SIRI ZA HOSTELI 01


Jioni ya alasiri waswahili wanasema jua la saa 9 likiwa limeingia kijana Zaki anawasili chuoni kwa mara ya kwanza akitokea mkoani Dar_es_salaam jasho jingi likimtiririka huku macho yake mfano wa uwaridi yakiangaza mazingira ya chuoni hapo...

"Hakika hiki chuo sikuchaguliwa kwa bahati mbaya japokuwa kipo ndani sana pia mbali na kijiji lakini kinavutia mno kweli mkoa huu wa Tanga ni mzuri sana, NIMEPAPENDA!" Zaki alijisemea maneno hayo matamu moyoni mwake akiwa na begi la mgongoni huku mkono wa kushoto akiwa amebeba begi lake kubwa la nguo alitimua vumbi kwa kuriburuza akikimbia harakaharaka kuelekea ofisi kuu za chuoni hapo.

Alifika na kukuta vurugu walimu wawili waliokuwa wanarushiana maneno machafu mmoja akidai kutorudi tena chuoni hapo hata angepandishwa cheo na kulipwa pesa nyingi kiasi gani na mwengine akimjibu bora uondoke umekuwa ukileta nuksi tangu uhamishiwe chuo hiki. Zaki alibaki akishangaa asielewe nini kinachoendelea kwa taratibu alipiga hodi akiwa tayari yupo mlangoni, ilisika sauti ya mwalimu mwengine tofauti kabisa na wale wawili waliokuwa wakigombana. 

"Karibu kijana unaonekana ni mwanafunzi mpya"

Mwalimu huyo aliyeonekana umri umekwenda sana alimkaribisha kwa bashasha kijana Zaki.

"Asante sana nazani hapa ndipo ofisini kama ramani yangu ilivyonielekeza"

"Bila shaka ujio wako tuliupata" 

Mwalimu huyo alijibu huku aliyeonekana kuwa bize sana na kompyuta akibonyeza bonyeza kisha na kumuuliza Zaki

"Umetokea Dar_es_salaam?"

"Ndio"

"Taarifa zako ninazo hapa japokuwa umechelewa kidogo sio sana lakini"

"Si unajua ni mara ya kwanza naingia chuo sikuweza kujua baadhi ya vitu vilikuwa vinanichelewesha"

"Usijari tulishakusajiri kila kitu ni muda wako wewe kuanza masomo tu, subiri nimpigie sekretari wa hapa akupeleke ukaweke mizigo yako hosteli"

"Sawa"

Simu ilinyanyuliwa na baada ya muda mfupi sekretari alikuja kumfata Zaki huku bado akiwa anapelekwa hosteli alizidi kushangaa mazingira ya chuoni hapo, chuo kilichopo ndani kabisa ya mji. 

Walipokuwa wanakaribia mazingira karibia na hosteli sekretari alimuacha Zaki aende mwenyewe huku akimwambia kuna watumishi wengine wanaohusika wangempokea, yeye jukumu lake lilikuwa kumuonyesha majengo ya hosteli hizo.

Zaki alimuaga sekretari kwa kumpa asante alimpungia mkono, alipomaliza aliikimbilia hosteli aliyoiona kwa mbali sana huku shauku ilimjaa moyoni mwake. Huwezi amini alipokaribia mazingira ya hosteli alirushwa na shoti ya ajabu na kasi aliyokuwa nayo ilimrusha juu sana macho yake yalifumbua mara moja nakuona mstari mwekundu wa ajabu tunaweza sema ni uzio ukiwa umezunguka hosteli hiyo na ghafla macho yake yalifumba hapohapo na kuanguka chini kama mzigo wa kuni.

ITAKUAJE NDIO KWANZA ZAKI ANAFIKA CHUONI HAPO KWA MARA YA KWANZA NA VIMBWENGA VINAANZA USIKOSE SEHEMU YA 02.

INAENDELEA.......🙏 

Post a Comment

Previous Post Next Post