IN'BOBO 03 lovestory

    Age +18.
Ilipoishia..

Kama saa saba ilinikuta nikiwa namalizia kula.nilipomaliza nikajongea kwenye kitanda na 
kujipumzisha.mara usingizi ghafla ukanichukua kwa muda nisioujua hadi pale nilipokuja kuamshwa na mtu ambaye sikumjua mpaka nilipofumbua macho.alikuwa ni yule mdada wa asubuhi ambaye nilikwenda kumrekebishia antenna yake.

ENDELEA.

Nilipomtazama vyema mkononi alikuwa amebeba kikapu ambacho ndani yake kulikuwako na hotpot,ambayo kivyovyote nilijua lazima ndani yake kutakuwamo chakula.mdada huyu alikuwa amesimama mbele yangu,huku akinitabasamulia tabasamu lake mwanana ambalo lilipelekea mashavu yake yabonyee kimtindo na kutengeneza vijishimo(dimpoz).

"Karibu....karibu uketi......."nilijifanya kumkaribisha mgeni wangu,ilihali mgeni mwenyewe tayari alikuwa ameshajikaribisha tangu muda mrefu tu.kabla ya kunijibu yule dada akacheka kidogo kuashiria kwamba tabasamu lake lilizaa furaha zaidi iliyomfanya acheke kabisa...

"Tunda una mambo jamaniii mnhhh!!"aliongea

"Nimefanyeje kwani....." nilihoji manake sikujua nini maana ya mwanadada huyu kuniambia eti 'nina mambo'.

"aa,hujafanya kitu,sema usingizi wako ni kituko aisee....yani nimeita weee huitiki,nikaamua kuingia coz mlango ulikuwa wazi......"

"duuu,nimechoka unajua we acha tu........nahisi usingizi muda wote yani,alafu mi nikilalaga aisee enhee,kuamka kwake sasa ndo huwa shughuli."

"mmnh polee,sio kwa usingizi huo tunda ipo siku utalia nakwambia...manake anaweza akaingia mwizi,akakuibia na akaondoka huku wewe ukiwa bado umelala na usijue chochote....."

"nitajirekebisha......."

"Any way......tuachane na hayo,aamnh humu kwenye kikapu nimekubebea chakula,nina imani hujatoka kwenda kula....so,ni muda wako sasa ule ushibe ukaoge sawa"huyu mwanada'shosti aliongea,lakini alinishangaza kwa namna vile alivyokuwa akiniongelea kwa mtindo fulani ambao haukuwa wa kawaida,ni kama alijifananisha na mpenzi wangu,manake sio rahisi mtu ambaye huna mazoea nae eti aseme 'ni muda wako sasa,ule ushibe'.

"nishakula mbona......yaaa niko vizuri"hapo niliongea huku mkono wangu ukiwa juu ya tumbo langu,nilikuwa nalipapasa na kumhakikishia yule mdada kuwa tumbo langu lilikuwa safi,yani halikuwa likihitaji chakula kwa muda huo.yule manzi hakutaka kunisikiliza,yeye akaweka kikapu chake juu ya kitanda changu, kisha akavuta ndoo moja ya maji akaikalia,akachukua hotpot na kuitoa ndani ya kikapu,akaifungua vyema na kunifanya nione chakula kilichokuwemo mule ndani ya hotpot.kulikuwako na wali ambao juu yake ulipendezeshwa kwa mchuzi wa rangi nyekundu uliotokana na kuungwa na nyanya zilizokuwa zimekwiva kisawasawa.hakika chakula kilivutia vilivyo...lakini tatizo likaja kwangu sikuwa nataka kukila kile chakula kabisa japo kilikuwa na muonekano pamoja na harufu nzuri.yule mwanadada ambaye katika kujibishana jibishana alikuja kunitajia jina lake ya kwamba alikuwa akifahamika kwa jina la sophia au soph,aliendelea kunilazimisha nile chakula chake alichoniletea....lakini kwangu ikawa ngumu,kwani nakumbuka wakati nipo katika kituo cha watoto yatima mlezi wetu mmoja aliwahi kutueleza kuwa hata siku moja tusijekupenda kupokea vitu ambavyo hatukuvijua ni wapi vilikotokea hata kama vitakuwa vinavutia kiasi gani..... hasahasa alichokuwa amelenga ni kuhusu vyakula ambavyo mara nyingi ni rahisi mtu kukuwekea kitu chochote cha kukudhuru.kwa hiyo tangu mlezi huyo alivyotuambia hivyo,maneno yake nikayaweka akili hadi hii Leo,yani ile tabia ya mimi kupokea vitu vya watu sikuwa nayo kabisa.

"Sophi mi nimeshiba bhana usijali......."

"Tunda usinifanyie hivo plz,chakula nimekuandalia wewe ebu kula usiwe na wasiwasi jamani"

"kwa sasa siko na njaa labda ukiweke nitakula baadae...."niliongea hivyo kumaliza mzozo.

"Kwa nini hutaki kula jamani tunda eeh,kula bhasi au tule wote kama vipi....."sophi bado aliendelea kuwa king'ang'anizi,nikaona isiwe shida kuendelea kukataa ilhali Sophi aliniambia kuwa atakula pamoja nami,tukaanza kula pale hadi tulipomaliza.

"Kumbe ulikuwa na njaa tu.....ila ulikuwa unajishaua bure"Sophia aliongea baada ya kuondoa vyombo na kuvirudisha katika kikapu.

"Nimekula bhasi tu kwa sababu tayari ulikuwa umeshakitenga,lah sivyo ata nisingekula."

"mmnh sawa bhana,asante kwa kula chakula changu,manake nilijua utakataa mazima....ningeumbuka mie jamani"

"Kwa kipi labda..."

"Si kwa huku kuleta chakula alafu kisiliwe"

"no....usijali bhana,ila siku nyingine ukiniletea chakula bila kunitaarifu nikikikataa usinilaumu kabisa.....yani hapa uliponikuta,tayari nilikuwa nimeshakula......."

"eti eeh....sawa nisamehe bhasi,alafu mbona kama uko mwenyewe mkeo yuko wapi....."baada ya sophi kuniuliza hivyo nilimtazama kwa umakini na nisijue namna ya kumjibu kwani uzito wa swali aliloniuliza haukupaswa kuulizwa na mtu kama yeye ambaye tumefahamia leo leo tu.

"kwa unavyonitazama unaweza ukafikiri kwamba mi nimeoa?"nilimdunga swali huyu sophi.

"Nop.....siwezi jua,but nimeuliza ili nipate jibu la uhakika kutoka kwako...."

"Owwky,aamnh mimi sijaoa....sitaki kuoa,na sijui kama nitakuja kuoa hivi karibuni,ni hadi baadae sana....ivo tu"

"Heee wewee na umri huu hutaki kuoa?kwa lipi sasa"

"kwa lipi?....si kwa maamuzi yangu tu ndivyo nilivyoamua"

"ata hupendezewi uwe peke ako jamani....chumba kama hiki ulitakiwa uwe na mwanamke wako anakusaidia saidia kupika mwenyewe adi raha yani......"

"ndo sijaamua sasa......Siku nikiamua nitaoa,mbona wanawake wako wengi sana wa kuoa......istoshe mi bado mtoto unajua.....sijafikia umri wa kuoa kabisa...."

"yani wewee mambo yako....lione vile sasa utoto ulionao ndo uko wapi"

"naujua mimi......"wakati tunandelea kuongea,stori zetu zilikatishwa na mlio wa simu yangu,ni kwamba ilikuwa ikiita.aliyepiga alikuwa ni pili,bhasi nikapokea...

"mmnh!! Nambie"

PILI:"poa.....mzima wangu?"

"Mi mzima,vipi wewe"

PILI:"safi tu....sema hujataka ata kuja kuniona we mwanaume jamani kwa nini lakini..... "

"kwani kuna ulazima wa kuonana kila siku"

PILI:"sasa je"

"Wee hamna kitu kama hicho...."

PILI:"ulazima upo tunda......we unadhani mi sikumisi?"

"sidhani kama unaweza ukammisi mtu ambaye mwanzo ulikuwa humtaki"

PILI:"aah bhana tunda achana na mambo ya zamani......na sio nilikuwa nakuchukia sema sikuwa napenda waniambie kuwa we ni mwanaume wangu...ni hivyo tu"

"ok tuachane na hayo.....nipe ratiba"

PILI:"jioni njoo kuna zawadi yako......"

"Zawadi gani hiyo"

PILI:"utakuja kuiona ukija,asaivi sikwambii......"

"Haya bhana....nikipata muda nitakuja......"

PILI:"jitahidi bhana mpenzi wangu uje sawa eeh,mi nimekumisi sana nataka kukuona...."

"sawa nitajitahidi...."

PILI:"plz bby wangu usikose kuja bhana"

"usijali"hivyo ndivyo nilivyomaliza kuongea na pili yule demu wangu mpya ambaye hata mchezo wa kikubwa sikuwa nimefanya nae.tukaendelea na mazungumzo mimi na sophi kabla ya muda kadhaa sophi kuaga kuondoka.

"tunda....baadae bhasi,mi kuna sehemu nawahi."sophia aliniaga kabla ya kuondoka.

××××××

jioni ya saa kumi na mbili kasoro nikaanza kujisogeza kunako mgahawa wa akina pili,kule majengo.nilichukuwa daladala kutoka four ways hadi majengo sokoni,nikashuka.nikaanza kukata mitaa kuelekea unakopatikanika mgahawa wao pili.dakika kadhaa nilikuwa nimekwisha fika,nilikuta mama yake pili akiosha vyombo katika kichanja kidogo cha kuoshea vyombo pale nje ya mgahawa, kana kwamba walikuwa wakijiandaa kufunga,kwani mgahawa wao haukuwa na huduma ya kuuza chakula hadi usiku,labda kuna baadhi ya siku walikuwa wakiuza hadi saa mbili hadi tatu,ndo mwisho...hapo wanafunga.lakini siku zingine walikuwa wakifunga saa kumi na mbili na nusu au saa moja ya usiku.

"Baba huuyooo........"mama pili alinichangamkia kama ambavyo alikuwa amezoea kunichangamkia siku zote..

"shikamoo mama......"nami niliusapoti uchangamfu wake kwa kumsalimia kwa furaha.

"Marhaba baba.....karibu,na tulivyokumisi jamani heee,nawe umetususa kama nini mwanangu....."mama pili aliongea huku akiupokea mkono wangu ambao nilikuwa nimeunyoosha kumsalimia huku nikiambatanisha na salamu ya 'shikamoo mama'.

"Hapana mama majukumu muda mwingine yanazidi,unakuta nakosa muda wa kuja ata kuwasalimia yani....."

"Anhaa sawa mwanangu.....mwenzio yuko huko ndani....sijui anafanyeje kwanza manake nimemwambia aje tusaidiane kuosha vyombo nashangaa amekaa tu....."mama pili aliongea akimaanisha kuwa pili ndiye alikuwa ndani,kwani huyu mama nilishawaambiaga tangu siku nyingi kwamba alikuwa akinichukulia kama mkwewe,kwa bintiye pili na ndio maana alinipa maelezo kuhusu yeye(pili).

"Anaonekana anakutegeaga kazi eeeh"niliongeza

"Mmnh baba utamuweza huyu.....ana vijisababu huyo hadi muda mwingine vinanikeraga,mara atakwambia anajihisi kiuno kinamuuma,mara kichwa yani bhasi tu ananichoshaga mno"bhasi mama pili alivyoongea hivyo mimi nikacheka kicheko kikubwa kiasi ambacho kwa hakika nilijua ni lazima kitafika kule ndani ambako pili alikuwako.ni kweli baada ya kupita sekunde kama tano,nikamuona pili akichungulia katika mlango wa mgahawa wao,tulipokutanisha macho akanikonyeza na kutabasamu,kisha akarudisha kichwa chake ndani....hiyo ilikuwa ni ishara ambayo iliashiria kuwa nilitakiwa kumfuata.nikapiga hatua za taratibu hadi mule ndani ya mgahawa.nilimkuta pili akiwa amesimama kana kwamba alikuwa amejitayarisha kunipokea.kitendo cha kusogea karibu yake,nikashtukia pili akiwa kifuani kwangu,ni kwamba alikuwa ameshanikumbatia.

"Pili acha bhana.....mama yuko nje je akiingia ghafla utajibu nini.....kwa hivi ulivyofanya"nilimtahadharisha pili kwa vile alivyokuwa amenikumbatia humu ndani ya mgahawa wao.nilihofia mama pili kutukuta tumekumbatiana mimi na bintiye,nadhani pangechimbika.

"No....tunda acha nikukumbatie tu,nilikumisi sana...."pili aliongea huku mikono yake akiwa bado ameikutanisha mgongoni kwangu vyema kabisa.yeye alionesha kutokuwa na wasiwasi kama ambavyo ilikuwa kwangu.

"Ebu acha hizo mada bhasi, tutaongea baadae,mama asije akaingia bure ikawa shida humu ndani....."bado niliendelea kumuonya pili.lakini awamu hii sikuongea kwa maneno tu,bali niliunganisha na kitendo cha kumtoa pili kifuani kwangu.

"Lakini tunda nini huuko.......unanikosesha raha bhana aaarggh,mi sijapenda"pili aling'aka huku akipigiza miguu yake chini,kama wafanyavyo watoto wakati wanapokuwaga wanawauwa wadudu ardhini.

"Pili kanakwamba huoni ata mazingira jamani,yani wee unataka nikuache ufanye unavyotaka wewe tu,aa aisee mi sio wa kihivyo....."nilionesha msimamo wangu mimi kama mwanaume.ujue wanaume hatujuagi tu,pale unapoanza mahusiano na msichana hakikisha humfichi kila kitu kinachokuhusu,especially tabia yako na mambo unayoyachukia pamoja na yale unayoyapenda,msichana akisha kuona msimamo wako daima hatoisumbua akili yako tena.kama boy hupendi demu wako avae nusu uchi au vijinguo vya kuchoresha mwili,usikae kimya...muite muelekeze kuwa 'bby nguo zako kweli ni nzuri lakini kwa upande wangu sivutiwi nazo...hasa hasa zikiwa mwilini mwako,kwani zinakuonyesha maungo yako,sasa love unataka kila mtu akione kile ninachojivunia kutoka kwako?plz acha kuvaa hizo nguo,sizipendi'.huo ni mfano tuu lakini unaweza kumkanya girfriend wako akaacha kufanya kitu ambacho hukipendi.sasa wewe jichanganye kwa kumficha one day utalia.Ndo maana pili alipoanza kuleta wenge nikamwambia kuwa tabia yake ya uking'ang'anizi sikuwa nimeipenda kabisa.hivyo sikutaka ijirudie.

Bhasi pili akajifanya kuchukia kimtindo, nikajisemea 'yani wewe unajishaua kama nini akati ushaingia anga zangu sa'subiri....',baada ya kujisemea hivyo nikapiga hatua kubwa kubwa kama tatu hivi,tayari nilikuwa nimeshatoka ndani ya ule mgahawa,na sasa nilikuwa namkaribia mama ake pili,pale alipokuwa akifanya fanya usafi wa vyombo vyake.

"mama nahisi muda umenitupa mkono....acha niwahi nyumbani mapema,nilipita mara moja kuja kuwasalimia tu...."nilimuaga mama pili,tena niliongea kwa sauti kubwa ili tu naye pili asikie.

"Wewee mbona haraka hivyo mwanangu jamani.....kunani?"

"nawahi mahala fulani mama,usijali lakini siku nyingine nitakuja tena..."

"Heee haya baba si tupo tu,mtatukutaga tu....."

Baada ya kumaliza kuagana na mama pili,nikaanza kupiga hatua kuondoka,mara IN'BOBO ya simu yangu ikapokea ujumbe,nikatoa simu na kuitazama,ni meseji ambayo ilitoka kwa pili ikiniuliza ni kwa nini naondoka.

"Mi siwezi kukaa na mtu aliyenuna bhana"hivyo ndivyo nilivyomjibu pili.

"Asa tunda kwani mi nimenuna jamani mbona hivyo lakini......sa'ndo nini unakuja haraka haraka alafu unaondoka,mi staki bhana fanya urudi eti....."

"huo ujinga wa kurudi sifanyi,kama we unataka nifuate..... huko siwezi kuja tena mimi"baada ya kuandika ujumbe huo na kuutuma,ikakatika dakika nzima bila kupokea ujumbe wowote kutoka kwa pili,nikajua amesusa lakini kumbe haikuwa hivyo,kwani muda punde ujumbe uliingia ukinitaka nisimame hapa nilipokuwa,na nisiendelee kusonga mbele,pili alikuwa amekubali kunifuata.kwa sababu sikuwa mbali sana na pale ulipo mgahawa wao,nikasimama mahala fulani ambako palikuwa si rahisi kwa mtu kuniona,kwani ni kama kiuchochoro fulani.na muda huu tayari kagiza kalishaingia na kalikuwa kakieleka kukomaa na kuwa giza kamili.mahala nilipokuwa nimesimama nilikuwa naweza kuona mtu yeyote aliyekuwa anakuja mbele yangu ila mtu huyo asingeweza kuniona kutokana na lile giza changa lililokuwa limeishaitawala duniani.

Kwa mbali nilimuona pili akija mbio mbio nadhani alitaka kuniwahi.alipofika jirani na nilipokuwa nikaamua kujitokeza ghafla kitendo kilichofanya pili apatwe na presha.

"ooh mungu wangu.......,tunda mambo gani haya tunastuana bhana,utanitoa roho mtoto wa mwenzio...." pili aliongea huku akinisogelea baada ya kunifahamu kuwa ni mimi.

"Muone kumbe nawe muoga....hahahahahaa....."

"Kwa nini nisiogope ilhali mi ni mtoto wa kike......."

"Mmnh sawa bhana yaishe manake duuuu sio kwa kustuka huko...."

"weee ungenitoa roho bure......"hapo pili aliongea akisogea zaidi kwangu na kutufanya tuwe kama tumegusana lakini si kugusana kiviile,bali ni kidogo tu.hakuna aliyemuongelesha mwenzie ndani ya sekunde kama ishirini hivi,kabla ya pili kuuvunja ukimya.....

"Tunda.....unajua nakupenda sana unalijua hilo?"pili ni kama aliongea katika hali ya kunihoji.

"Najua unanipenda,lakini sio sana kama unavyosema"

"Bhasi naomba ujue kuwa nakupenda,tena nakupenda sana......."

"Nitaaminije"

"Ipo siku utaamini tu kuwa ni kweli nakupenda.......nilianza kukupenda muda mrefu sana,sema sikuwa nataka ujue,najua ungenitesa sana"pili aliongea.

"Eti eeh,sa'mbona hukuniambia kama unanipenda?"

"Hee tundaaa mi ni msichana......unadhani ningewezaje kukuambia kuwa nakupenda.....ilinibidi niwe mpole tu,ningoje siku uje unitongoze,na kweli ukanitongoza....nikasema hapa ndo penyewe sikuachi kabisa...."

"Wacha weee"

"Kweli tunda......ila ukweli ndio huo nakupenda sana,alafu naomba ujue kuwa mi sipendi kushea penzi langu na mtu,so nihakikishie kama nitakuwa peke angu....."pili aliongea huku mikono yake miwili akiwa amenishika mashavuni.ni kama alikuwa akinilaghai kwa vijimipapaso vyake.

"Nikwambie kitu pili....."badala ya kukijibu kile alichokiuliza pili,nami nikataka kuingizia mada yangu.

"Nambie mpenzi wangu..."

"We ni mzuri sana,napenda vile ulivyo,napenda kila kitu chako,we ni mrembo..."hapo tayari nilikuwa nimeshalivuruga lile swali la pili ambalo aliniuliza eti nimuhakikishie kama atakuwa peke yake,kitu ambacho hakikuwa na ukweli endapo ningemjibu kwamba ni kweli atakuwa peke ake.kwani kabla yake tayari nilikuwa na marry.

"jamani kweli uyasemayo....."

"amini hivyo pili, japo nimeona wengi lakini jua umewazidi wengi....."

"aaaih jamani tunda kweli?"

"Ni kweli pili"nilipoongea hivyo pili alifurahi sana kwa kudhania kuwa kile nilichokuwa nimekiongea pengine ni kweli,kumbe ni uongo mtupu.pili akiwa amenishika mashavuni alikikutanisha kichwa chake na kichwa changu,tukawa kama tunagongana vichwa hivi,lakini haikuwa hivyo.baadae kidogo tukajikuta pua zetu zikiwa zimegusana mwishowe midomo yetu nayo ikakutana,tukaanza kunyonyana mate kidogo kidogo,matokeo yake tukazama katika denda zito.aisee ilikuwa ni balaa.pili alikuwa yuko vizuri sana katika kulana mate,kwani alikuwa akitoa miguno iliyoniweka katika wakati mgumu sana,kwenye maeneo yangu nyeti.chombo changu kilikuwa kimesimama mpaka sio poa.midomo yangu na ya pili ilikuwa imenasana vilivyo huku kila mmoja wetu akifurahia namna ambavyo alikuwa akipata mate ya mwenzie.nilikuwa nimemkamata pili kiunoni kwa mikono yangu,huku muda mwingine nikijaribu kuminya minya kiuno cha mtoto huyu mbichi.mambo sasa yalikuwa mambo,manake tulifikia hatua ya kuanza kutomasana hovyo hovyo kwani tayari ashki za miili yetu zilikuwa juu sana hivyo tulitaka kuzishusha kwa kutaka kufanya mambo ambayo yalitakiwa kufanywa chumbani.lakini mimi kama mwanaume niliye na uwezo wa kuiendesha akili yangu vyema,niliamua kusitisha kuendeleza kile ambacho tulitaka kuelekea kukifanya.

"pili hapa sio mahala pake,tufanye siku nyingine......"

"Bhana tunda nini huuko mi nataka.....naomba unipe hapa hapa,siwezi kulala leo kama utaniacha hivi hivi...."

"hapana kufanya hivyo sintoweza.......tutafute siku ili kukakatane kiu zetu,sio vyema kufanya vitu hivi njiani...."niliendelea kumsihi pili kuacha kile alichotaka tuendelee kukifanya.....lakini yeye alionekana kushindwa kunielewa,nadhani zile hamu zake zilikuwa juu zaidi kiasi cha kushindwa kuzi control.kwa kutumia ushawishi wangu wa kiume nikafanya kila namna hadi pili akakubali kuacha.bhasi hakukuwa nakingine cha ziada tukaagana pale mi nikasepa zangu.

*****

asubuhi kukakucha vyema,mapema sana tayari nilikuwa sokoni,katika biashara yangu.kwani mzigo uliingia sokoni usiku wa leo hivyo nilitakiwa kuupokea.ni kweli niliupokea vyema na kuuweka golini kwangu kama ilivyokuwa siku zote ambazo nilikuwa nikifanya.baada ya hapo nikaendelea na biashara yangu kama kawaida.majira ya jioni kabisa kama saa kumi hivi,nikiwa bize na upangaji wa biashara yangu ghafla niliguswa begani na mtu ambaye sikumjua....kuja kugeuka mtumee nilipigwa na bumbuwazi la aina yake kwani sikuamini kwa kile nilichokuwa nakiona......

itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post