Publish: 29/08/2020
ILIPOISHIA
Kitendo kilichosababisha Keti aamke na kutaka kutoka nje ila mkono wa kijana Bedo mwanafunzi mwenzake kwa upande mwengine ndiye mpenzi wa Keti chuoni hapo uliuwahi mkono wa Keti na kuushika kwa nguvu..
"Unakwenda wapi wakati unajua chuo hiki hakiruhusu mtu kutoka majira ya Alfajiri"
**********************
"Bedo huyu mwanafunzi ni mgeni mahali hapo hajui chochote kuhusu chuo hiki"
"Muache ikifika saa 1 utaenda kumuangalia"
"Unaongea kuhusu nini, niachie mkono wangu ni utu gani unanifundisha"
"Keti naongea kama mpenzi wako"
"Nimekuwa mtu wa kukusikiliza muda wote ila sio kwahili jambo anahitaji msaada wetu"
"Sawa nenda"
Keti alitoka ndani haraka na kumuacha Bedo aliyerudi kujifunika shuka.
"Zaki, Zaki uko wapi" ilikuwa sauti ya msichana Keti ikiita alipotoka nje
"Zaki uko wapi nimekuja kukusaidia"
"Zakiiiiii"
Keti aliendelea kuzunguka kutokana na ukubwa wa chuo hiko, alimtafuta hadi majira ya saa 12 na nusu yaliingia
"Zaki tusamehe Sana hatukukwambia sheria za chuo hiki mapema"
Keti alichuchumaa chini na kuanza kulia ghafla alisikia sauti ya mtu anayehema kwa kasi sana, alinyanyuka na kufatilia sauti hiyo huku taratibu aliona buti moja la kijana Zaki alipoendelea kutembea alishuhudia buti jengine.
"Zaki upo mahali hapa ila upo wapi?"
Keti aliendelea kufatilia ndipo alipomuona Zaki amening'inia kwenye shimo lefu la chuoni hapo huku akiwa ameshikiria mti mdogo sana uliomsaidia asianguke. Keti alimkimbilia kwa haraka zaidi
"Zaki upo sawa"
"Keti nisaidie nimeshikiria hapa kwa muda mrefu sana"
"Usijari sawa nipo hapa msaada umefika"
"Sawa"
Keti aliangaza angaza kama angeona kamba au mjiti lakini alikosa ikambidi kukata mti mdogo wa matunda uliokuwa karibu na shimo hilo kisha aliusukuma hadi chini kumtoa Zaki, naye alishikiria vyema hadi kutoka shimoni hapo.
"Asante Keti"
"Usijari Zaki"
Ila kitendo cha Keti kukata mti ule ghafla giza nene lilitokea huku radi nyingi sana zililia mawinguni na mwanga wa radi ulionesha shimo lile lilivyokuwa linajifunga taratibu
"Keti tazama shimo linajifunga"
"Zaki tupo kwenye hatari inatubidi tuwahi mapema sana kurudi ndani ya hosteli"
"Kuna nini Keti"
"Huu sio muda wa kuongea tusalimishe maisha yetu kwanza"
Keti alimshika mkono Zaki na mbio zikaanza kurudi hosteli
KWANINI WANAKIMBIA, WATAWAHI KUFIKA KWENYE LANGO LA HOSTELI?
Usikose sehemu ya 05
Tags:
CHOMBEZO