MREMBO MCHARUKO-9

 


MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

Wanakijiji wote walikusanyika kwenye uwanja mkubwa ambao ni maalumu kwaajili ya ngoma, kulikuwa na sehemu pembeni wamezungusha makuti hao vigoli wanaotaka kuolewa wanakaa humo halafu mmoja mmoja anatoka nakuja uwanjani kucheza hadi wote waishe halafu wanajipanga mstari anapita mtoto wa Mfalme nakumchagua mmoja aliempenda.
Basi mambo yakaanza uwanjani hapo ngoma zikaanzwa kupigwa huku watu wakijiweka tayari kumpokea Mfalme na familia yake ambapo alitoka nyumbani kwake nakuelekea kwenye ngoma sasa akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na mimi nikiwepo pia walinzi wengi walitulinda hadi tulipofika nakwenda kukaa sehemu iliyotengwa maalumu kwa Mfalme viti kikubwa vya ngozi viiliwekwa hapo.
Baada yakukaa wakatoa salamu zao kwa Mfalme nakumtakia maisha marefu, Mara akaja mwanaume mmoja mbele akiwa ameshika karatasi nakuanza kuongea.
"Jamani wanakijiji tumekusanyika hapa kwenye tukio kubwa linalomuhusu mtoto wa Mfalme Muthan anaetaka kuchagua mke leo hii, naamini wote tumefurahia ili jambo pia mabinti au vigoli wetu warembo wameshajiandaa vizuri kwaajili yakuonyesha uwezo wao wakucheza ngoma vigeregere jamani kinamama"
Alisema nakufanya watu walipukwe kwa shangwe kubwa, halafu akaendelea kusema.
"Kuna mabinti kumi waliojitokeza ngoja niwaite majina yao waje hapa mbele muwaone Shamima, Maua, Somoe, Halima, Mwahija, Sara, Shani, Moze, Karima, na Zawadi ni wasichana wanaojiamini sana sasa nawakaribisha wa kwanza ni Moze aje mbele"
Aliita majina yao wote wakatoka mbele kila mtu akawaona nilishtuka kumuona Shamima kumbe naye alikuwepo nikajisemea kimoyomoyo ngoja nione nani atashinda.
Basi ngoma ikapigwa akaanza Moze kucheza alijitaidi mwenyewe akacheza nusu saa nakutoka akaja mwengine pia hivyo hivyo hadi ilipofika zamu ya Shamima alikuwa anajikakamua huyo kama mfyatua matofari nilibaki namtizama nikitamani nikamtie hata makofi atoke pale mbele basi alipomaliza akaingia msichana wa mwisho Zawadi naye akacheza hapo alipotoka tu nikasema sikubali naingia kati maana ngoma ilinisisimua balaa nikaisi mwili wote unanisisimka, nilitoka mbio kule mbele nilipokaa hadi watu wakashangaa kuna nini walinzi wakataka kunikamata nikawastopisha wasiniguse hapo wazimu ushanipanda sasa, niliingia kati nikazungusha kiuno kama sina akili nzuri.
"Watu wanacheza kama wamebemendwa vile ngoja niwaonyeshe ngoma zinachezwaje"
Nilijisemea kimoyomoyo hapo watu wote kimya macho yapo kwangu nilizungusha kiuno nimesimama hadi nikachuchumaa ufundi wote nilimaliza hapo nikaona nikae staili ya chura sasa na zigo langu Snura akasome basi nilianza kucheza kichurachura hapo mara nitishinge tako moja moja burudani ya nguvu nikaitoa nilikata mauno watu hawakuamini wakaanza kushangiria namimi ndo mizuka ikazidi nilicheza uwiii hadi nikaja kunyanyuliwa juu juu.
"Lisaaa Lisaaaa Lisaaa oyooooo piga keleleeeee"
Basi nakwambia nilibeba juu juu huku wakizidi kushangiria, walinikera kunikata stimu yangu.
Mara ghafla namuona Muthan amekuja nakuwaambia wanishushe chini baada ya hapo akasogea kunikumbatia.
"Nakupenda Lisa! Jamani huyu ndio mkewangu"
Aliongea watu wakazidi kushangiria mara akaja Nuhri.
"Waoo wifi yangu"
Alinikumbatia nakunishika mikono hadi kwa Mfalme nikapewa baraka hapo hapo wakaja wamama wawili na kanga nikafunikwa kama mwali nakutolewa uwanjani nikapelekwa ndani kwenye chumba kimoja kwaajili ya maandalizi ya ndoa.
"Jamani mimi sipo tayari kuolewa nilicheza kujifurahisha sio kutaka kuchaguliwa"
Yani mambo yalipelekwa haraka hata sikuelewa kwanini imekuwa hivyo nilijuta kwenda kucheza ngoma imeniponza nikiolewa nitarudije nyumbani nilijikuta nashindwa kujizuia nikaanza kulia.
Akaitwa Mfalme nakuambiwa sitaki kuolewa ikabidi aje na mkewe wakanibembeleza nakunisii nikubali watanipeleka nyumbani kwetu hapo kidogo moyo wangu ukaridhika.
Ninakubali sasa Malkia Tamara alifurahi sana.
****
Hatimae nikaanza kusingwa mwali nakufundwa kuishi na mume, maandalizi yalipamba moto huko nje vyakula vikaanza kupikwa watu wakaalikwa hadi kutoka falme nyingine waje kuhudhuria sherehe.
Nilisingwa kiasili nikapendeza sana walinipaka hina wifi yangu Nuhri alinichora mwilini jamani nilikuwa kama malaika ikaletwa nguo ya kimalkia nikavishwa gauni kubwa zuri limenakishiwa na vito vyakumeremeta ni mamamkwe wangu huyo ndo alienipa iyo nguo Muthan nae alipendeza alivaa joho kubwa lakifalme.
Basi maandalizi yalikamilika na ndoa ikafungwa huku watu wote wakishiriki kwenye harusi yetu walikunywa na kula hadi wakasaza.
Kulikuwa na kijana ni mtoto wa Mfalme ambae babayake aliarikwa kwenye sherehe yetu wakahudhuria wote aliponiona alinipenda sana nakutamani hiyo ndoa angekuwa ananioa yeye, moyo wake uliuma sana bahati nzuri akamuona Shamima ambaye alikuwa mnyonge sana sababu tangu mwanzo alikuwa anajitapa yeye ndie ataolewa lakini imekuwa tofauti ilimuuma hata kwenye harusi watu wote walikuwa na furaha kasoro yeye alikuwa mnyonge sana.
Yule mtoto wa Mfalme aliitwa Millar akamfuata Shamima nakujenga ukaribu naye ambapo aliwatuma walinzi wake wamuitie Shamima nakuanza kuongea nae
"Kunakitu nataka unisaidie"
Alimwambia nakumfanya Shamima ashtuke.

Mwendelezo elfu moja. 0719618409 Lisa Ntanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post