SIRI ZA HOSTELI 10


ILIPOISHIA

"Naomba unipe historia yako iliyowahi kukutokea hadi umefikia hapo ulipo, Mimi ni Askari mpelelezi niliyetumwa na serikali huru ya Tanzania kufatilia kesi yako baada ya mauaji yako yaliyotokea miaka 3 iliyopita wazazi wako bw na bi Romi walifatilia Sana kesi yako na kukata tamaa ya kukupata tena ila Kaka yako Khelumi hakuwahi kukata tamaa kabisa hadi mimi kuletwa hapa na sababu ya mimi kukuona na kukusikia ni mkufu huu uliopo shingoni kwangu nilipewa kabla ya kuanza kazi"

Turudishe matukio nyuma ilikuaje binti Feria kutoka kwenye hali ya ubinadamu na kuwa mzuka ambao haushikiki wala kuonekana... 
********************

KUMBUKUMBU ZA NYUMA..........

Nilifika chuo baada ya kumaliza masomo yangu ya kidato cha sita nchini uganda wazazi wangu walinihitaji nirudi nyumbani Tanzania kuendeleza masomo yangu. Nilipotuma maombi ya kujiunga ilikuwa furaha yangu kuu kusikia nami nilikuwa mmojawapo niliyechaguliwa chuo hiki, nakumbuka mara moja nilipofika chuo hiki nilikutana na mzee wa makamo alinisimamisha nakunihoji..

"Wewe ni mgeni kwenye mkoa huu?"

"Ndio bibi, shikamoo"

"Sihitaji shikamoo yako hadi nikuombe mbona haukunisalimia nilipoanza tu kukuuliza"

Bibi yule aliongea maneno mengi kama laana sikuwahi kumuona wala kumjua ndio ilikuwa mara ya kwanza naonana naye, niliumia sana japo sikumjibu chochote.

Nakumbuka mida ya jioni nilifika chuoni nikiwa nimechoka sana, sikufikia ofisini kama ilivyokawaida ya kutoa ripoti kwa mara ya kwanza ukifika kwenye miji ya watu. Nilisindikizwa na wafanyakazi wa hapa kupelekwa mojakwamoja Hosteli hizo nakuwekwa chumba kimoja na aliyekuwa rafiki yangu alitambulika kama Moni, nilitokea kumpenda binti yule hata yeye ndiye aliyekuwa kioo kwangu kunionyesha mazingira ya hapa chuoni.

Mchana wa siku iliyofata wenzangu walipokuwa darasani wanasoma mimi nilienda ofisini kwa Mkuu kutoa ripoti yangu na kupewa namba yangu ya usajiri.

Kwa unyenyekevu wa hali ya juu nilikutana na Mkuu wa chuo hiki aliyetambulika kama Bw.Lume alinipokea na kunihoji maswali mengi huku alichunguza sana familia yangu iliyokuwa mashuhuri kwenye jiji hili. Nilivyomaliza kuandikisha nilipelekwa darasani nikiwa rasmi mwanafunzi wa chuo hiki.

Nilianza masomo yangu vizuri hakika niliyafurahia mazingira lakini siku zilivyozidi kwenda ndipo marafiki walivyozidi kuongezeka kwa upande wangu ila kamwe sikumsahau rafiki yangu Moni, vijana wengi walianza kuingia katika maisha yangu wakidai kunihitaji kimahusiano sikuwahi kumkubali hata mmoja. Kutokana na hali hiyo chuki zilianza baina ya marafiki wakidai Feria nilikuwa naringa sana kwasababu nilitoka familia tajiri haikuwa rahisi nitembee na kijana yeyote chuoni hapo jambo ambalo halikuwa kweli.

Visa vilianza chuoni hapa nilikuwa nikitoka kidogo nje ya hosteli basi lazima nikute kwenye begi langu kitu kimepungua, madaftari yangu yalichanwa kila nilipoyaweka hata nilipoweka nguo nilikuwa sizikuti kama nilivyoweka, na sitaisahau siku niliyodhalilishwa mbele ya wanaume nilipokuwa napita huku nilivaa gauni langu refu jeupe kumbe lilichanwa eneo la makalio mimi sikujua kwasababu bweni la wanaume na la kwetu lilijitenga kipindi cha nyuma. 

Nilichekwa sana nilipokuwa natembea sikuelewa nini walichekea kwa mbali nilimuona msichana mgeni kwenye macho yangu nilikuja kumjua baadae alitambulika kama Keti alinikimbilia huku mkononi alishika taulo na kunistiri, alikuwa mwema sana aliniokoa ila aibu yangu ilitembea chuo chote niliinua macho yangu kumtazama kila mmoja aliyekuwa akinicheka huku msichana yule aliongea kwa hasira sana nakumbuka maneno yake alisema....

"Mnacheka nini hii ni nini mnafanya ndio tabia mbaya mlizotoka nazo huko nyumbani kwenu sio vizuri kabisa haipendezi mlichokifanya lazima nikashtaki kwa mkuu wa chuo leo"

Ghafla kimya kilitawala eneo lile ila kilio changu kilikuwa zaidi ya vicheko vile..nililia sana.

KUMBE KETI ROHO YA WEMA ALIKUWA NAYO TANGU MWANZO FERIA BADO ANAENDELEA KUTUSIMULIA. Usikose sehemu ya 11. 

Post a Comment

Previous Post Next Post