SIRI ZA CHUMBANI 13



ILIPOISHIA

Alinikabidhi, niliyanywa ila kizunguzungu nilichokihisi hakikuwa cha kawaida nilianguka na kupoteza fahamu kilichojiri sikutambua.
************

Nilikuja kushtuka muda ulienda sana na pembeni yangu nilimshuhudia mkuu wa chuo hiki akinitazama huku alifurahi sana, nilijipapasa kwenye mwili wangu nakugundua alinibaka. 

Kilio kilianza upya huku alinitishia endapo ningemwambia mtu angeniua haraka sana. Nilinyanyuka taratibu sikumjibu lolote. Makazi ya mkuu huyo yalikuwa nje kidogo na chuo hiki nilijiburuza nakutoka nje nikiwa nimechafuka sana, alijaribu kunisimamisha na kunilazimisha nisiende popote nikiwa kwenye hali niliyokuwa nayo lakini moyo wangu haukumsikia wala kumuelewa nilijawa na hasira na kumtazama kwa mara ya mwisho. 

Kisha nilijiburuza kuondoka zangu ilikuwa mida ya usiku mwingi uoga wote ulinitoka kutokana na fedheha niliyofanyiwa moyo wangu ulivuja damu ya kilio muda wote nilipata maumivu sana sehemu za Siri lakini sikuchoka kutembea, nikiwa njiani nilishuhudia kwa macho yangu Mkuu alikuwa na vijana nane waliokuwa wakinitazama na mikononi mwao walishika silaha za kila namna. 

Nilipiga kelele moja tu sikufanikiwa kuongeza ya pili safari hii walinibaka wote hakuna aliyeniacha walipomaliza nikiwa nipo chini nilimuona Mkuu kakamata kisu alinichoma mara 3 kufuta ushahidi kama nilikuwepo duniani. Aliponichoma nilishuhudia nikiwa mzima huku mwili wangu ulikuwa chini umelala nilijishikashika kama nilikuwa mimi kwa mbele yangu nilimuona mzee ambaye nilikutana naye kipindi nakuja chuoni kwa mara ya kwanza na kudai sikumsalimia. Alinitazama na aliniambia..

"Binti usiwe na huzuni haupo kwenye hali ya ubinadamu tena tayari wewe ni mzuka"

Bibi yule alicheka sana tena kwa nguvu kisha alipotea nilishuhudia kwa mara nyingine mwili wangu ulibebwa na vijana wa Mkuu nakupelekwa chuoni ambapo walishachimba shimo tayari waliutupa mwili wangu nakufukia. Nilipiga kelele ya hasira iliyosababisha kukata mawasiliano kati ya watu waliomo chuo na walio nje ilikua si kompyuta, simu, saa wala aina yoyote ya mawasiliano ilifanya kazi nilivyozidi kupiga kelele ya hasira ndipo milango yote ya kutoka ilijifunga ilikuwa wa nje anaweza kuingia ndani ila wandani hawezi kutoka nje.

FERIA ALIISHIA HAPO lakini Zaki aliendelea kumuuliza

"Kwanini nimeona mizuka ya watu wengi sana chuoni hapa wakati waliohusika walikuwa vijana nane tu?"

FERIA ALIENDELEA KUSIMULIA

niliposababishiwa hali hiyo sikuwa na akili tena ya kibinadamu nilianza kuua kila mwanachuo kwa wiki walikufa wanachuo 3 hali ilivyozidi kuendelea huku nilikuwa namaliza taratibu waharifu wangu hadi walipobaki wawili ambapo wanachuo walianza kushtuka kutoniona chuoni na kisha vifo vya wanachuo wenzao huku bado adui yangu Mkuu nilimshuhudia hakiwapa simulizi za uongo kwamba nilitoroka chuoni. Nilipojaribu kumfata mkuu kwenye nyumba yake nilishindwa kuingia kutokana na mitego aliyoiweka haikuwa rahisi mimi kuingia katika nyumba yake.

Walileta waganga wakila namna kunizuia nisiwateketeze hadi walipofanikiwa kunifunga kwenye mti ambapo walinizuia kutoka tena huku masharti walipewa kutotoka kila majira ya alfajiri na jioni ya saa 12 kuwa kwenye hosteli zao.

Zaki alimuuliza swali la pili baada yakupata jibu la swali lake la kwanza....

"Kati ya hao vijana nane ulisema kabaki mmoja na Mkuu tu huyo mmoja aliyebaki ni nani hapa chuoni na majina yake?"

"Kijana aliyebaki ni mwanachuo wakawaida na majina yake ni Bedo Idan Kwizu"

"Bedo huyu mchumba wa msichana Keti?"

"Ndio"

Zaki macho yalimtoka na kuvuta taswira ya kijana Bedo alivyokuwa akimzuia Keti hasimsaidie kwa lolote lile.

ZAKI KAGUNDUA SIRI KUBWA KUHUSU KIJANA BEDO ITAKUAJE? Usikose sehemu ya 14 

Post a Comment

Previous Post Next Post