SIRI ZA HOSTELI 05


Publish: 31/08/2020

ILIPOISHIA

"Huu sio muda wa kuongea tusalimishe maisha yetu kwanza"

Keti alimshika mkono Zaki na mbio zikaanza kurudi hosteli
***********

Walizidi kukimbia huku Keti alizidi kumuhamasisha Zaki asigeuka nyuma wala akisikia sauti gani inamuita, maneno ya Keti yalikuwa kweli walivyokuwa wanakimbia kitu mfano wa upepo ukujao kwa kasi sana ulikuwa unakuja nyuma yao.

"Zaki kama nilivyokwambia usigeuke nyuma ni hatari kwako na kwangu" 

"Sawa Keti nimekuelewa sana"

Walifika kwenye lango la kuingilia hosteli huku waligonga kwa nguvu wapate kufunguliwa, mpenzi wa Keti kijana Bedo aliwahi kufungua na wao waliingia....

"Mna hatari sana mmefungua mzimu wa Feria uliofungwa muda mrefu sana usitudhuru na hili nililijua tu tangu amefika huyu kijana, ona sasa ameleta mabalaa"

"Nyamaza Bedo ameleta mabalaa gani wakati yalikuwepo tangu zamani nini unazungumza"

"Unamtetea ni mpenzi wako?"

"Huyu ni mwanafunzi mwenzetu kumbuka hilo"

"Sihitaji kujua lolote kumuhusu"

Bedo alijiondokea zake kwa hasira, huku Zaki alimsogelea Keti nakumfuta machozi yaliyokuwa yanamtoka 

"Nyamaza Keti una roho ya kipekee tangu nifike chuoni hapa kwa haya mauzauza niliyokutana nayo haikuwa rahisi mtu yeyote kuwa karibu yangu kunisaidia wewe ni wa pekee"

"Zaki twende ndani ukapumzike"

"Naomba kabla ya kuingia ndani uniambie kuhusu huo mzimu wa Feria"

"Stori ni ndefu sana Zaki huu sio muda wake"

Keti alitangulia kuingia ndani vyumbani huku Zaki naye hakutaka kubaki alimfata.

Majira ya 2 kamili ya asubuhi hali ile ilitulia na wanafunzi walirejea hali ya kawaida, muda wa kuoga na kujiandaa kwenda madarasani uliwadia. Na kila mwanachuo akiwemo Zaki safari hii hakutaka kubaki kabisa aliongozana na wenzake kuelekea darasani.

Walipofika darasani Zaki alikaa siti ya upande wa katikati huku macho yake yalimtafuta Keti nakugundua alikaa nyuma na kijana Bedo. Profesa aliingia na tamko la kwanza aliongelea juu ya hali iliyotokea asubuhi japokuwa hakuongea kwa undani zaidi lakini baadhi walielewa kusudi ni lipi.

Kipindi Profesa anaendelea kuzungumza Zaki anashuhudia msichana aliyevalia vazi jeupe huku nywele zake zikiwa zimejiachia sana kiasi cha kuficha hadi sura akiwa ubaoni anatazama darasa.

"Unamuona yule dada" ilikuwa sauti ya Zaki aliyemuuliza kijana wa pembeni yake lakini majibu aliyojibiwa yalikuwa 

"Msichana gani"

"Yule pale ubaoni"

"Wewe umepagawa Profesa msichana?"

"Au basi basi basi"

Zaki alimkatisha rafiki huyo na kumgeukia mdada wa upande wake wa kushoto na kumuuliza swali lilelile kuwa amemuona yule msichana pale ubaoni lakini majibu yalikuwa yaleyale kuwa "hakuna mtu zaidi ya Profesa". Zaki alitulia kama maji kwenye mtungi na kubaki na maswali kichwani mwake....

"Ina maana namuona peke yangu?"

ZAKI ANAONA MIZUKA...ITAKUAJE... usikose sehemu ya 06 

Post a Comment

Previous Post Next Post