IN'BOBO 01. -love story

    Age +18.

"Triiii triiii triiii "mlio mkali wa alarm nilio kuwa nimeutega kwenye simu yangu uliniamsha mida hii ya alfajiri,mida ambayo huwa nimejizoeza kuamka kwa ajili ya kujiandaa kwenda kwenye mihangaiko yangu.nilijinyanyua taratibu kwenye kijitanda changu cha tatu na nusu,mdogo mdogo nikatoka nje,kwenda kujisaidia haja ndogo.baada ya hapo nikarejea ndani.nikachukua kopo langu lenye mswaki pamoja na dawa,kisha nikachota maji kidogo kwenye kikombe...nikatoka tena nje kwa ajili ya kwenda kujiswafi kinywa.kilikuwa ni kitendo cha kama dakika kadhaa tu,nikawa nimemaliza.nikaingia ndani,huko niliweka kopo langu na kuvaa shati langu lililokuwa lime fubaa kutokana na kulifua mara kwa mara.nikaliendea torori langu,na kulitoa nje kwa ajili ya kuanza kuelekea huko nilikokuwa napatia ridhiki yangu ya kila siku.torori lilikuwa ndio ofisi yangu kwanyci lilinihudumia kwa mahitaji ya chakula na mambo mengine madogo madogo,ijapokuwa katika mavazi hali ilikuwa si nzuri.bhasi pasipo kupoteza muda nikaufunga mlango wa chumba changu, kisha nikaanza kusukuma torori langu dogo kuelekea sokoni.

kwa hatua za haraka haraka, niliichapulisha miguu yangu kuwahi sokoni,kufunga mzigo kwani kulikuwa na ongezo la wanunuzi pindi panapokucha kabisa hivyo watu tulio na vijimitaji vidogo vidogo ilitubidi kuwahi kwenda kuchukua mzigo kabla ya wale wenye nazo hawajafika.mimi nilikuwa mfanya biashara wa matunda,nikiwa natumia torori dogo la matairi ya pikipiki,kutembea huko na huko kuuza matunda yangu mtaani.hiyo ndio kazi iliokuwa inanipa mimi kula.sikuwahi idharau kazi yangu hata siku moja kwani iliyaendesha maisha yangu kwa asilimia kubwa.nilipofika sokoni nikafanya manunuzi ya mzigo wangu kisha nikauandaa vyema ili kunapopambazuka nianze kusambaza sehemu mbalimbali kama ilivyo kawaida yangu.mungu ni mwema kiza kikatoweka nuru ya jua ikaanza kuangaza katika uso wa dunia taratibu taratibu, lakini hatimae nuru ikawa imekuwa angavu zaidi.pilika pilika za kila mja aliyeletwa duniani zilienda vyema kwani mwanga ulikuwa ndio taa ya kusaidia viumbe mbalimbali kuendesha shughuli zao.

Nikiwa nimeshaanza rasmi kutembeza biashara yangu,niliamua kupitia katika mgahawa fulani kwa ajili ya kupata angalau kuliamsha tumbo langu kwa chochote,kamwe nisingeweza kufanya kazi huku njaa ikiwa inanisurubu.ulikuwa ni mgahawa niliokuwa napendelea sana kula kutokana na namna ya uandaaji wao wa chakula na mazingira yao ya kazi kiujumla.

"wee pili...mbona humuhudumii mmeo,akati amefika muda mrefu heee....huoni kama anaenda kazini mwenzio...mtalala njaa shauri yako!!!" mama wa mgahawa aliongea hivyo,tena aliongea na bintiye aitwae pili.mama huyu alikuwa amezoea kuniita mkwe kutokana na kwamba umri wangu niliokuwa nao,ulifaa kabisa kumuoa binti yake huyo pili.kwa hiyo akawa ananichukulia kama mimi ni mwanaume ambaye ninaweza kuwa na bintiye kimapenzi.ila haikuwa kweli bali ni utani.na mara nyingi nilikuwa namsikia binti pili,alivyokuwa akizozana na mama yake juu ya kuambiwa kuwa eti mimi ni mumewe.

"Mama ushaanza matani yako mi sipendi unajua.....wee haya tu"pili alijibu huku akiwa bize kuniandalia kifungua kinywa mezani kwangu.

"Kwa hiyo we hutaki mume mwanangu.......hivi huoni kama kijana wa watu alivyo mchapakazi..au we unataka masharobaro wenu hao wanaovaa suruali zipo matakoni kama wamejinyea.....mwanangu sifa ya mwanaume ni kazii,usafi baadae"mama mgahawa au kwa jina lililozoeleka,mama pili aligongomelea ule utani wake kwa bintiye pili ambaye kwa sasa alikuwa amekwisha maliza kunihudumia.

"Mi nshakwambia sitaki matani yako mama jamaniii aaargggh.mijanaume kwangu itanisaidia nini" pili alijibu.bhasi mi nikatabasamu tu kuona jinsi mama na bintiye wanavyozozana kimatani.kama dakika kumi na tano zilinifaa katika kula na kujipatia maji kidogo ya kunywa kisha nikalipia kile nilichokitumia,nikaondoka zangu kuingia dotido,wajanja wanaitaga hivyo ila kwa lugha rahisi ni mtaa kwa mtaa.nilianza kupiga business yangu bila wasiwasi wowote.sikuwa najali jua wala nini, nilichokijali ni kuona biashara yangu inasonga mbele.nilikuwa natembea umbali mrefu mno kutafuta wateja,lakini kwa juhudi pamoja na maombi mungu alikuwa akinisaidia hivyo hivyo kiubishi nilikuwa nauza.

"Kakaaa.....kakaaa wee muuza matunda!!!" Nilisikia sauti ikiniita.na haikuwahi kutokea kutokusikia sauti ya mteja,yani masikio yangu yalikuwa active kusikiliza ni nani atakaye niita kwa ajili ya kuhitaji matunda,kuliko ata kusikiliza sauti nyinginezo.nikageuka na kumuona mdada mmoja aliyekuwa na bambataa la haja,akinipungia mkono ishara ya kuniita.chapu nikamkimbizia biashara yangu.

"hapa ni mia mbili,hapa ni mia na hamsini,huku ni mia.....maembe yapo ya mia tatu na ya jero jero"nilimtolea maelezo mteja wangu huyu ambaye alihitaji kujua bei ya matunda yangu.nilikuwa nauza ndizi,embe na maparachichi.

"mmnh!! Mbona bei kali sana kaka'angu"yule dada aliongea kuonesha kuwa nilikuwa nauza matunda yangu kwa bei ghali sana,lakini nikamtuliza kwa maneno mazuri ya kibiashara biashara hadi akajikuta akiridhika kuniungisha baadhi ya matunda.

"Hahahahahaa.....ila wewe bhana una mbwembwe,......haya nifungie ndizi za buku jero,embe nipe za elfu mbili,parachichi nipe mawili tu,mi mwenyewe sio mlaji sana"yule mteja wangu alinipa maelezo hayo.

"Sawa, ndizi na embe unataka za bei ipi"niliuliza ili nipate kuelewa nimfungie matunda ya bei ipi.

"Ndizi niwekee za mia na hamsini,embe nipe za jero jero, ndo nzuri."yule mwanadada alihitimisha kutoa maelezo,maparachichi hakuyataja kwa sababu bei ilijulikana kuwa ni mia tano kwa parachichi moja,bhasi nami nikamfungashia kama vile alivyosema, baada ya hapo akanipa hela yangu....mimi huuuyo nikaendelea kusaga miguu yangu kusaka wateja.kwa kudra za mungu siku ilikwenda salama sambamba na biashara yangu kuuzika vizuri.mida ya jioni ndo nilikuwa najirudisha zangu nyumbani, huku mkononi nikiwa na kimfuko chenye wali ambao niliununua kwenye ule mgahawa niliokunywa chai asubuhi.huu ulikuwa ndio mlo wangu wa usiku.sikuwa napika,siku zote niliishi kwa kula vyakula vya mgahawani tu.baada ya kufika gheto kwangu.nikajimiminia maji na kwenda kuoga,niliporejea nikajipakaa mafuta kisha nikachukua moja ya sahani,nikamiminia ule wali wa kwenye kimfumo katika sahani.baada ya hapo nikajisogeza kitandani kwangu nikaketi,sikuwa na viti vya kukalia ata kimoja.hivyo nilikaa kitandani mkononi Nikiwa na ile sahani yangu ya wali.kabla ya kuanza kula nilifumba macho na kisha nikakiombea chakula pamoja na kumpa mungu shukrani kwa kunipatia mlo huo,nilipomaliza ndipo nikaanza kula.hayo ndo yalikuwa maisha yangu ya kila siku.yaani asubuhi na mchana nilikula mgahawani lakini jioni japo nilinunua chakula kwenye mgahawa lakini sikuwa nakula hapo hapo,bali nilikuwa naomba kuwekewa kwenye kimfuko laini na kwenda kulia chakula hicho nyumbani.hayo ni maisha ambayo nilikwisha yazoea na ndio maisha niliyoyaona ni nafuu kwangu baada ya kutoroka katika kituo cha watoto yatima.

Nakumbuka kipindi natoka katika kituo hicho cha watoto yatima nilikuwa na miaka kumi na nne,kama ujana ndo kwanza ulikuwa ukiniingia.nikajikuta niko mtaani baada ya kushindwa kuishi kule tulikokuwa tukilelewa.niliishi mtaani kwa karibu miaka minne,ulaji wangu ukiwa wa shida pamoja na ulalaji pia.lakini nilichokuwa namshukuru mungu ni kwamba licha ya mimi kupata dhoruba mbalimbali, za kulala mahala pachafu,kula vyakula vya kwenye madampo....kung'atwa na mbu katika kipindi cha mvua,haikuwahi kutokea mimi kuumwa.kila siku niliamka salama na kuendelea na maisha yangu.nilipo kuwa na miaka kumi na nane ndipo nilipopata wazo la kuanzisha biashara yangu hii ambayo ninayo hadi sasa.lakini kabla ya kuanza,nilijibana sana kimatumizi na kujiwekea akiba mpaka pale ilipofikia katika lengo nililokuwa nimejiwekea.nikanunua torori langu,kisha nikaanza kununua matunda na kutembeza mtaani.na mpaka sasa ni miezi sita tu imekatika tangu niianze biashara hii,ila ni mwaka umepita tangu nilipokula kiapo kuwa sintokuwa tena chokoraa,bali nitatafuta pesa kwa nguvu zangu zote na kwa akili zangu pia.kwa hiyo kwa sasa nina umri wa miaka kumi na tisa, naendelea kujipambania mwenyewe kwa kibiashara changu hiki kidogo.

siku fulani nikiwa nimerudi kutoka katika mihangaiko yangu ya siku zote nilikuta ujumbe katika kijisimu changu kibovu cha itel ambacho nilikuwa nimekifunga funga mipira ili kisisambaratike kwani hakukuwa na nati hata moja katika matundu ya kushikizia.baada ya kuusoma nilistuka sana nikakaa vizuri ili niurudie kuusoma pengine niliuelewa vibaya hapo mwanzo.ujumbe ulisomeka kama ulivyosomeka mwanzo,hakukuwa na mabadiliko yeyote.

"Nini.....laki saba?....wee hivi kweli au matani mbona sielewi elewi......"nilijiuliza,hapo ni baada ya kuurudia kuusoma ule ujumbe mara kadhaa.ni ujumbe uliokuwa umetoka katika mtandao niliokuwa nautumia.ujumbe ulinijulisha kuwa,pesa taslimu laki saba na sitini ilitumwa katika akaunti yangu,halafu katika ujumbe huo huo kwa chini...nilitajiwa namba iliyohusika kunifanyia muamala huo.sio siri nilishangaa nisiamini kama ghafla nimepata pesa nyingi kiasi hicho tena kwa kutumiwa na mtu nisiyemfahamu.kwangu ilikuwa ni zaidi ya maajabu.niliikumbatia simu yangu mbovu mbovu na muda mwingine niliipiga busu ile meseji ambayo sikuwa nimeifuta,bado niliendelea kuitizama tu.nilikuwa na furaha mno kwa usiku huu.na kama kungekuwa bado ni mapema bhasi ningekimbia kwenda kuzitoa hizi pesa,lakini kwa bahati mbaya usiku ulikuwa umeshakuwa mkubwa.maduka ya kutolea pesa yasingekuwa wazi hadi muda huo.nikalala nikiwa nimeikumbatia simu yangu,huku muda mwingine nikishtuka na kuangalia kama simu ilikuwepo.hiyo yote ni kihoro cha kutamani kukuche haraka ili nikatoe zile pesa nilizotumiwa.

Katikati ya usiku mnene simu yangu ilinistua baada ya kuanza kutoa mlio wa kuitia,kana kwamba kuna mtu alinipigia mida hii ya usiku.kwa shida na wenge la usingizi nikaangalia kwenye kioo cha simu na kuona kuwa ilikuwa ni namba ngeni ndiyo ilinipigia.....nikapokea kisha nikaanza kuzungumza na huyo aliyenipigia.yule mpigaji aliyenipigia simu,alijitambulisha kuwa aliitwa alice lemega,na sababu iliyofanya anipigie usiku huu ni baada ya kugundua kuwa alikosea kutuma pesa,akajikuta akituma kwangu,hivyo aliniomba kurejeshewa fedha zake kama sio zote bhasi ata nusu tu ya pesa hiyo.baada ya kusikia vile nilinyong'onyea sana,kwani zile pesa tayari nilikwishaanza kuzipangia bajeti zangu,ambazo zilikuwa zinaingojea asubuhi ifike tu ili nianze kuzitimiza....lakini ikatokea haya ya sasa daaa nililaumu sana.yani mtu unapata bonge la zari kumbe zari lenyewe linakuwa fake duu aisee sio poa kabisa. 

Kiukweli nilijifikiria mara mbili mbili juu ya kuzirejesha zile pesa lakini baadaye nikasema acha nirudishe tu pesa za watu kwani siku zote cha dhuruma hakina utamu kabisa,yani ata kama utakuwa unakitumia bhasi moyo wako lazima utakuwa unasononeka ndani kwa ndani na kujishuhudia wenyewe tu kuwa hicho ukitumiacho ni cha dhuruma.na mimi sikutaka iwe hivyo.siku zote nilijifunza kula kwa jasho langu na sio kula kwa kudhurumu au kumuibia mtu ambaye wewe mwenyewe hujui huyo mtu ana shida kiasi gani.nilichomwambia yule mdada aliyejitambulisha kuwa anaitwa alice ni kwamba ni sawa nimekubali kumrejeshea pesa yake.....na nikamuahidi kuzituma mara baada ya kumaliza kuongea nae.ni kweli baada ya kumaliza kuongea na alice,niliamua kufanya muamala wa kuzirejesha pesa kwa mwenye nazo,sikutaka kudhulumu jasho la mtu ata kidogo.niliamua kuzirudisha pesa zote pasipo kubakisha ata shing'mia...ila tu kwa sababu kwenye akaunti yangu sikuwa na pesa,ilibidi ile laki saba na sitini,ipungue.haikwenda ikiwa imetimia...kwa sababu kama mjuavyo huduma za kurusha pesa na kupokea pesa zina gharama zake.kwa hiyo kipindi narudisha pesa kwa alice,kuna kiasi fulani kilipungua katika ile laki saba na ushee.

"Samahani,kiasi kilichopungua katika hela hiyo..... ni gharama niliyoitumia kukurejeshea fedha zako dada"niliamua kuandika ujumbe huo kuelekea kwa alice ili kumjulisha upungufu wa fedha zake.

"Asante sana kaka.....we ni mtu mwema sana,mwingine asingekubali kunirejeshea pesa hizi....."alice aliongea.

"Usijali dada.....tumeumbiwa kuthaminiana.....nimelithamini jasho lako....ni haki yako kurejeshewa pesa yako"ni hivyo ndivyo nilivyomjibu ujumbe wa mwisho na baadae nikajilalia zangu,simu nikiwa nimeiweka chini,sikuikumbatia tena.sikuwa na haja ya kufanya hivyo tena dili limegeuka dirisha.

Naamu,siku zikasonga na hatimae ikakatika wiki moja nzima tangu tukio la kutumiwa pesa nyingi na kisha mimi kuzirejesha linitokee.asubuhi moja nikiwa bado nimelala, baada ya siku hii kuamka afya yangu ikiwa sio nzuri hivyo kutohitaji kwenda kibaruani kwangu.....nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni alice,yule yule mdada niliyemrejeshea fedha zake siku kadhaa nyuma.

"Habari za masiku kaka...."nilisikia alice akiniambia hivyo kupitia spika yangu ya simu.

"Salama waendeleaje na hali" nami nilimrejeshea salamu yake.

"Naendelea vyema.......aaamnhh samahani siku ile sikupata nafasi ya kukufahamu zaidi ya wewe kunifahamu mimi.......sijui naweza kulijua jina lako?"alice alinihoji.

"Yaaa......mi naitwa lucky"nilijitambulisha

"Ooooh.....lucky,unaishi wapi wewe?" alice aliniongeza swali.

"Niko dodoma...... ninaishi huku na mambo yangu yote nayafanyia huku huku pia"

"Asante kwa kukufahamu lucky....asubuhi njema"

Bhasi mazungumzo yetu yakaisha kihivyo kwa alice kunitakia asubuhi njema.kama ilivyo kawaida siku zikaendelea kusonga mbele kwa kasi huku sasa mawasiliano kati yangu na alice yakichanganya vilivyo.ndani ya muda mfupi tulishakuwa marafiki wakubwa.kila siku alice alikuwa akinipigia simu,kama sio kunitakia asubuhi njema,bhasi usiku alikuwa akinipigia na kisha tunazungumza kidogo kabla ya yeye kunitakia usiku mwema.huo ndo ukawa mwanzo wa urafiki wetu mimi na alice.

*****

"leo mume wako kapoaaa hadi namshangaa .....sijui anaumwaa!!??" Mama pili alimuuliza bintiye pili.walikuwa wakihojiana kuhusiana na muonekano wangu wa leo.sikuwa nimechangamka kama siku zingine ijapokuwa huwa sio mchangamfu kivile.

"asa si umuulize huyo hapo jamanii," pili aliongea kwa ukali...si unajua kuwa hapendagi aitwe mke wangu.bhasi ilikuwa hivyo.alionekana kuwa na hasira.

"Sikia pili ebu nenda kamuulize....anasumbuliwa na nini....." Mama pili aliongea. hapo pili akajikuta akijifikiria kwa muda kisha nikamuona akitembea kwa madaha mpaka akafika kwenye meza niliyokuwa nimeketi.

"Hivi we tunda man,ndo huwa unamwambia mama kuwa utakuja kunioa?" pili aliniuliza.aliniita kwa jina la tunda man kwa sababu ndilo jina nililokuwa likiitambulisha kazi yangu yaani muuza matunda, sema wao wakaliboresha na kuniita tunda man.au muda mwingine waliniita tunda boy....yote haya majina yalikuwa sawa tu,kwa sababu yaliitambulisha shughuli yangu ipasavyo.hakuna ambaye alilijua jina langu kamili.wengi waliyatumia hayo majina mawili.

"sio mimi......yeye hupenda kukutania hivyo.....lakini sikuwahi kumwambia chochote juu yako" nilimjibu.sikuwa mzungumzaji sana.mi nilikuwa ninajibu kulingana na swali tu,sikujua kuongeza maneno katika mazungumzo.nilipomjibu hivyo pili akamtizama mama yake kwa muda kisha akayarejesha macho yake kwangu.....

"Na ole wako nije kusikia unamwambia mama kitu chochote kinachonihusu....nakwambia utantambua......enhee mbona leo uko hivyo una tatizo gani" pili alinipa onyo kabla ya kurejea kwenye mada husika.

"mimi nipo kawaida tu mbona..." Niliongea

"kawaida? Unataka kusema si hatukujui"

"Simaanishi hivyo.....ila elewa tu kuwa mi niko kawaida,sema leo sijataka kuzungumza tu"nilimhakikishia pili kuwa nilikuwa sawa kabisa,sikuwa na shida yeyote.pili hakuwa na jingine,akajiondokea zake.bhasi nikala pale kisha nikaingia katika mishe zangu.siku hii nilirudi gheto nikiwa hoi,biashara haikuwa nzuri hivyo nilitembea sana.nilipokula chakula changu ambacho nilirudi nacho nikajilaza,lakini muda mfupi kabla ya kupatwa na usingizi simu yangu ikapata uhai,ikaanza kuita kwa makelele(nadhani mnazijua itel zilivyo na mikelele),bhasi kile ki itel changu kilikuwa kinaita.mpigaji akiwa ni Alice.unajua tangu tufahamiane mimi na alice,mpigaji amekuwa yeye,mimi sikuwa na muda wa kuweka salio kwenye simu istoshe maisha yangu yalikuwa ni unga unga mwana.vocha kwangu ilikuwa dili.zaidi ya kungoja kupigiwa tu.

" unajua nini alice,niache nilale mwenzio nimechoka sana...nimefanya kazi sana leo... Nahitaji kulala mapema "

"Ok,ila pole kwa kazi .....na vipi kwa nini usimwambie wifi akufanyie huduma ata ya masaji jamanii"

"mi bado mdogo sana sijafikia hatua ya kuwa na familia" niliongea ukweli wangu.

"Wee lucky bhana........udogo huo udogo gani ulionao hadi usiwe na familia hadi sasa"

"Udogo wa umri tu.....miaka kumi na tisa sio mingi....natakiwa kupambana Kwanza kutafuta maisha,kuliko kuwahi kutengeneza familia"

"Duuu ila we hatari.....unaonekana una plani kubwa sana aisee."

Nikazungumza na huyu rafiki angu kwa dakika kama tatu,kisha nikalala zangu.

*****

Maisha yakaendelea, siku zikazidi kukatika kwa kasi,mwishoe mwaka tuliokuwa nao ukaisha na tukaingia mwaka mwingine mpya kabisa.urafiki wangu na Alice bado ulikuwepo vile vile,tulishauriana vitu mbalimbali, japo mimi sikuwa nimeifahamu miaka halisi ya huyu Alice.kwa maelezo ambayo alikuwa ananipatia ni kwamba umri wangu ulipishana kidogo na umri wake hivyo ilikuwa kama tuko sawa.urafiki wetu ulishadumu kwa miezi minne tangu tufahamiane.mimi tayari nilikuwa nimeshatimiza miaka ishirini,nilikuwa ni kijana sasa aliyekuwa amekamilika.kwani miaka ishirini ni umri wa kijana kuishughulisha akili yake ipasavyo...na ndivyo nilivyokuwa nafanya.akili yangu na jumla ya viungo vyangu vyote vya fahamu vilikuwa bize kufikiria maisha tu.hakuna kingine.

nashukuru mungu,kidogo maisha kwangu yalianza kuwa nafuu,chumba changu nikakiboresha kidogo kwa kununua viti, huku chini nikitandika kapeti la kishkaji lakini ulalo wangu ukiwa ni ule ule nilichobadirisha ni godoro tu,lakini kitanda kilikuwa cha zamani.kuna siku fulani nikiwa nimetulia zangu chumbani kwangu,simu yangu ikapokea ujumbe......kiuchovu chovu nikainyanyua simu na kuitazama ile meseji ilikuwa inasemaje.sikuamini.....narudia sikuamini mara macho yangu yalipousoma ule ujumbe.akaunti yangu ilipokea shilingi laki tatu kutoka katika namba ya Alice.nilipoona tu kuwa namba iliyonitumia ni ya Alice,nikanyong'onyea,nikajua ni mchezo ambao utajirudia kama ambavyo ilinitokea mara ya kwanza.niliamua kumuandikia ujumbe Alice kuwa alikosea kutuma pesa tena,hivyo ningezirejesha ndani ya muda mfupi...lakini kabla ya kuutuma ujumbe huo,Alice akanipigia simu na kunijulisha kuwa alinitumia kiasi hicho cha fedha ili kinisaidie kwenye siku mbili tatu,wala hakukosea kama nilivyofikiri.

"Lakiii...niii niiii.....pesa nyingi alice" niliongea kwa kitetemeshi kuonesha dhahiri kwamba nilikuwa na mshituko sana nafsini mwangu.lakini alice kwa upole akanisihi kuwa niwe na amani, pesa alizonitumia nizitumie tu bila wasiwasi.bhasi nikakubali,lakini huku nikiwa na uoga wa kurudia kwa tukio kama ambalo liliwahi kunitokea .lakini cha kushangaza siku ikapita, ikafuata siku ya pili nayo ikapita vile vile....nikisubiri huenda alice angeniambia nimrejeshee pesa yake lakini haikuwa hivyo.kila aliponipigia alinisalimia tu kisha kunitakia siku njema.mpaka siku ya tatu ndipo nilipo amini kwamba ni kweli ile laki tatu nilikuwa nimepewa kabisa.sikuwa na shaka tena,nikaenda kuzitoa zile fedha na kuziingiza katika bajeti yangu.kikubwa nilichokifanya ni kuukuza mtaji wangu mdogo ambao nilikuwa nao,na fedha zingine nikanunua baadhi ya vyombo vya ndani.maisha yakaendelea.

*****

"Mmnhh!! Mkwe leo umependeza jamanii......mpaka siamini kama ni wewe" mama pili aliniambia mara baada ya mimi kuingia kwenye mgahawa wao.mama huyu alinizoea sana,kiasi cha watu kudhani labda ni kweli nilikuwa mkwe wake halisi,kumbe haikuwa hivyo.

"amna mama.....kawaida tu.....,nipatie chai ya rangi na chapati nne niwahi kazini chapu." niliongea Nikijumlisha na kutoa oda yangu ya kifungua kinywa kwa siku hii.

"Anhaaa sawa mwanangu, lakini leo siioni benzi yako.....umeiacha wapi" mama pili aliniulizia kuhusu torori langu ambalo sikuwa nalo kwa leo.

"Siku hizi kuna mtu ananisaidia.....mi niko pale pale tu sokoni.....nauzia pale kwa bei ya jumla."

"Heee umepanda chati siku hizi......." Mama pili alionesha mshangao wake.

"Ni neema za mungu tu....mama,mke wangu kaenda wapi mbona simuoni?!!" Nilitania kidogo.

"kaenda kuteka maji nadhani atarej.......heee nae kumbe ndo huuyo anaingia"mama pili aliongea, na kunifanya nigeuke kumtizama pili kule alikokuwa akitokea.niliachia tabasamu mara baada ya kukutanisha macho nae.

" we tunda man,leo wapiii.........au unasafiri nini"pili alinichokoza kwa maneno yake.nilicheka kidogo na kumuuliza.....

"Kwa nini"

"Sijazoea kukuona hivyo......kumbe ukivaa nguo nzuri nawe unakuwa mzuri eeh"

"Aaa wewe ushaanza porojo zako.....mi nishakuzoea" bhasi pili akacheka sana lakini huku akiwa amekazania kuniambia eti leo nilivyovaa vizuri bhasi nami nimekuwa mzuri.....kitu ambacho nilichukulia kama utani tu.nilipomaliza kula nikalipa kisha nikaondoka zangu.....huku nyuma nikiacha pili akiniambia kuwa ole wake asikie nina mke mwingine akati yeye yupo nitaisoma namba.

Nikarudi kazini kwangu,nikafanya kazi mpaka jioni,nikarudi zangu nyumbani mkononi nikiwa nimenunua samaki wangu watatu tayari kwenda kujiandalia chakula.mfumo wa kujipikia niliuanza mara baada ya kuanza kushinda sokoni,kwani nilikuwa nikirudi nikiwa sijachoka,tofauti na siku za nyuma ambazo nilikuwa nikirudi nikiwa hoi kutokana na kutembea kutwa nzima.nilipoingia Chumbani kwangu niliwasha jiko kabla ya kwenda kuoga,baada ya kurudi nikafanya kila namna mpaka nikamaliza kuandaa chakula.nikala kisha nikajitupa kitandani kwangu nikalala.

asubuhi niliamka kama kawaida nikajiandaa na kwenda job.lakini siku hii kidogo nilianza kujihisi tofauti.ujana tayari ulianza kunisumbua.....kwani nilijikuta nikianza kuyakodolea macho makalio ya akina dada mbalimbali waliokuwa wakiingia na kutoka ndani ya soko.ni kweli mwili wangu sasa ulikuwa na ashki nyingi sana za kuhitaji kuwa na msichana kimapenzi. tangu kuzaliwa sikuwahi kujihusisha nayo zaidi akili yangu ili focus katika kazi.lakini sasa nilihisi kuanza kushindwa. kwa kijana rijali kama mimi kuishi zaidi ya miaka kumi na kitu bila kuwa na mpenzi ilikuwa ngumu.moyo uliniambia kuwa nilitakiwa kufanya kitu juu ya jambo hilo.nikiwa naendelea na biashara yangu mara nikastuliwa na sauti nyororo kutoka mgongoni kwangu,kuna dada alikuwa akiniita alihitaji huduma.sikuamini baada ya kugeuka na kumtizama alikuwa ni mrembo wa haja,mwenye lips pana kidogo,mrefu na mwenye rangi ya chocolate.kiuno chembamba kilichozigawa sehemu za juu na chini za mwili wake.ni kweli alifaa kuitwa mrembo.mkononi mwake alikuwa amening'iniza mkoba wa kike uliokuwa na maua ua fulani upande mmoja.sketi yake iliyokuwa imefanana rangi na mkoba wake ilimfanya aonekane mrembo zaidi.

"nikuhudumie nini miss...." nilimuuliza baada ya kumgeukia.

"Naomba nipe ndizi chane mbili,maembe ya elfu nne na parachichi kumi"yule mrembo alinipa maelezo.sikuchelewa kumhudumia,nikamfungashia matunda kisha akanilipa na kutaka kuondoka.

"Miss......"nilijikuta nikimuita baada ya yule mdada kugeuka.kuna kitu nilitaka kumwambia ndio maana nilimuita.aliitika kisha akageuka na kunitizama.....

"Naweza kuipata namba yako.....??!!" ni kama nilimuuliza vile.yule dada akafikiri kitu kabla ya kujibu

"Namba yangu?ya nini labda"

"nitahitaji kuongea na wewe kwa muda fulani......kwa sasa mazingira hayaruhusu kutokana na mimi kuwa niko kazini"nilijieleza

"no haitawezekana......huwa sitoi namba kwa mtu nisiye mjua"

Nilipojaribu kumbembeleza mrembo huyu kuniachia namba,alikataa kabisa akaondoka zake.bhasi nikajisemea kuwa hiyo haikuwa ridhiki yangu.nikapotezea na kuendelea kufanya kazi.lakini kama bahati siku fulani tena nikiwa sokoni,yule mdada akaja kuniungisha kwa mara nyingine. nilihisi kama bahati kuonana nae kwa mara nyingine kwani siku niliposhindwa kuipata namba yake nilijua sintomuona tena.kama soko lilikuwa kubwa angeweza kununua ata sehemu nyingine Siku ambayo angekuja tena.siku hii alinisalimia kwa uchangamfu mkubwa,nikamhudumia kama ambavyo alitaka.mwishoe nikamkumbushia kuhusu kunigea namba,leo hakuruka kwani yeye mwenyewe aliniomba simu yangu na kuiandika namba yake kisha akajibipu,ili kuipata namba yangu.

"nikusevu nani......vile" aliniuliza.

"tunda......tunda man" nikamtajia jina lililokuwa likijulikana na wengi.

"heee tunda man?.......ndo jina lako au la utani"

"Ndo jina langu"

Hivyo ndivyo tulivyobadirishana namba na huyu mdada ambaye aliitwa marry au marrysiana,ila yeye alipenda sana nitumie jina la marry zaidi kuliko kulitumia la marrysiana.siku hiyo ikapita,ikaingia siku nyingine mpya kama kawaida nilikuwa golini kwangu nikizichanga changa.ilipofika jioni nikarudi gheto kwangu.nikafanya maandalizi ya msosi nikala kisha nikajilaza kitandani.baadae nikagundua kuwa sikuwa nimemtafuta marry tangu ile jana alivyonipa namba.nikachukua simu yangu na kumpigia.....mwanzo iliita bila kupokelewa,nikarudia mara ya pili hapo ikapokelewa...

"ulikuwa ushalala?" nilimuuliza kutokana na kuona kupiga kwangu simu kwa mara ya kwanza hakukuwa na majibu.mpaka niliporudia.

"No...nilikuwa bafuni mara moja.....nambie"kilichofuata hapo ni salamu za hapa na pale lakini hatimae nikafunguka lengo la mimi kumuomba namba ya simu yeye marry.nilimwambia kuwa alitokea kuziteka hisia zangu kwa kiasi kikubwa,tangu nilipomtia machoni.moyo wangu ulitamani sana kuwa nae.hivyo nilikuwa nahitaji kupokelewa katika moyo wake.nilihakikisha nammwagia sumu ya hatari kiasi kwamba kupona asingeweza

"Tunda nimekusikia lakini siwezi kukudanganya.......kwa sasa sina jibu sahihi la kukupa,naomba unipe muda nitakujibu" hiyo ndiyo kauli ambayo aliniambia baada ya kujieleza sana.sikutaka kuwa na haraka kwani nilijua kuwa wanawake wako na tabia fulani za kitoto ambazo huziendekeza sana hivyo sikuhitaji kumharakisha,pengine jibu ambalo ningepatiwa lingekuwa si jibu jema.nikakubali kusubiria tu.ndivyo ilivyokuwa.zikakatika siku mbili bila mimi kumtafuta marry,naye vile vile hakunitafuta.siku ya tatu usiku,nikapokea ujumbe kwenye IN'BOBO yangu uliokuwa ukitoka kwa marry.aliniuliza kuwa mbona nilimchunia sana,na sikumtafuta kwa siku kadhaa.

"Nilikuwa bize sana siku mbili hizi......nilikosa muda wa kukutafuta kabisa"Nilijitetea

"ata meseji jamani......ilishindikana?sio vizuri hivyo"

"Marry nielewe hivyo tu,ubize ulinikumba hakuna kingine"

"Haya bhana...... hivi unaishi sehemu gani hapa mjini"

"Niko four ways tu hapa karibu"four ways ni mtaa niliokuwa naishi mimi.

"Ok lini utakuwa free nije nipajue kwako....."marry aliniuliza,hapo moja kwa moja nikajua tayari maombi yangu yalikuwa yameshakubaliwa,kama ingekuwa sio hivyo,marry asingeomba kuja kupajua kwangu.nilichomjibu ni kuwa ningemjulisha siku ambayo ningekuwa na nafasi.kuanzia siku hii marry hakuniita tena tunda man,au tunda kama nilivyokuwa nimemtajia jina langu hapo mwanzo.... akaanza kuniita majina mengi ya kimapenzi kila siku.muda mwingi alikuwa akinitumia jumbe mbalimbali za kunidhihirishia kuwa ananipenda sana.nilizifurahia meseji zake,na kuna muda mwingine nilimjibu baadhi ya meseji zake,nae akafurahi sana.mapenzi yakashamiri kati yangu na marry.yaani ikawa kila muda meseji zinamiminika kwenye IN'BOBO yangu hadi kero.

" kesho sitoenda kazini,nimemaliza mzigo nadhani hadi siku mbili au tatu ndipo nitaendelea.kama una nafasi kesho tuonane"usiku mmoja nilimwambia hivyo marry,mara baada ya yeye kunipigia simu na kuniulizia kuhusu kuwa na nafasi.marry akaniahidi kuwa kesho yake angefika bila kukosa tena mapema tu.

****

Siku iliyofuata mida ya saa sita mchana tayari marry alikuwa gheto kwangu,akinipikia.baadae alipomaliza tulikula na kujilaza kwenye kitanda.tukaanza kupiga stori za hapa na pale kabla ya marry kunilalia kifuani kwangu....ilikuwa ndo mara yangu ya kwanza kulipata joto la kifua cha mwanamke. mwili wangu ulinisisimka sana,kiungo changu cha uzazi kikaanza kuniletea fujo ndani ya boksa niliyokuwa nimeivaa.mtafaruko kwenye suruali uliongezeka zaidi mara marry aliponiletea mdomo wake na kuanza kuunyonya mdomo wangu.nilikuwa mgeni sikujua ile ilikuwa ni nini hasa ambayo marry alikuwa akinifanyia,zaidi nilifuatisha vile alivyokuwa akifanya yeye.mchezo ukanoga,marry akaendelea kunichezea katika mwili wangu,matokeo yake nilijikuta Niko kifuani kwa marry huku mpini wangu ukiwa ndani ya kinu chake.nilikuwa natwanga kweli kweli. si unajua ndio leo nilikuwa nakizindua kifaa changu kwa hiyo nilikipigisha kazi kiuhakika.kumbe kule kujituma kwangu,ilikuwa furaha kwa marry kwani alijikuta akipanda vilele vingi,pasipo mimi kumsaidia.gemu ya siku hii ilikuwa tamu kinoma,hata marry aliniambia kuhusu hilo mara baada ya kumaliza mchezo wetu.

"Tunda....nanii hii yako iko na radha sana,nimeinjoi.ni tamu hadi kisogoni eti" ni moja ya kauli ambayo marry aliniambia.nikatabasamu na kumwambia kuwa hata yeye alikuwa mtamu sana.siku hii tulijikuta tukifanya mapenzi vya kutosha hadi mida ya saa kumi na mbili ndipo nilimsindikiza marry kurudi kwao.mwanzo wa kuujua utamu wa mapenzi ni hapo.nikajikuta nikitamani kuongeza msichana mwingine ili niwe nafaidi utamu mara kwa mara.nikapiga hesabu za haraka haraka nikaja kugundua kuwa pili alikuwa anafaa sana...istoshe mama yake alikuwa akinikubali sana.hivyo niliona ni vyema nikamuanza huyo.

Itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post