SIRI ZA HOSTELI 11



ILIPOISHIA

"Mnacheka nini hii ni nini mnafanya ndio tabia mbaya mlizotoka nazo huko nyumbani kwenu sio vizuri kabisa haipendezi mlichokifanya lazima nikashtaki kwa mkuu wa chuo leo"

Ghafla kimya kilitawala eneo lile ila kilio changu kilikuwa zaidi ya vicheko vile..nililia sana.
********************

Keti alinichukua na kunitoa mahali pale alinipeleka kwenye hosteli ya vyumba vyao, muda wote nilikuwa nalia tu. Aliniambia Mambo mengi sana kuhusu chuo hiki, watu wa hapa pia nisiwasikilize, Kisha aliondoka kuelekea kwa mkuu wa chuo.

Nilikaa sana hadi nilipitiwa na usingizi rafiki yangu Moni alinifata na kuniamsha, aliniambia kuwa 

"Amka Feria walioanza kukucheka wamepewa adhabu na mkuu wa chuo twende ukaone"

Nilikuwa na huruma iliyopitiliza niliponyanyuka na kuona adhabu ambayo walipewa wanaume wote na kuna wengine ambao hata hawakuhusika iliniuma sana nilishangaa miguu yangu iliongoza mojakwamoja ofisini kwa mkuu.

Nilipofika niligonga kwa unyenyekevu mkubwa na kukaribishwa, aliniomba niketi na kumueleza shida yangu. Nilimwambia awapunguzie adhabu ambayo aliwapa ni kubwa sana sio wote walionicheka, niliongea sana lakini cha ajabu mkuu alibaki akinicheka tu, maswali yaliongozana kwenye akili yangu kwanini mkuu alikuwa akinicheka? 

Ndipo niliposikia kauli ambayo sikuitegemea huku macho yangu yalikuwa shahidi, mkuu alinishika mikono yangu miwili huku alinipapasapapasa kwa ishara ya kunitamani huku macho yake yalinitazama sana kwa tamaa. Kauli yake naikumbuka aliniambia...

"Usiogope binti mrembo kuwa na amani hiki chuo ni mali yangu cha kufanya nikushiriki na mimi kimapenzi ili uishi kwa amani chuoni hapa lahasivyo! Utaendelea kunyanyasika kila siku"

Nilimjibu kwa mshangao

"Mkuu Ina maana wewe unajua kinachoendelea hapa chuoni, vyote ninavyofanyiwa?"

Mkuu alicheka zaidi ya sana tena safari hii hadi machozi yalimtoka machoni mwake, kwa ujasiri wangu nilinyanyuka na kusimama kumwambia...

"Sijaja kwaajili ya mapenzi nimekuja kusoma nimalize elimu yangu iliyonileta naomba niwaachie chuo chenu naondoka kwa amani kabisa yaishie humu ofisini"

Nilimaliza kauli hiyo na kutoka huku nikiwa nakimbia hadi hosteli nilibeba mizigo yangu nakuchukua vitu vyangu vyote sikutaka kuongea na mtu yeyote zaidi ya kulalamika na moyo yangu. 

Rafiki yangu Moni aliposikia nahitaji kuondoka chuoni hapo alinifata na kunizuia lakini hakufua dafu nilianza kuburuza mizigo yangu hadi getini.

Nilipofika getini nilishangaa walinzi walinizuia kutoka kwa amri ya mkuu wa chuo, nililalamika sana na kuwaomba kutoka lakini walikataa nilichukua simu yangu ya mkononi na kuhitaji kuongea na baba kinachoendelea chuoni hapo lakini nilipokonywa na mkuu kwa macho yangu mawili. Nilimuuliza..

"Kwanini unanizuia nipo hapa bure? Wazazi wangu wanatoa malipo ni maamuzi yangu kubaki au kuondoka kwanini unanizuia?"

Mkuu yule hakunijibu lolote badala yake alinivuta mkono wangu kwa nguvu kunipeleka ofisini huku aliamuru mizigo yangu irudishwe hosteli...

FERIA BADO ANAENDELEA KUTUSIMULIA, KUMBE ZAMANI NETWORK ILIKUWEPO PIA, ITAKUAJE? Usikose sehemu ya 12. 

Post a Comment

Previous Post Next Post