SIRI ZA HOSTELI 06


Publish: 08/09/2020

ILIPOISHIA

Zaki alimkatisha rafiki huyo na kumgeukia mdada wa upande wake wa kushoto na kumuuliza swali lilelile kuwa amemuona yule msichana pale ubaoni lakini majibu yalikuwa yaleyale kuwa "hakuna mtu zaidi ya Profesa". Zaki alitulia kama maji kwenye mtungi na kubaki na maswali kichwani mwake....

"Ina maana namuona peke yangu?"
*****************

"Wanachuo sitafundisha sana leo zaidi ya kuwaachia maswali machache ambayo mtayajadiri mkitoka hapa" sauti ya profesa ilipaa kwa kila mmoja na yeye aliondoka zake

Zaki alimuona binti yule aliyemfata nyuma profesa hakutaka kukaa tena darasani hapo badala yake alienda kufatilia nyuma nini kitaendelea, binti yule aliyevalia vazi jeupe alizidi kumfata nyuma Profesa hadi alipoingia ofisini.

Zaki alibaki kuchungulia dirishani kutazama nini kingejiri, Profesa alivyokaa kwenye kiti chake cha kuzunguka binti yule alinyanyua mfano wa kitu alichokishika mkononi na kukaa tayari kumchoma nacho maeneo ya mgongoni, hali ile Zaki aliiona na kukimbia haraka kuingia ofisini kumvaa yule binti asifanye alichokikusudia. Huwezi amini Zaki alimrukia badala yake yeye alianguka chini kutokana na binti yule asiyekuwa mtu wa kawaida lakini kwenye macho ya Zaki alionekana ni binadamu kama wengine alipotea aliposhindwa kutimiza haja yake...

"Wewe vipi mbona umeingia ofisini bila hodi na umenivamia ghafla" Profesa alifoka kwa hasira

"Profesa nisamehe bahati mbaya nilimuona mdudu mfano wa nyuki akikusogelea nilizani ningempata lakini haikuwa kama nilivyotaraji"

"Wanachuo wa siku hizi hamna adabu kabisa embu nitokee hapa"

Zaki aliondoka kwa aibu lakini akili yake ilimfikiria binti yule aliyemuona kisha alipotea ghafla.

"Zakiii" ilikuwa sauti ya msichana Keti ikimuita

"Naam Keti upo poa"

"Ndio nimekutafuta sana twende kwenye michezo ya hapa chuoni"

"Aaha kumbe kuna michezo chuoni hapa"

"Ndio twende bhana"

Keti alimvuta Zaki waelekee kwenye michezo.

Uwanjanii......

Michezo iliendelea huku Keti alimzalimisha sana Zaki ajiunge Mpira wa miguu kwakuwa yeye mwenyewe alipenda basi alikubali kwa moyo mmoja kujiunga na kuingia uwanjani...

Mechi ilianza ya kutafuta magoli uwanjani ilikuwa mshikemshike huku Zaki alionyesha umaarufu wa kuwa mbele kwenye ufungaji wa magoli, mabinti kibao walimshangilia sana mwanachuo mgeni kuonyesha uwezo wake...

Kipindi Zaki yupo uwanjani anaendelea kulisakata vumbi anashuhudia mizuka kibao ikiwa uwanjani hapo, mwanzo alimuona mmoja darasani lakini safari hii aliiona kibao wengine walikuwepo sehemu ya ushangiliaji wengine aliwaona sehemu ya Mpira wa kikapu kibaya zaidi wengine walikuwepo kwenye Mpira wa miguu wakicheza na wao.

"Wametokea wapi watu hawa waliovalia nguo nyeupe na kwanini wamejiunga nasi kwenye michezo ina maana hawa wanachuo hawawaoni au wanafanya makusudi inanibidi niwaaminishe kuwa kuna watu wa dunia nyingine mahala hapa"

ZAKI ATAFANYA NINI? Usikose sehemu ya 07 

Post a Comment

Previous Post Next Post