SIRI ZA CHUMBANI 12



ILIPOISHIA

"Kwanini unanizuia nipo hapa bure? Wazazi wangu wanatoa malipo ni maamuzi yangu kubaki au kuondoka kwanini unanizuia?"

Mkuu yule hakunijibu lolote badala yake alinivuta mkono wangu kwa nguvu kunipeleka ofisini huku aliamuru mizigo yangu irudishwe hosteli...
***********************

Nilivutwa harakaharaka hadi ofisini nilivyofikishwa alinisukuma nakuanguka chini huku aliniambia..

"Nakupa sekunde 30 kuanzia muda huu unipe jibu lako la kuwa mahala hapa"

"Nilishakwambia nahitaji kuondoka nyumbani kwetu"

Nilishtuka bao la usoni hali iliyosababisha msichana Keti aliyekuwa mlangoni kuiita 

"Baba"

Macho yangu yalipigwa na butwaa nilipomuona na kugundua Keti alikuwa mtoto wa mkuu huyo, machozi yalinitoka kuona mkuu alichonifanyia kinaweza kumpata binti yake wakati wowote kwasababu alikuwa wa kike, nilimkimbilia Msichana Keti nakumkumbatia nililia sana, alinibembeleza vya kutosha huku alikuwa akigombana na baba yake...

"Sikuja kukushtakia umpige hana makosa yoyote"

Nilijua kabisa Keti hakujua kilichoendelea kati yangu na baba yake. Alinitoa mahali pale ofisini na kunipeleka kwenye hosteli ya chumba nilicholala ndipo alinikabidhi kwa rafiki yangu kipenzi Moni. Huku Moni alijua bado nilikuwa na kilio kwa kitendo nilichofanyiwa cha kuchekwa na wanaume hakujua nini kiliendelea kwenye maisha yangu na Mimi nilihofia kumwambia kwa kumuogopa mkuu wa chuo hiki.

Basi nilipitiwa na usingizi nilipokuja kushtuka ilikuwa alfajiri tayari niliamka na kuketi kitandani kwangu huku bado hali yangu haikuwa sawa kifikra niliwaza sana madhumuni ya kuendelea kukaa hapo yalikuwa kitu gani kwasababu tayari elimu yangu iliwekwa doa.

Kulipambazuka asubuhi kabisa wanafunzi walipoenda kuoga mimi nilikuja kuitwa na walinzi niliambiwa mkuu ndiye alinihitaji niligoma kwenda ila ilipofika mida ya darasani kwakuwa ilikuwa kipindi chake alitumia nafasi ya kujiosha maovu yake mbele ya wanafunzi akidai hakupendezwa na kitendo nilichofanyiwa na wanafunzi wenzangu. Baadae alipomaliza kufundisha aliniomba nimfate ofisini.

Kama kawaida yake nilipoenda bado alinisisitizia kuwa karibu naye lakini nilikataa na kuondoka zangu. Ilipofika siku ya michezo hapo chuoni nakumbuka nilikuwa timu ya Mpira wa kikapu wa wasichana nilipokuwa nacheza niliomba ruksa ya kupata maji ya kunywa na mojakwamoja nilienda kwa rafiki yangu Moni kwasababu yeye ndiye nilimuachia chupa ya maji yangu.

Alinikabidhi, niliyanywa ila kizunguzungu nilichokihisi hakikuwa cha kawaida nilianguka na kupoteza fahamu kilichojiri sikutambua.

NANI ALIMUWEKEA DAWA UNAFIKIRI...FERIA BADO ANAENDELEA KUTUSIMULIA. Usikose sehemu ya 13 

Post a Comment

Previous Post Next Post