SIRI ZA HOSTELI 07


Publish: 09/09/2020

ILIPOISHIA

"Wametokea wapi watu hawa waliovalia nguo nyeupe na kwanini wamejiunga nasi kwenye michezo ina maana hawa wanachuo hawawaoni au wanafanya makusudi inanibidi niwaaminishe kuwa kuna watu wa dunia nyingine mahala hapa"
******************

Zaki aliendelea kucheza mpira huku macho yake hayakuacha kuwatazama mizuka ile 

"Aisee kuna mizuka ina maumbo na sura nzuri kwanini hawapo kwenye dunia yetu?"

Kipindi anaendelea kuwatazama mizuka hiyo alishangaa mbele yake mzuka mmoja ukija kwa kasi kuchukua mpira uliokuwepo mguuni kwake. Zaki alishtuka hali iliyosababisha kuanguka chini na mzuka ule ulimpita kupitia mwili wake hata mpira hakugusa kutokana na kukosa uwezo wa kibinadamu...

"Zaki vipi upo salama" ilikuwa sauti ya msichana mwengine tofauti na Keti huyu alitambulika kama Moni ni msichana aliyekuwa mshangiliaji kwenye mchezo huo...

"Nipo sawa" Zaki alinyanyua macho yake kumtazama msichana huyo mgeni kwenye maisha yake...

"Amka utoke uwanjani kwa muda huu"

Msichana huyo alimkokota akisaidiana na watoa huduma wa mahali hapo, Zaki bado aliendelea kumtazama binti huyo hasielewe kwanini alimkimbilia kumsaidia wakati hakuwahi kumpa msaada siku zote.

"Aaaaaagha" ilikuwa sauti ya kijana Zaki aliyeugulia maumivu makali sana kwenye mwili wake  

"Utapona sawa" sauti nyororo ya msichana Moni ilimnyamazisha Zaki.

"Zakiiiiii" naye Keti kwa bashasha huku akikimbia mahali alipo alimuita 

"Keti ulikuwa upande gani?"

"Niliondoka hapa kwenu nikaenda kwa majirani zetu wa mpira wa kikapu ndipo niliposikia wamekuangusha uwanjani baada ya kuwafunga sanaaaa" huku akicheka 

"Kumbe na wewe ni mcheshi sana Keti"

"Eeh kuna muda"

"Ngoja niwaache kidogo naelekea kwenye mpira wa kikapu" Sauti ya msichana Moni iliwaaga...

Zaki alimtazama na kukumbuka kitu....

"Keti yule dada unamjua si ndio anaitwa nani?"

"Namjua vyema sana jina lake anaitwa Moni"

"Nahitaji kumpa Asante alinisaidia kunileta hapa"

"Aaah sawa nikampe?"

"Apana nahitaji kumshukuru mwenyewe"

"Sawa yupo darasa moja nasi Ila hosteli tofauti yeye yupo juu kabisa"

"Ghorofa ya 4?"

"Ndio"

"Sawa nitamuona baadae"

Maongezi yaliisha na Zaki alisimama huku akiugulia maumivu kwa mbali alitembea zake taratibu kurudi zake hosteli mwenyewe nakuingia bafuni kujimwagia maji. Alipomaliza alilala zake kitandani huku mawazo yalimpeleka mbali sana kumfikiria binti yule Moni.

"Kwanini alikuwa wa kwanza kunisaidia?"

Zaki alinyanyuka alipoona wanachuo wakirudi hosteli alivaa viatu vyake na kuondoka zake kutoka nje

"Inabidi niende ghorofa ya 4 sasa"

Kwakuwa hakukuwa na lifti basi alipandisha ngazi huku akikimbia kuelekea juu. Aliulizia baadhi ya wanachuo kuhusu msichana huyo na kupata majibu, alifika karibu na mlango wa chumba alicholala nakupiga hodi lakini mlango ulikuwa wazi aliingia na kumuona msichana huyo aliyekuwa peke yake akitazama kitu mikononi...

"Samahani nimeingia baada ya kugonga sana nilikuja kukushukuru"

Zaki alivyozidi kumsogelea karibu aligundua msichana huyo alikuwa analia...

"Moni"

Aliposikia jina alinyanyua uso wake kumtazama Zaki usoni.

"Kwanini unalia?" 

Zaki aliketi kitandani alipokuwa Moni nakumkumbatia, lahaullah! Zaki alishuhudia kitu kile alichokuwa amekishika ni picha ya msichana mrembo sana. Mawazo ya Zaki yalimpeleka mbali nakugundua kama aliwahi kumuona sehemu msichana huyo...

"Ndio ndio ndio huyu msichana nilimuona siku ile ubaoni Profesa alivyokuwa anafundisha na ndiye aliyekuwa anahitaji kumchoma na kitu mgongoni ofisini kwake, huyu ni nani yake mbona analia hivi kuna siri kubwa imejificha kwenye hosteli hii" 

Zaki moyo wake uliongea maneno hayo mazito.

KWANINI ANALIA HAKIKA HII STORI ISIKUPITE KUNA MENGI YA KUJIFUNZA HUMU. Usikose sehemu ya 08 

Post a Comment

Previous Post Next Post