SIRI ZA HOSTELI 09


Publish: 23/06/2020

ILIPOISHIA

Keti ilimbidi haulize kwa mshangao mkubwa sana, lakini kila mtu alijibu "hapana"..

Zaki maswali yalianza kumjia kwa mfululizo kichwani kwake, Nani analia? Kwanini nisikie sauti yake peke yangu? Ina maana richa ya kuwaona hadi sauti zao na uwezo wa kuzisikia?
*****************

Zaki alianza kusogea taratibu hakitoka zake nje

"Zaki tafadhali usiende nje" sauti ya msichana Keti ilimsimamisha..

Huku kama kawaida Bedo hakuacha kumzuia Keti hasimfate 

"Huwezi kukaa kutulia hadi na wewe hutoke huko nje, hakuna kutoka nielewe"

"Bedo unaongea kuhusu nini unaelewa hali anayoisikia Zaki ni ya namna gani?"

"Hata kama hiyo sio njia ya kusuruhisha kiurahisi namna hiyo wewe tulia kuliko kwenda wote wawili mkapotee"

Maneno ya Bedo yalimtuliza Keti nakumuacha pekee Zaki aliyekuwa tayari katoka zake nje.

NJE...

Zaki aliendelea kufatilia sauti ile iliyokuwa inaendelea kulia kwa huzuni kubwa, hadi alipoikaribia na kugundua ni msichana yuleyule aliyemuona ubaoni na hata ofisini kwa Profesa.

"Kwanini unalia?" Zaki alianza kumuuliza

"Unauwezo wa kunisikia?" Binti yule alimjibu kwa mshangao..

"Sio kukusikia tu nakuona pia"

"Unaniona kweli?"

"Ndio sina uwezo tu wa kukushika"

"Wewe ni nani?"

"Binadamu kama ulivyokuwa wewe mwanzo"

"Kwanini unaniona na kunisikia?"

"Kwasababu nimekuja kwaajili yako"

"Unamaanisha nini?"

"Hahahahaa tuachane na hilo niambie msichana mrembo jina lako ni nani?"

"Naitwa Feria"

Kumbukumbu zikarudi nyuma upande wa Zaki na kuliwaza jina hilo alilisikia wapi mara ya mwisho.

"Aaah ile siku tulipokuwa tunakimbilia hosteli baada ya Keti kuniambia kuna hatari na Bedo kuongea kuhusu kumfungulia binti huyu, Sasa nimepata picha halisi"

Zaki alijisemea akilini mwake huku akili ilimcheza cheza kuhusu jambo hilo.

"Vipi mbona upo kimya" Feria ilimbidi haulize kidogo

"Naomba unipe historia yako iliyowahi kukutokea hadi umefikia hapo ulipo, Mimi ni Askari mpelelezi niliyetumwa na serikali huru ya Tanzania kufatilia kesi yako baada ya mauaji yako yaliyotokea miaka 3 iliyopita wazazi wako bw na bi Romi walifatilia Sana kesi yako na kukata tamaa ya kakupata tena ila Kaka yako Khelumi hakuwahi kukata tamaa kabisa hadi mimi kuletwa hapa na sababu ya mimi kukuona na kukusikia ni mkufu huu uliopo shingoni kwangu nilipewa kabla ya kuanza kazi"

Turudishe matukio nyuma ilikuaje binti Feria kutoka kwenye hali ya ubinadamu na kuwa mzuka ambao haushikiki wala kuonekana... 

ZAKI NI ASKARI MPELELEZI LABDA WENGI WETU TULIKUWA HATULIJUI... 

Post a Comment

Previous Post Next Post