SIRI ZA HOSTELI 02


Publish: 24/08/2020

ILIPOISHIA

Zaki alimuaga sekretari kwa kumpa asante alimpungia mkono, alipomaliza aliikimbilia hosteli aliyoiona kwa mbali sana huku shauku ilimjaa moyoni mwake. Huwezi amini alipokaribia mazingira ya hosteli alirushwa na shoti ya ajabu na kasi aliyokuwa nayo ilimrusha juu sana macho yake yalifumbua mara moja nakuona mstari mwekundu wa ajabu tunaweza sema ni uzio ukiwa umezunguka hosteli hiyo na ghafla macho yake yalifumba hapohapo na kuanguka chini kama mzigo wa kuni.
******************

Zaki alikuja kushtuka kazungukwa na wanafunzi wenzake wengi wao walikuwa wakike hakupiga kelele alijikaza kwa uhodari kisha alianza kumtazama mmojammoja kwa mshangao mkubwa ilisikika sauti ya binti ikimkaribisha...

"Karibu usiogope sisi ni wanafunzi wenzako pia tumekuokoa kukuleta ndani hapa"

Zaki hakujibu lolote badala yake alinyanyuka kidogo na kutizama nje alikuwa wapi lahaula! Alijiona yupo hosteli hapo ambapo alipigwa shoti muda mfupi uliopita.

"Naombeni nipumzike" Zaki aliwaomba kwa mshangao na uoga wa hali ya juu hata walipomuacha mwenyewe usingizi haukumfika kabisa badala yake alifungua begi lake na kutoa mkufu wa thamani aliopewa na wazazi wake kabla ya kuja chuoni hapo...

Alikaa kwa muda mrefu mwenyewe alihisi ukimya umetawala sana kuashiria hakuna mtu aliyekuwepo hosteli hapo...

"Hellloooo! Kuna mtu nje hapo" Zaki alijaribu kuita lakini wapi sauti yake ilijirudia mfano wa mwangwi mzito..

Alinyanyuka kwa uoga huku mkono wake wa kulia alishika biblia kitabu alichopendelea kukisoma sana alipokuwa nyumbani kwao. Alitoka na kutembea taratibu huku alishuka ngazi kwa uoga hadi nje akiwa anatembea kwa hofu alikaribia eneo lililomrusha na shoti kipindi anaingia mahali hapo alinyanyua mkono wake wa kushoto na kujaribu kushika, kabla ya kukaribia kushika sehemu ile iliyoonekana kwa macho ya kawaida palikuwa hakuna kitu ilisikika sauti nyuma yake ikimuita...

"Wewe"

Zaki alishtuka na kuanguka katikati ya uzio ambao aliuona kipindi anaingia..

"Vipi upo sawa?" Alionekana binti nazani ni yule aliyemuaga alipokuwa ndani na kumuacha Zaki apumzike.

"Wewe ni nani?" Zaki ilimbidi aulize kwa uoga wa hali ya juu

"Naitwa Keti ni mwanafunzi kama wewe katika chuo hiki ila sio mgeni"

"Naitwa Zaki"

"Oh basi nyanyuka kwanza hapo chini"

Zaki alinyanyuka taratibu huku macho yake yalimtazama sana Keti kwa umakini..

"Una matatizo ya kuanguka anguka?"

"Apana"

"Kwanini inakutokea hali hiyo nilikuwa ghorofa ya tatu nikifanya mazoezi ndipo nilipokuona ukitembea kwa machale sana nikaona labda utakuwa haupo sawa nikashuka haraka kukutazama"

Zaki alionekana kama mtu mwenye mawazo sana asielewe amjibu nini binti huyo.

Usikose sehemu ya 03. 

Post a Comment

Previous Post Next Post