IN'BOBO 02. love story

    Age +18.

Ilipoishia..

"Tunda....nanii hii yako iko na radha sana,nimeinjoi.ni tamu hadi kisogoni eti" ni moja ya kauli ambayo marry aliniambia.nikatabasamu na kumwambia kuwa hata yeye alikuwa mtamu sana.siku hii tulijikuta tukifanya mapenzi vya kutosha hadi mida ya saa kumi na mbili ndipo nilimsindikiza marry kurudi kwao.mwanzo wa kuujua utamu wa mapenzi ni hapo.nikajikuta nikitamani kuongeza msichana mwingine ili niwe nafaidi utamu mara kwa mara.nikapiga hesabu za haraka haraka nikaja kugundua kuwa pili alikuwa anafaa sana...istoshe mama yake alikuwa akinikubali sana.hivyo niliona ni vyema nikamuanza huyo.

TWENDE NAYO.

Jioni hii sikutaka kurudi room kwangu,niliamua kunyooka moja kwa moja hadi katika mgahawa wa mama pili,lengo langu ni kwenda kuanza kumfuatilia pili na si kwa ajili ya kupata chakula kama nilivyokuwa nimezoea.

"Hee we tunda man,veepee mbona mida hii leo kunanii?!!"pili aliniuliza mara aliponiona.ni kweli siku ya leo niliwahi kwenda tofauti na siku zingine ambazo nilikuwa nikifika katika mgahawa huu kama saa mbili au saa tatu za usiku,lakini leo ni mapema mno nimefika hapa,ndo maana huyu pili alionesha mshangao juu ya hilo.

"kwani ajabu mimi kuja hapa asaivi?"Nami nilijibu swali la pili kwa mtindo wa kuhoji.

"sijakuzoea kukuona mida kama hii ndo maana nimeuliza......"

"siku hazifanani bhana,leo haiwezi kufanana na jana....."niliongea.

"mmnh!! Haya mwaya......nikuhudumie nini mume"nilishangaa pili akiniambia hivyo...tena kwa kuniita 'mume' ilihali siku zote yeye ndiye alikuwa kipaumbele kukataa asiitwe yeye ni mke wangu.

"sipendi mautani......hiyo mume imeanza lini...."nilimchokoza pili kwa swali langu hilo la kijinga.

"heeee kwa hiyo unanikana leo....kwani we si ndo huwa mnaitana mkwe na mama au...."

"kwa hiyo kama tunaitana hivyo,ndo we uwe mke wangu ki kweli kweli?"hapo pili alitabasamu tu akashindwa kujibu swali nililomuuliza,zaidi alijifanya kupotezea.

"eee....tuachane na hayo,niambie leo imekuaje mapema yote hii ushafika....njaa imekukomoa sana au"

"Amna.....mi leo sijafuata chakula wala njaa hainiumi,sema kuna kilichonileta......."hapo niliongea huku nikitizama huku na huko kuangalia uwepo wa watu,nikaja kugundua kuwa hakukuwako na watu wengine zaidi ya sisi wawili.

"Mmnh!! kilichokuleta ni nini.....kama hujaja kula?"pili alihoji,akiuliza dhumuni la mimi kuwepo hapo muda huu.

"sikia mama ako kaenda wapi kwanza......"

"kaenda kwa mama ake zaina,yule rafiki angu unayemkutaga muda fulani hapa"

"Anhaa oky,anaweza kurudi saa ngapi labda"

"aah bhana tunda una maswali mengi aisee....we siuseme shida yako tuuu,mambo ya kumuulizia mama,sijui kaenda wapi....mara nini na nini,unanichosha eti"pili alilalamika.

"haya unaona kama nauliza ujinga siyo poa.....tuachane na hayo,pili leo shida yangu ilikuwa ni wewe.....sijafuata chakula wala nini"nilipasua jipu.

"Shida yako ilikuwa ni Mimi.....kivipi"

"unajua pili,nimeanza kukufahamu siku nyingi sana,japo huwa nakuja na kuondoka kwa haraka lakini naamini nimejihakikishia kuwa we ni msichana mmoja mzuri sana unayefaa kuwa na mwanaume......nimegundua kitu ndani ya moyo wangu.nafsi yangu imekuwa ikikuhitaji sana,sema tu muda haukuwa rafiki kwangu kukuambia.mi leo nimeamua kukuambia ukweli wangu.....hata kama utanikasirikia whatever,sitojali....pili mi nakupenda nataka uwe mwanamke wangu....."niliongea, kisha nikameza funda la mate kusafisha koo langu ambalo lilikuwa na mikwaluzo ya kiaina.kitu nilichokiongea pili alionekana kutokukiamini kwani aliamua kukaa kabisa,pengine ili anisikilize vyema.huyu pili baada ya kukaa alitulia kwa muda mwingi bila kuzungumza kitu,lakini hatimae akanyanyua mdomo wake na kuongea kitu......

"Tunda....mbona kama unanishangaza leo......unajua sikufiri kama leo utaniambia hivi.niambie umefikiria nini hadi umechukua uamuzi wa kunitongoza...."

"pili,mimi ni mwanaume......istoshe sio mwanaume pekee bali ni mwanaume niliye rijali....hivi nitaachaje kuziweka hisia zangu wazi hasa kwa mwanamke mzuri kama wewe,nitawezaje kukaa kimya..sio siri nimeshindwa pili.mdomo wangu umeshindwa kukaa kimya kuendelea kuuficha ukweli juu ya mapenzi yangu kwako.....nielewe hivyo tu kuwa nakupenda na nakuhitaji uwe wangu,usifikirie kuhusu matani ambayo huwa nataniana na mama yako.leo niko siliazi,sijaja kukutania wala kukuletea vituko.ni kweli moyo wangu unakupendaaa"niligongomelea hoja yangu.

"hivi tunda man ni wewe unayezungumza au mwingine...... mbona leo unazungumza vitu vizito vizito.......(hapo kidogo pili akaachia kicheko cha kiaina)......usikute tunda leo umekunywa.....ebu tuone"hapo pili alijinyanyua na kuusogeza uso wake jirani kabisa na Mimi,nadhani alikuwa akijihakikishia juu ya kile alichokuwa amekibashiri.

"mbona sisikii harufu ya pombe......" aliniuliza huku uso wake ukiwa bado jirani na ulipo mdomo wangu.

"kwa hiyo ni kweli we unafikiri kuwa nimelewa siyo?.....mi huwa situmii kilevi bhana" niliongea huku nikiwa katika tabasamu.

"wewe huyo au nani,mbona unaonekana umekaa kilevi levi vile"pili alinitania.

"Ushasema muonekano..... na sio tabia yangu,muonekano huwa haubashiri tabia ya mtu,bali matendo yake haswaa ndio huwa yanasadifu(huashiria au hudhihirisha),tabia ya muhusika."

"Duuu ushanigeuza mwanafunzi sasa.....manake sio kwa kunifafanulia huko....."

"Sawa,vipi sasa kuhusu nilichokuambia......"nilirejea katika mada yangu,manake niliona pili alitaka kuipoteza.

"hivi tunda umemaanisha kweli.....jamaniii,mi nachukulia ni utani tu eti?"

"pili nishakwambia, leo sijaja kutaniana na wewe,nakuhitaji kabisaa sio masikhara"daaa sasa tukiwa bado tunaendelea kujibishana mimi na pili,mara mama ake pili akaingia,huyo ndiye alikatisha mazungumzo yetu.tukajifanya kupiga stori za kawaida tu pale.

"Heee mkwe huuuyo,leo naona nyota zimeendana hadi mmekaa pamoja.......maajabu"mama pili alitania wakati anaingia.

"Wee nawe mama ushaanza,kwani mi kukaa na tunda kuna tatizo gani"

"akhuu hakuna shida ila umenishangaza,manake kila siku ooh mi sitaki mautani yenu,sijui mimi simtaki tunda....haya sasa leo vipi mwenzetu.....tunda kanoga au,sema ueleweke kama tunda kawa mtamuu....." Mama pili alimtania bintiye.mi kipindi hicho kimya nimenyamaza.vile walivyokuwa wakijibishana ni kama walikuwa sio mtu na bintiye,kumbe ni kweli walikuwa ni binti na mama yake.ila kwa upande wangu mi nilichukulia ni kama kuzoeana kwao ndo kulipelekea wajibishane kwa mtindo wa kama marafiki.

"Akhaa niache na mambo yangu.....mi habari ya tunda hainihusu,kaja hapa kama mteja tuu,wee kama unafikiria vingine utajua wewe....."

Nikaona kama tayari inshu yangu ilikuwa imeingia mdudu.nikaamua kujibaraguza kwa kuagiza kikombe cha chai nikanywa kisha nikaaga na kuondoka.Nikiwa nimeshapiga hatua kama thelathini,nilishangaa pili akinikimbilia na kunisimamisha....

"kwa hiyo tunda ndo unaenda....."

"yaa ndo naenda,huoni kama mama karudi....tutaongea nini sasa....."

"Usiwe hivyo bhana si tunaendelea kuongea tu"

"hapana,sio vizuri.wacha niende tutaonana tena mungu akipenda"

"Ndo hutaki ata kusikia jibu lako jamaniii"

"nitakuja tena......usijali.ni lazima nitafuata jibu langu tu"

"yani weweee.....haya bhana,lakini mi nilitaka ungoje jibu lako kabisa."

"Tatizo muda,au fanya hivi nikuachie namba yangu utanitafuta muda wowote ukipenda......we simu si unayo?" Pili akatikisa kichwa ishara ya kukubali kuwa simu ni kweli alikuwa nayo.bhasi tukabadilishana namba kisha nikaondoka zangu hadi gheto.room kwangu sikuwa na ratiba nyingine zaidi ya kuanza kupika.nilipomaliza kupika nikala na kupanda kwenye kitanda changu kwa ajili ya kulala.wakati ndo usingizi unataka kunichukua,simu yangu ilianza kuita,kitendo kilichonifanya nistuke usingizini.niliamka huku nikiwa namtukania mtu huyo aliyenipigia,matusi ya nguoni kwani nilihisi ni kama usumbufu tu kuamshana mida ya usiku ambao watu mara zote huwa wamejipumzisha baada ya kutoka katika mihangaiko yao ya kutwa nzima.nilipojinyanyua vyema,nikaichukua simu na kupokea baada ya kuangalia mpigaji wa simu hiyo ni nani......kumbe ni marrysiana(marry).

"Bby mbona umekuwa mkimya ata kuniuliza kama nimefika salama jamani hutakiii"marry alianza kujibebisha.

"Mi nilijua utanianza wewe,nawe kumbe ulitegemea mimi nikuanze....."

"Yees Darling,nilitaka unianze wewe kipenzi changu"

"ok nisamehe bhasi malaika wangu,sintorudia.nitakuwa naku text mara kwa mara sawa Queen?"

"Sawa honey......unafanya nini asaivi..... "

"Nipo nimelala tu hapa,usingizi ndo kwanza ulikuwa umeanza kunichukua nawe ukapiga simu"

"Kumbe ulikuwa umelala?"

"of coz"

"Jamani........natamani ata ningekuwa nimelala kifuani kwako......"

"Usijali ipo siku utalala mpaka uchoke"

"Kweli my?"

"Amini hivyo.....one day utalala kwenye kifua changu usiku kucha na hutoamini....."

"Waaaoooohh,unanitamanisha bby.....alafu tunda naomba nikuulize kitu.uko na Mimi kwa muda au utanioa niwe mkeo?"

"marry mbona uko na haraka kuniuliza hivyo mamie,kuhusu hilo tutalizungumza zaidi siku nyingine.... usiwe na shaka na Mimi"

"Ni lazima niwe na shaka tunda,mi sipendi kuchezewa chezewa alafu niachwe.....naitaka ndoa ndo nitakuwa na amani"

"Usiwe na wasi......siku ikifika tutaongea.."

"Mmnh!!haya......ila tunda nimejikuta natamani unioe eti....,nahisi nikiwa mkeo nitafaidi sana penzi lako."

"Usijali ipo siku" unajua mi sikutaka kuzungumzia kuhusu mambo ya kuoana kwa sababu kiukweli sikuwa na wazo la kuoa kabisa,bali nilitaka tu kuwa na sehemu za kukidhi haja zangu za kimwili na sio kuoa.wakati naongea na simu ya marry,simu nyingine ilionekana kuingia.alikuwa ni Alice anapiga.bhasi nikamuomba marry akate simu ili niweze kuongea na mama,nilimdanganya hivyo marry ili kuondoa maswali mengi.nilikuwa namuheshimu sana Alice ndo maana niliona upo umuhimu wa mimi kupokea simu yake.

"vipi lucky ulikuwa ushalala?"Alice aliniuliza,nami nikamjibu ndiyo nilikuwa nimekwisha lala ila sema tu muda punde nilikuwa nikiongea na mmoja wa rafiki zangu kwa njia ya simu.

"aanhaa oky,ndo maana niliambiwa simu yako inatumika,kabla hujapokea"

"yaa ndo nilikuwa naongea na huyo rafiki yangu"

"nimekuelewa,lakini sorry sijui nitakuchelewesha kulala?,kuna kitu nataka kuzungumza na wewe"

"Amna nimezoea kulala muda wowote tu,waweza kuongea....."

"unajua lucky,bado nashindwa kuelewa we ni mtu wa aina gani"Alice alianza hivyo baada ya kumuondoa wasiwasi juu ya yeye kuhisi labda atanichelewesha kulala.

"kwa nini"

"Sio rahisi mtu kukurudishia zaidi ya laki saba.....ni ngumu sana kukuta mtu mwenye roho ya aina yako.lakini we uliweza....nambie uliwezaje kunirudishia zile pesa zote?"

"niliweza kufanya hivyo kwa Sababu,mimi si mtu wa tamaa na vitu ambavyo sijavitolea jasho....."

"aisee uko na roho ya ajabu sana,inawezekana kwenu ni maisha mazuri eeh si ndo hivo lucky?"

"ata sio hivyo......maisha yangu ni ya kumuomba mungu tu,na kwa bahati mbaya siko na familia....ninaishi peke yangu tu"

"Mmnh pole,wazazi wako wapo wapi kwani....."

"Sijui waliko.ila nakumbuka tangu nianze kupata akili,nilijikuta katika kituo cha watoto yatima tu,simfahamu baba wala mama......"

"Oohh pole lucky,ila usijali maisha yataendelea."

"ni kweli naamini hivyo kwamba maisha yataendelea....."

"Una elimu gani lucky"

"mimi, niliishia darasa la sita nikiwa katika kituo cha yatima,baadae nikatoroka nikaingia mtaani nikaanza maisha yangu.kwa hiyo sina elimu yeyote kwa lugha nyingine.kwani elimu yangu niliyonayo ni ndogo sana,inanisaidia kusoma na kuandika tu,labda na kufanya mahesabu yangu katika kibiashara changu kinachonifanya naishi"nilisema hivyo kwa sauti ya huzuni sana...nilipoongea hivyo nilihisi mabadiliko kwa Alice kwani alikuwa akitoa kwikwi kama ya mtu anayelia,nikajua lazima Alice alikuwa akilia.

"Alice......Alice....alice mbona kimya?"niliita,lakini alice hakuitika zaidi ya kumsikia akitoa sauti ya kwikwi tu pasipo kuongea.

"alice plz ongea na Mimi bhasi mbona upo kimya jamani"

"lucky, nafikiria ni kiasi gani unavyopitia changamoto za kimaisha bila wazazi......we bado mdogo sana,ulitakiwa uwe shule,lakini leo hii miaka ishirini uliyonayo uko mtaani kweli jamanii......"

"Ndo hivo alice,mi sina wazazi unadhani nitamdekea nanii,nakomaa tu mwenyewe...."

"lucky......sio siri nalia kwa sababu nakuonea sana huruma......kipindi mi naishi maisha ya raha,nina wazazi na ninasoma shule za gharama...kumbe mpo watu ambao mnavikosa vyote hivyo......"

"Ni kweli alice,lakini isikufanye ukanililia mimi masikini......ndiyo maisha yangu haya,ambayo mungu aliniandalia,siwezi kumlaumu pengine ipo sababu ya yeye kunichagulia uchaguzi huu...."

"Pole sana lucky.......ila nakuahidi kitu......ipo siku utaishi maisha mazuri sana.tena hutokuja kuamini....kikubwa tuombe uzima tu."

"Ni kweli ...sipingani na hilo kwani pasipo uzima hakuna lolote linaloweza kuendelea"

Usiku huu tulijikuta tukiongea kwa muda mrefu mno kiasi kwamba hata usingizi haukuweza kunipata.kwani mimi na alice tulifarijiana kwa vitu mbali mbali,tukapeana moyo na kutiana nguvu ya kuzidi kusonga mbele kimaisha pasipo kukata tamaa.vingi alivyoviongea alive nilivihifadhi kichwani.......lakini kuna neno moja tu ambalo huyu alice aliniambia nikashindwa kutambua nini maana yake,nakumbuka aliniambia...

"kwa wema wako lucky.....ipo siku nitakuwa na wewe"

Hapo kidogo aliniacha njia panda kwani sikujua hasa ni nini alimaanisha.nilipotaka kumhoji zaidi,aliniambia kuwa muda ulikuwa umekwenda sana hivyo nisijali ataniambia maana ya maneno hayo siku nyingine.baada ya hapo akanitakia usiku mwema kisha akakata simu yake.nami siiuwa na lingine tena nikaweka simu pembeni ya kitanda changu,kisha nikavuta shuka na kujifunika gubi gubi,nikalala zangu.

××××××

Asubuhi na mapema nilistuliwa na mlio wa mlango wangu ambao ulikuwa ukigongwa kwa nguvu.nikainuka nikaufuata mlango na kufungua,nilikutana na mwanadada aliyekuwa amesimama mbele ya mlango wangu.nikapiga miayo kisha nikafikicha macho yangu na kusema.....

"nikusaidie nini anti"

"samahani kwa kukuamsha....."

"Bila samahani...."

"Naomba msaada wako kaka angu,antenna yangu ya luninga imekaa vibaya inashindwa kuonesha vizuri......yani picha inacheza cheza.....kanisaidie kurekebisha tafadhali."

"duuu ooopfffhh,sawa naomba uningoje nipige mswaki mara moja....."

"sawa hakuna shida.....nitakusubiri"

"Poa.....karibu bhasi ndani.....sio vyema kukaa nje"

"No apa panatosha tu jamani.....usijali"

Bhasi yule mdada alipokataa kuingia ndani,nikaingia zangu ndani na kuchukua kopo langu lililokuwa na mswaki pamoja na dawa,nikatoka navyo nje,nikaenda kuviweka juu ya tofari moja la siment, nikarudi ndani nikachukua kikombe na kuchota maji kiasi kisha nikatoka navyo nje kama ambavyo nilifanya mwanzo.baada ya hapo nikachukua mswaki na kuutia dawa,mdogo mdogo nikaanza kuswaki huku yule mwanamke akinitizama namna ambavyo nilikuwa najishughulisha pale.kuna muda nilimuona akicheka na kutikisa kichwa,nikajua labda kuna kitu alikikumbuka ndio maana alijichekea mwenyewe.nilipomaliza kuswaki,nikapeleka vitu vyangu vyote ndani.kisha nikatoka tena na kuufunga mlango vyema,nikaongozana na yule dada hadi kwake.hakukuwa mbali sana na pale nilipokuwa nakaa,ni umbali wa nyumba kadhaa tu toka kwangu hadi kwake na huyu binti.

nilipofika nikapanda juu ya bati,kwa ajili ya kwenda kuiweka sawa ile antenna,kwani tayari nilikwisha jua tangu mapema kuwa kutakuwa na waya uliokaa vibaya na ndio maana picha ilikuwa inacheza cheza,kama ambavyo yule mwanada shosti alivyoniambia.ni kweli baada ya kupanda kule juu ya bati na kutizama vyema kwenye antenna nilikuta waya mmoja ukiwa umekatika,labda ni kutokana na ukali wa jua au nini ,sikutambua kilichokata ule waya.bhasi nikaunganisha.kule ndani ya chumba cha yule dada nikasikia sauti ikiniambia kuwa luninga ilianza kuonesha vizuri hivyo tatizo lilionekana kupona.nikashuka chini na kuomba maji ya kunawa,nikanawa pale kisha nikaaga na kutaka kuondoka....

"subiri chai bhasi kaka.......sijui unaitwa nani....."

"naitwa tunda....lakini kuhusu chai usijali siku nyingine nitakuja kunywa kwa leo hapana..... acha niwahi kwenye majukumu yangu"

"Sio vizuri lakini.....umenisaidia alafu ata chai usinywe jamaaaniii"

"Usijali,nadhani leo ndio mwanzo wa kufahamiana.siku nyingine tutakuwa tumeshazoeana.kwa hiyo suala la kunywa chai halitakuwa tatizo tena......"

"Mmnh!!!sawa bhana..... hapa mi ndio kwangu,naishi mimi peke angu......so karibu.muda wowote utaojisikia kunitembelea uko huru."

"anhaa sawa,nadhani nitakuwa nakuja kukutembelea...... usipate hofu"baada hapo nikaondoka zangu kurudi gheto kwani sikuwa na pahala pa kwenda....mzigo nilikuwa nimemaliza na waliokuwa wakiniletea waliniambia kuwa,mzigo mwingine utanifikia ndani ya siku tatu zilizokuwa zikifuata.hivyo nikawa sina kazi tu.lakini siku ya leo ni siku ya pili tangu niambiwe hivyo na wale wafanya biashara wenzangu,hivyo nilibakiwa na siku iliyokuwa ikifuata tu,then ningeendelea na kazi zangu kama kawaida.nilipoingia ndani na kucheki simu yangu,nilikuta meseji kama tatu kwenye IN'BOBO yangu.nikazifungua moja baada ya nyingine.

"We tunda......leo huji kunywa chai?" hiyo ilitoka kwa pili,yule dada wa mgahawani.

"Umeamkaje hubby"hii ilitoka kwa marrysiana au marry kwa kifupi.

"Lucky,vipi ushaamka?"ni text iliyotumwa kutoka kwa alice.nikaamua kuanza kumjibu alice...

"ndiyo nishaamka...."

"mbona umechelewa kujibu....."Alice aliniuliza hivyo baada ya kumjibu ujumbe wake wa kwanza.

"nilitoka,nilienda mahala fulani hivi......ndio nimerudi muda huu"

"Mmnh!!! Wewe usije ukawa umetoka kwenye michepuko"Alice alisema hivyo katika hali ya utani.

"hamna,sinaga tabia hizo aisee"

"Haya bhana nilitaka kukutakia asubuhi njema" bhasi baada ya Alice kunitumia ujumbe huo,nikamshukuru kwa kunitakia asubuhi njema,nami nikafanya kama alivyofanya yeye,yani nilimtakia asubuhi njema pia,huo ndo ukawa mwisho wa kuchati kati yangu na alice.nikahamia kwa hawa wawili waliokuwa wamebakia.

"Mi huko siji napika chai yangu nyumbani......"nilimjibu hivyo pili.

PILI;"nani anakupikia....?"

MIMI;"napika mwenyewe tu...."

PILI;"usije ukawa unapikiwa na videmu vyako,nikivikuta nitavibutua....onhooo"pili alinipiga mkwara

MIMI:"weee thubuutu,utavikutia wapi...."

PILI;"kwa hiyo tunda kumbe ni kweli una videmu vingine eeh....mbona umeniambia hivyoo"

MIMI:"ndio we si unaniringia.....wenzio wananitaka sasa kwa taarifa yako"nilimpandisha presha pili

PILI;"tunda mi sitaki ujinga wako huo......yani naomba uachane navyo hivyo videmu vyako.....laah sivyo mi siwezi kukubalia.... "

MIMI;"nimekwambia hivi,kuna wenzio wananitaka.....kwa hiyo ukiringa nakuacha natafuta mwingine...... "

PILI;"kumbe eeh sawa....kwa hiyo ukivyokuwa ukiniambia unanipenda ulikuwa unaniongopea......"

MIMI:"hahahahahaa sikiliza bhana pili........nakutania tu,mi sina ata demu mwenzio.labda wewe ndo utakuwa demu wangu wa kwanza.... "

PILI:"akhuuu usinidanganye huuukoo.....we si umesema una mademu sasa je?"

MIMI:"nimekwambia nakutania bhana mbona hunisikii au ndo umepata sababu ya kunikataa.."

PILI:"sio nakukataa tunda.....ila mi sipendagi kushea.nataka niwe peke angu"

Huyu pili nikaamua kumpigisha stopu kuchati nae,nikahamia kwa marrysiana.nae nikachati nae kwa muda kabla ya kuacha nae na kuhamia kwa pili kwa mara nyingine.nikachati nae pale hadi mtoto pili aliponambia kuwa amenikubalia ombi langu,lakini alipenda tufanye siri,ili mama yake asijue.nikamuahidi kufanya hivyo.

*******

Kama saa saba ilinikuta nikiwa namalizia kula.nilipomaliza nikajongea kwenye kitanda na kujipumzisha.mara usingizi ghafla ukanichukua kwa muda nisioujua hadi pale nilipokuja kuamshwa na mtu ambaye sikumjua mpaka nilipofumbua macho.alikuwa ni yule mdada wa asubuhi ambaye nilikwenda kumrekebishia antenna yake.

Itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post