SIRI ZA CHUMBANI 08


Publish: 11/09/2020

ILIPOISHIA

"Ndio ndio ndio huyu msichana nilimuona siku ile ubaoni Profesa alivyokuwa anafundisha na ndiye aliyekuwa anahitaji kumchoma na kitu mgongoni ofisini kwake, huyu ni nani yake mbona analia hivi kuna siri kubwa imejificha kwenye hosteli hii" 

Zaki moyo wake uliongea maneno hayo mazito.
********************

"Moni usilie sielewi kwanini unalia ila huzuni yako imenigusa ghafla kwenye moyo wangu"

Moni alitoka taratibu kifuani kwa Zaki na kumtazama usoni kwa huzuni kubwa na kumuuliza....

"Jina lako nani halafu wewe ni mgeni chuoni hapa?"

"Naitwa Zaki, ndio ni mgeni namaliza wiki tangu nimefika chuo hiki. Pia asante kwa msaada ulionipatia leo uwanjani"

"Usijari Zaki karibu kwa mara nyingine chuoni hapa, umepapenda?"

Swali la Moni lilimgusa sana Zaki lakini halikuwa gumu kujibu

"Nimepapenda sana kumechangamka tangu nimefika eneo hili"

Zaki alijibu lakini moyoni mwake alisema "laiti ungejua mauzauza ninayokutana nayo acha tu"

"Kweli Zaki?"

"Ndio"

"Basi sawa karibu"

Moni alichukua picha ile nakuirudisha mahali alipoitoa.

"Naomba nikuulize swali Moni"

"Uliza bila Shaka"

"Huyo niliyemuona kwenye picha ni nani yako?"

"Ooh! Ni rafiki yangu kuna tatizo?"

"Apana nilivyofika nilikuona ukiitazama na kulia"

"Eeh nilimpenda sana sielewi niseme vipi"

"Unaweza nipa historia yake kidogo"

"Huu sio muda wake Zaki kwasababu upo hapa siku yoyote nitakupa historia yake, twende tukaoge si unajua chuo hiki saa 1 mwisho inabidi tuwe vyumbani"

"Sawa"

Zaki kwa mara ya pili swali lake linashindwa kujibiwa aliamua kurudi zake chumbani kujumuika na wenzake kwasababu alishaoga hakuwa na haja ya kwenda kuoga tena badala yake alichukua simu yake nakuwasha data lakini mnara haukupanda hata kidogo, alijaribu kutoka nje kutafuta mnara lakini hakufanikiwa..

"Ina maana huku mnara wa simu haupandishi hakuna Network duh!"

Zaki alirejea ndani kipindi hiko muda ulishaisha wakuwa tena nje.

"Zakiii" Keti aliyekuwa mmojawapo kwenye chumba walicholala alimuita

"Niambie Keti uko freshi?"

"Ndio Zaki nakuona upo bize na simu yako kuna shida?"

"Nilikuwa nahitaji kuingia hewani lakini mnara haupandi zaidi ya kuniletea sifuri"

"Inabidi siku nikitulia nikwambie sheria za hiki chuo ujue maana kama ni hivyo utasumbuka sana ila kiufupi huku hakunaga Network"

"Kivipi mbona siku ya kwanza nilipofika ofisini kipindi nahojiwa taarifa zangu zilikuwa zinaingizwa kwenye kompyuta au hazitumii umeme?"

"Network iliyokuwepo ni ofisini kwa walimu tu na wao wakitoka mule huku nje network hakuna"

"Hayo ni maajabu sasa tuishi sehemu moja halafu network isiwepo sehemu nyingine, sehemu nyingine iwepo mbona nashindwa kuelewa.."

"Ndio hivyo Zaki kwani ulikuwa na shida nayo sana?"

Kabla Zaki hajajibu alianza kusikia sauti ya kilio Kama mtu analia upande wa nje, alijaribu kusimama ili hasikie vizuri kwa ukaribu zaidi.

"Keti kuna mtu analia"

"Mtu analia nani?"

"Nasikia kabisa kuna mtu analia nje"

"Wewe unausingizi, hivi jamani kuna mtu kati yetu anasikia kelele za mtu nje akilia?"

Keti ilimbidi haulize kwa mshangao mkubwa sana, lakini kila mtu alijibu "hapana"..

Zaki maswali yalianza kumjia kwa mfululizo kichwani kwake, Nani analia? Kwanini nisikie sauti yake peke yangu? Ina maana richa ya kuwaona hadi sauti zao na uwezo wa kuzisikia?

ZAKI ANASIKIA SAUTI ZA MIZUKA JE ATATOKA NJE NINI USHAURI WAKO KWAKE? Usikose sehemu ya 09 

Post a Comment

Previous Post Next Post