SIRI ZA HOSTELI 03


Publish: 26/08/2020

ILIPOISHIA

"Kwanini inakutokea hali hiyo nilikuwa ghorofa ya tatu nikifanya mazoezi ndipo nilipokuona ukitembea kwa machale sana nikaona labda utakuwa haupo sawa nikashuka haraka kukutazama"

Zaki alionekana kama mtu mwenye mawazo sana asielewe amjibu nini binti huyo.
****************

Alijiondokea zake mahali hapo pasipo kusema chochote. Keti alimtazama sana Zaki aliyekuwa mwenye mawazo sana hali iliyomsababishia adhoofike kiakili.

"Pole Zaki ugeni unakusababishia yote hayo ila natumaini utakuwa sawa hivi karibuni".

Zaki alirudi ndani alipokuwa mwanzo nakutulia zake ikiwa tayari muda wa jioni wa saa 12 ulishaingia, alisikia kelele za wanafunzi wakirejea kutoka walipotoka mmojawapo alikuwepo Keti. 

Zaki alijifunika shuka gubigubi asisikie sauti hizo huku macho yake yaliyokuwa ndani ya shuka yalitoa machozi taratibu. Ndipo sauti ya msichana Keti ilimuita kwa mara nyingine

"Zaki muda huu ni wa kuoga na kupata chakula tafadhali amka kabla ya kufika saa 2 usiku inabidi tuwe vyumbani kwaajili ya kulala"

Zaki hakujibu lolote badala yake alizidi kujifunika kwa uoga wa hali ya juu. Keti alipomuona hataki kuamka aliondoka zake akiwa na baadhi ya marafiki zake wa hapo chumbani. Kwa mara ya pili Zaki alibaki mwenyewe chumbani hapo akiwa kwenye shuka usingizi ulimpitia wa dakika.

Muda ulienda hadi kufikia mida ya saa 1 na nusu usiku wanafunzi walirejea hosteli kwa kelele kama ilivyo awali tena za safari hii zilimuamsha hadi kijana Zaki. 

Waliingia na kila mmoja aliwahi kitanda chake, hosteli hiyo haikuwa kitu cha ajabu jinsia mbili kulala chumba kimoja kutokana na ukubwa wa chumba pia na sheria zao ziliwabana iwe hivyo. 

Wenzake waliporudi Zaki aliamka kufungua begi lake alichukua taulo pamoja na sabuni na kutoka zake nje kidogo ilikuwa ukifungua mlango tu unaingia milango ya kwenda bafuni kisha kulikuwa na mlango mkubwa wakutoka nje kabisa kwenda kwenye hosteli zengine.

Zaki alioga taratibu huku maji baridi yalimpiga usoni na kurejesha furaha ya nyumbani kwao alipomaliza alitoka zake na kurudi ndani kulala huku kila mmoja alimshangaa pasipo kumsemesha kitu. Kwakweli njaa ilimuuma sana japo hakuonyesha kwa mtu yeyote badala yake alivaa shati yake na bukta na kulala zake.

Alfajiri ya saa 11 Zaki alikuwa wa kwanza kuamka alichukua mkufu wa wazazi wake alioupenda sana haikuwa rahisi kuuacha pasipo kuvaa ilihali muda wa kulala tu. Zaki alivaa mabuti yake ya mazoezi na kutoka zake nje kupasha viungo kama alivyozoea hata alipokuwa nyumbani. Lahaula! baada ya dakika kama 5 hivi zilisikika kelele upande wa nje kijana Zaki akiomba msaada....

"Nisaidieni" Alipiga yowe la nguvu

Kitendo kilichosababisha Keti aamke na kutaka kutoka nje ila mkono wa kijana Bedo mwanafunzi mwenzake kwa upande mwengine ndiye mpenzi wa Keti chuoni hapo uliuwahi mkono wa Keti na kuushika kwa nguvu..

"Unakwenda wapi wakati unajua chuo hiki hakiruhusu mtu kutoka majira ya Alfajiri"

Usikose sehemu ya 04. KIMEMKUTA NINI KIJANA ZAKI. JE KETI ATATOKA IKIWA AMESHIKIRIWA? 

Post a Comment

Previous Post Next Post