SIRI ZA HOSTELI 14



ILIPOISHIA

"Bedo huyu mchumba wa msichana Keti?"

"Ndio"

Zaki macho yalimtoka na kuvuta taswira ya kijana Bedo alivyokuwa akimzuia Keti hasimsaidie kwa lolote lile.
*************

"Naomba nikuombe kitu" Zaki alitoa kauli kwa Feria Mzuka unaoishi 

"Sawa unaweza kuomba"

"Naomba ufungue Networki ya eneo hili ili mpango wangu ukamilike wa kukamata wahalifu waliokufanyia unyama huo nakuomba usifanye jambo lolote baya nimekuja kwaajili yako"

Zaki alimaliza maneno hayo nakumuacha Feria peke yake kikubwa na cha mwisho alimwambia 

"Nyamaza kulia sauti yako inaumiza ufahamu wangu itanifanya nifanye vitu kwa haraka"

Feria alimjibu "Sawa" nakutoweka mahali pale kimiujiza 

Zaki aliondoka haraka na kurudi hosteli akiwa mzima kitendo ambacho kila mmoja alimshangaa hakiwemo msichana Keti.

"Zaki wewe ni mzima?" Aliongea msichana Keti huku machozi yalimtoka na kumkumbatia.

Akili ya Zaki haikucheza zaidi ya kumtazama kijana Bedo aliyekuwa anamuheshimu sana hata alipoleta ugomvi alijizuia kwa heshima yake.

"Wakati wako umekwisha Bedo kila baya ulilolifanya litalipwa hapa" Maneno ya hasira yalimtoka Zaki moyoni mwake 

Zaki waliachiana na Keti nayeye akarudi kwenye kitanda chake kujipumzisha.

Asubuhi ya furaha ilichipua huku akili ya Zaki haikuwa tena kwenye hali ya kusoma zaidi ya kufanya kazi yake alifungua kitabu chake alichokipenda sana kiliitwa "MAISHA YA MATESO" alipokuwa anasoma alisikia sauti za wanachuo upande wa nje kila mmoja alikuwa akiongea lake

"Aisee leo nimepata taarifa za mtandao"

"Itakuwa Networki imerudi jamani hata mimi kompyuta yangu imewaka"

"Nyie ni kweli nimewasha data na mnara umesoma, ili ni jambo la ajabu sana"

Muda wote Zaki alikuwa akisikiliza tu pasipo kusema lolote. Alitoka na kuelekea bafuni kujimwagia Kisha alipomaliza muda ulishafika wa kwenda darasani, wanachuo wote waliondoka na kumuacha Zaki aliyekuwa anatafuta kalamu aliyoiweka somo la mwisho alipokuwa darasani.

"itakuwa imeelekea wapi hii kalamu eeh nimeiona ni hii hapa"

Zaki aliponyanyuka alishtuka na ngumi nzito usoni mwake, alipotazama alimuona Bedo aliyekuwa akimcheka kwa dharau. Zaki hakukubali alimkamata Shati kwa nguvu zote naye Bedo alifanya hivyohivyo huku walitamkiana maneno ya kishujaa

"Sikia wewe achana na mpenzi wangu Keti naona haujafata masomo hapa chuoni zaidi ya wadada wa hapa"

"Niheshimu Bedo sawa Keti kama dada kwangu na mimi nimekuwa nikimchukulia hivyo siku zote tangu nilipofika chuoni hapa"

"Wewe ni malaya Kama walivyo wengine na kama umezoea nakwambia nitakuua"

Ngumi zilianza kulika Kati ya Bedo na kijana Zaki huku Bedo alimpiga kwa hasira za kuchukuliwa mpenzi wake Keti naye Zaki alirudisha hasira ya kumuona ni muharifu wa mauaji ya msichana asiye na hatia Feria.

 Hakukuwa na mtu mwengine zaidi yao ambapo ilikuwa hatari sana ya kuuana.

Ngumi ziliendelea kulika huku waliangushana na kugongeshana kwenye vitanda vya juu na chini ( double decker ) Zaki aliendelea kumpiga kwa hasira naye Bedo aliendelea kujibu kwa hasira.

NINI KITAFATA IKIWA HAKUNA MTU ZAIDI YAO? Usikose sehemu ya 15 

Post a Comment

Previous Post Next Post