwani nyie ni wachawi au?" Nikawauliza nakuwafanya wacheke halafu mmoja akanijibu
"Sisi ni watu kawaida ila tunaishi kiutamaduni yani kiasili pia tunamilikiwa na mfalme usiogope sisi watu wema twende tukusaidie"
Basi waliposema hivyo kidogo uoga ukanipungua nikainuka nakuongozana nao, walikuwa wanaimba nyimbo zao zakushangiria sijui hata sikuwaelewa.
Tulipita maporini humo huku ile miale ya moto ikitusaidia kuona mbele hatimae nikaanza kuona kwa mbali nyumba baadhi huku moto umewashwa kwa nje. Tulizidi kusonga hadi tulipofika kwenye hiko kijiji chao moja kwa moja nikapelekwa kwenye nyumba kubwa nje wamesimama walinzi walioshika mikuki mikononi mwao tukawasogelea.
Basi wakasalimiana nakuomba waingie ndani kuonana na mfalme ambapo walikubaliwa tukaingia wote.
Aliitwa kijakazi mmoja akatumwa amwambie Mfalme kuna wageni wake nje ambapo baada ya muda mfupi alitoka nikamuona mwanaume wa makamo tu si mtu mzima sana alikuwa amevaa nguo za kijadi kama mganga vile.
"Uishi miaka mingi ewe mfalme wetu"
Walisema huku wameinamisha vichwa vyao chini namimi nikawageza nikainama.
"Karibuni"
Alisema huyo mwanaume ambaye ni Mfalme kisha akasogea kwenye kiti cha ngozi nakukaa.
"Ewe Mfalme wetu mtukufu huyu binti tumemkuta porini usiku huu amesema kapotezana na wenzake tumeona kuliko kumuacha msituni auliwe na wanyama tukaamua kumleta mbele zako ili umsaidie"
Aliongea mwanaume mmoja kati ya wale walionikuta porini kule.
"Kwasasa ningependa apumzike hadi kesho ndio niamue nini kifanyike juu yake! Somoiyeee njo haraka"
Aliisema Mfalme nakumuita kijakazi mmoja jina lake Somoiye ambaye alikuja nakuinamisha kichwa kwa adabu zote.
"Naam mtukufu Mfalme"
Alisema akiwa ameinama bado.
"Mchukue huyu msichana kampeleke chumba cha wageni mpe chakula ashibe na maji aoge kisha mbadirishe nguo hizo"
Alisema Mfalme
"Sawa mtukufu Mfalme"
Aliitikia huyo binti Somoiye akanishika mkono tukaondoka hapo nakunipeleka kwenye nyumba moja iliyokuwa ya udongo imezungushwa na nyasi.
Tukaingia ndani ambapo kulikuwa na mkeka chini uku pembeni kuna kitanda cha kamba na shuka juu.
"Unaitwa nani?"
Aliniuliza
"Naitwa Lisa"
"Ooh Lisa liene"
"Sio hivyo ni Lisa tu"
"Yani nimeongeza maana yake umekuja mwenyewe"
Alisema ila sikumuelewa
"Ngoja nikakuletee chakula kwanza"
Alisema akainuka nakutoka humo ndani kulikuwa na kibatari kinawaka ndo mara ya kwanza naingia nyumba ya nyasi kwani hata kwa bibiyangu sio kijijini ni Songea mjini nyumba yake ya tofari na kuna kilakitu ndani hadi maji yapo, sasa huku nilipokuja leo ndo mara ya kwanza kilakitu kigeni kwangu.
Baada ya muda mfupi Somoiye akaja na sinia limefunikwa juu
"Karibu Lisa liene"
Alisema nikamshukuru nilifunua nakukuta ugali na nyama yakuchoma nilikuwa na njaa nikaufakamia wote hadi nilipotosheka alinipa maji ya kunywa matamu hayo kama ya mvua.
"Kuishi huku hadi raha jamani"
Nilijisemea kimoyomoyo.
"Asante Somoiye"
"Usijali mrembo wangu"
Alikuwa mcheshi huyo mdada ambae kiumri yeye mkubwa kwangu basi akatoka na vyombo aliporudi alishika vitenge viwili na tait fupi moja akanipatia
"Njo nikuonyeshe bafu uoge kisha ukapumzike"
Alinambia nikatoka nakuingia kuoga hadi nilipomaliza akanisaidia jinsi yakujifunga hizo nguo, Kitenge kikubwa nilijifunga chini kiunoni na kingine kidogo kama kitop nikajifunga juu nikafanana na mavazi aliyovaa yeye sasa.
Baada ya hapo nikarudi kulala ndani.
"Usiku mwema kesho asubuhi nitakuja kukuona sawa"
Alinambia akaondoka nakuniacha nimejawa na mawazo siamini maisha yangu yamekuwaje.
Kulala kwenye kitanda cha kamba niliogopa nikalala kwenye mkeka chini, usingizi haukuja mapema nilikuwa na mawazo sana hata sijui muda gani nilipitiwa nikaja kushtuka asubuhi kumekucha.
"Lisa liene amka"
Ni Somoiye ndie alikuja kuniamsha nikashtuka nakutoka nae nje ambapo alinipeleka kwa Mfalme aliniitaji.
Sasa niliweza kuona hiko kijiji kilivyo madhari yake ilivutia kulikaa kiasili sana nakupendeza.
Nyumba nyingi za udongo na kuezekwa kwa nyasi zilienea maeneo mengi huku kukiwa na miti ya matunda mbalimbali na mboga za majani walizopanda nilizidi kushangaa sababu sikuwahi kufika vijijini nakujionea zaidi hii ni milki ya kifalme ambayo wanaishi kiutamaduni nilipenda sana kulivyo nikawa naangaza macho sehemu nyingi nakuangalia.
Basi nikafikishwa kwa Mfalme nakumsalimia ambapo nilimkuta na mkewake Malkia Tamara alikuwa mwanamke mzuri sana mwenye haiba ya upole.
"Unaitwa nani binti?"
Aliuliza huyo Malkia
"Naitwa Lisa"
"Ooh basi tutakuita Lisa liene maana yake umekuja mwenyewe"
Alisema akitabasamu nikamkubalia sawa.
Baada ya hapo wakaanza kunihoji nimefikaje kijijini kwao, nikawaelezea ilivyokuwa wakanipa pole nakuahidi watanisaidia jinsi yakuondoka kurudi nyumbani.
"Ila nimepapenda sana huku kwenu kuzuri naomba nikae hata mwezi mmoja"
Nikawaomba ili niendelee kujifunza mengi basi walikubali nakusema nitaishi nao hapo kwao nilifurahi sana.
"Inabidi lipigwe baragumu nakuwaitwa wanakijiji watambue uwepo wa mgeni hapoakijijini"
Alisema Mfalme na mkewe akakubali.
"Mashable kapige ngoma wanakijiji wakusanyike"
Aliamliwa kijana mmoja ambaye aliondoka mbio nakwenda kupiga ngoma.
Mara vijakazi wakaja na kifungua kinywa wakaweka kwenye meza moja iliyokuwa humo ndani tulipokaa ambapo Malkia akanikaribisha chai, Mara ghafla akaja kijana wa kiume umri wake kama miaka ishirini na tano hivi alikuwa amevaa mavazi yakifalme pia.
"Muishi miaka mingi Mfalme na Malkia"
Alisalimia baada ya hapo akakaa nakujumuika nasi
"Lisa huyu ni kijana wangu nina watoto wawili wakike ambaye ametoka yupo kwa shangazi yake na wakiume ndo huyu "
Alisema Malkia
"Muthan huyu anaitwa Lisa ni mgeni wetu hapa kijijini"
Alimuelezea mtoto wake ambaye alimuelewa utambulisho ukaisha hapo tukaanza kula pamoja, nilipata bahati sana yakukaa na kula na Mfalme na familia yake.
Huko nje wanakijiji walikusanyika wengi uwanjani ambapo ni mbele ya nyumba ya Mfalme basi tulipomaliza kula tukatoka wote pamoja nakuelekea uko kwenye uwanja ambapo kulikuwa na mikeka imetandikwa mingi watu wamekaa hapo kwa mbele kulikuwa na viti anavyokaa Mfalme na familia yake.
Ilikuwa sehemu maalumu kwa mikutano hakukuwa na jua walijenga kama ukumbi hivi ambapo likitokea tatizo wote wanakusanyika hapo.
Watu walikuwa wengi zaidi wamevaa nguo za kitamaduni walipendeza machoni mwangu.
Wakubwa kwa watoto walijaa hapo,
"Mdumu miaka mingi Mfalme na Malkia"
Walisema wote nakuinama kwa heshima.
Mfalme alisogea akakaa kwenye kiti chake cha ngozi sijui ya mdudu gani yule na Malkia pia akakaa kwake na mtoto wao akakaa pamoja na mie huku pembeni walikuja walinzi kama sita na mikuki yao wakasimama pembeni yetu kutulinda.
Mfalme akakohoa nakuanza kuongea na wananchi wake
Kabla ajaanza akatokea msichana mmoja kavaa nguo zake fupi sana anatembea kwa maringo huyo akasogea sehemu nakukaa huku akijipepea kama anasikia joto.
"Wewe binti uliefika sasa hivi uje uku mbele"
Aliongea Mfalme akiwa amechukia.
Itaendelea.
MREMBO MCHARUKO-8
MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

Yule msichana akasogea hadi mbele huku akionekana muoga sana.
"Uishi miaka mingi ewe Mfalme wetu"
Alitoa heshima kwa Mfalme ambaye alikuwa amekunja sura.
"Kazimta njoo umchukue huyu binti"
Aliongea Mfalme mara akaja mwanaume mwenye mwili mkubwa nakumbeba yule msichana.
"Nisamehe Mfalme nimekosa"
Alilia akiomba msamaha nilipigwa mshangao sikujua kosa lake ni lipi.
Mfalme akaanza kuongea.
"Mnaonyesha tabia mbovu kwa mgeni huyu binti hana heshima inawezekanaje Mfalme afike wa kwanza halafu yeye achelewe anakuja kwa maringo kama bata maji vile shenzi kabisa"
Alionyesha kweli amechukia sana.
"Tumepata mgeni huyu binti anaitwa Lisa"
Alisema Mfalme nakuniomba nisimame watu wanione utambulisho ukafanyika kila mtu akanijua sasa baada ya hapo watu wakatawanyika yule msichana ambae nilisikia anaitwa Shamima alisamehewa akaambiwa asirudie tena kuchelewa.
Maisha yangu mapya yakaanza hapo nikiishi kwa Mfalme nikiwa kama mmoja wa familia yao.
Baada ya siku chache kupita mtoto wao wa kike alirudi ambae anaitwa Nuhri alitambulishwa kwangu alifurahi kuniona umri wetu ulilingana tukazoeana nakuwa marafiki, nilipenda kujua madhari mengi ya hiko kijiji ambapo Nuhri akaomba ruhusa kwa wazazi wake tukawa tunatoka nakunitembeza sehemu mbalimbali nione kulivyo.
Siku moja vijakazi walikuwa wanaenda mtoni kuchota maji nikaongozana nao namimi nikabeba chungu kimoja kikubwa maana hakuna ndoo ni vyungu na maji mengine yanahifadhiwa kwenye mitungi yanakuwa ya baridi sana.
Basi tulifika tukakuta ugomvi msichana mmoja na Shamima
Ikabidi nisogee niulize kunanini.
"Mimi nimewahi kufika nachota maji huyu Shamima amekuja nakunipokonya kata halafu anachota yeye"
Alisema huyo msichana sikujua jina lake nani na huyo Shamima nilimjua sababu ya kumuona siku ile aliyochelewa kwenye kikao.
Nikatizama huyo Shamima kwanza
"Wewe kwanini usingoje mwenzio amalize kuchota maji ndio ufuate we zamu yako?"
Nilimuuliza msichana ananyodo sana alinitazama kwa dharau juu hadi chini akatoa msonyo nakutema mate iliniuma sana.
"Naisi hunijui kama mie naitwa mrembo mcharuko ngoja nikufundishe adabu ukasimulie wenzio"
Nilimwambia nikamvaa mwilini tukadondoka chini nikaanza kumshushia makofi alikuwa hata nguvu hana analia kuomba msaada wale wengine walipoona nampiga walishangiria sana.
"Mpigee huyooo amezidi kujiona mzuri hapa kijijini mkomeshe"
Nikasema kumbe ndo alivyo leo atanitambua tena alikuwa mwembamba mie bonge nilimkalia juu nilimpiga alilia sana nilipotosheka nikainuka.
"Haya omba msamaha"
Nilimwambia alikuwa analia tu.
"Inuka muombe msamaha Moze"
Yule msichana mwengine jina lake Moze nikamwambia amuombe msamaha akainuka nakumuomba baada ya hapo vijakazi wakachota maji tukaondoka nakurudi nyumbani.
Yule msichana alienda kwao akamshtakia mamayake ambaye alichukia sana wakabebana hadi kwa Mfalme wao kuja kushtaki.
"Mfalme tumeishi miaka mingi kwa amani kijijini kwetu hakujawahi kutokea ugomvi huyo binti mgeni ni mkorofi kampiga mwanangu kwanini?"
Mama aliongea kwa hasira huyo akimwambia Mfalme, mimi nilikuwa chumbani na Nuhri tukipiga stori nikamsimulia yaliyotokea alicheka sana, Mara akaja Somoiye kuniambia naitwa na Mfalme tukatoka wote na Nuhri tukaenda nilishtuka kumuona Shamima yupo na mwanamke mtu mzima nikajua ni mzazi wake.
Basi kesi ikaanza hapo nikasemwa kwanini nimepiga.
"Huyu binti anadharau sana halafu anajiona mzuri mwenyewe hivi mimi na huyo nani mzuri ebu niangalieni mbele na nyuma ananifikia huyo"
Yani akili zangu nazijua mwenyewe niliulizwa lingine nikajibu lingine nakusimama nikijigeuza wanitizame kwanza.
"Wewe mtoto sijafuata shepu yako hapa kwanini umempiga mwanangu?"
Alipandwa hasira yule mama,
"Nimemfundisha adabu sababu hawezi kunidharau mimi"
Niliongea hadi Mfalme akaingilia nayeye nakuomba tuyamalize tuombane msamaha.
"Looh nani amuombe msamaha huyu"
Nilikataa na yule naye akakataa mwisho wakafukuzwa waondoke
"Nitakukomesha wewe"
Alisema Shamimu
"Hehe halooo ingia anga zangu nikutoe manundu"
Nilimjibu nikikunja ngumi wakaondoka huku nyuma Nuhri aliangua kicheko kikubwa.
"Nakupenda bure Lisa yani umejua kunichekesha leo"
Alisema tukaingia ndani nakuendelea kupiga stori Mfalme yeye alikuwa ananiangalia jibu lakunipa hana tangu siku hiyo habari ikaenea kijijini nimepiga Mrembo wa kijiji Shamima ni msichana ambaye alikuwa anajisikia nakujiona mzuri sana anadharau hana heshima kabisa sasa alinipata kiboko yake nilimnyima raha sana sababu kijiji kizima alikuwa anatingisha yeye kuja kwangu kulimfanya asiwe na amani alinichukia sana halafu nilimzidi kilakitu basi alibaki anaumia tu.
Basi siku moja Asubuhi nikaona wanaume wengi wamekuja nakumchukua Muthan yule mtoto wa Mfalme wakiume wakaondoka naye siku mbali hakurudishwa ikabidi nimuulize Nuhri.
"Muthan kapelekwa wapi?"
"Ooh sikukwambia kumbe anataka kuoa yule ameenda mizimuni kutambika"
"Wee kumbe anataka kuoa sasa huyo mwanamke wake mbona sijawahi kumuona hapa?" Nilizidi kumuuliza
"Sio hivyo yani mila zetu mwanaume akifikisha miaka ishirini na tano anatakiwa aoe na mwanamke pia miaka ishirini anatakiwa aolewe na mila zetu hairuhusiwi kuzini wala kuwa na uhusiano na mume au mke hujitafutii bali tunaweka ngoma wasichana vigoli wanacheza na mwanaume anachagua halafu ndoa inapita"
Alinielezea Nuhri nikamuelewa.
"Kwaiyo Muthan pia ataweka ngoma kutafuta mke?" Nilimuuliza.
"Ndio tena leo anarudi naisi kesho ngoma inawekwa"
Alinambia nikamuelewa sasa nilibaki kwa hamu nione harusi zao inakuwaje.
Maandalizi yakaanza watu wakaweka ngoma zao uwanjani moja ikapigwa wakakusanyika wanakijiji nakupewa habari wale wasichana vigoli wanaotaka kuolewa wakaambiwa wajiandae.
Maandalizi yakafanyika Usiku Muthan akarudi nakuwekwa ndani akipokea baraka za wazazi wake.
Hatimaye kesho yake ikafika siku yakumtafuta mke wa mtoto wa Mfalme.

Bei ya ofa mwendelezo hadi mwisho lipa 1000 tu! Namba za malipo Voda 0763361677, tigo 0719618409 jina Lisa Ntanga ukilipa nitumie muamala wasap nikutumie.

Post a Comment

Previous Post Next Post