ILIPOISHIA
Ngumi ziliendelea kulika huku waliangushana na kugongeshana kwenye vitanda vya juu na chini ( double decker ) Zaki aliendelea kumpiga kwa hasira naye Bedo aliendelea kujibu kwa hasira.
*******************
Ilifikia wakati Bedo alizidiwa nguvu kutokana na Zaki kuwa Askari aliyepitia mafunzo mbalimbali kuhusu upiganaji.
"Sikia wewe mimi namuheshimu Keti kama dada sio hivyo ufikiriavyo" Zaki alimaliza kumjibu hivyo Bedo aliyekuwa hoi taabani akiwa chini anaugulia maumivu.
Kisha Zaki aliondoka zake kwa hasira hadi darasani ambapo alimkuta Profesa akiwa bado anafundisha.
"Hodi" alianza kwa kubisha hodi
"Karibu ooh wewe ndiye kijana mgeni chuoni hapa?"
Zaki alijibu "Ndio Profesa"
"Ulikuwa wapi kipindi hadi kinaishia hiki?"
"Profesa nilikuwa natafuta kalamu yangu"
Wanachuo wote walicheka kicheko kisicho kawaida.
"Unajua unaongea na nani?"
"Hapana Profesa"
"Mkuu wa chuo hiki"
Zaki kumbukumbu ilimrudia nakukumbuka ndiye aliyekuwa baba wa Keti na ndiye muhalifu wa kwanza kuhusu kifo cha Feria.
"Aaah Mkuu kumbe, nilikuwa natafuta Kalamu nikasikia sauti ya msichana alikuwa akilia nilipotoka nje niligundua kuwa si wakawaida namaani....sh"
Kabla ya kumaliza mkuu alimuwahi na kumwambia
"Nenda kakae kwenye siti yako"
Zaki alifanikiwa kupita huku alimuacha na mawazo sana mkuu aliyeonekana kama mtu aliyechanganyikiwa, hata kufundisha hakuendelea tena.
"Ina maana Feria akunidanganya" moyo wa Zaki uliongea peke yake.
Mkuu alipotoka zilibaki kelele darasani humo ambapo kila mwenye simu, laptop aliitoa kuchezeachezea kutokana na Networki kuwepo.
"Zaki Mambo vipi" ilikuwa sauti ya msichana Moni aliyemfata Zaki aliyekuwa kimya muda wote
"Moni poa upo sawa"
"Nipo sawa sana Zaki, nilitegemea na wewe ungekuwa mmojawapo wa furaha hii ya kurudi Networki mahala hapa"
"Hapana nina furaha pia kwasababu imenipa urahisi wa kuwasiliana na wazazi wangu si unajua tangu nilivyofika hapa sikuwasiliana nao"
"Aaah sawa Zaki nimekuelewa"
"Nakuomba ukanisaidie kitu"
"Kitu kipi hiko?"
"Twende"
Zaki alimshika mkono Moni nakuondoka naye kipindi hiko Keti alishuhudia kitendo kile hali iliyosababisha aache kucheka na kufurahi pamoja na marafiki zake.
"Keti unatazama nini nje?" Zilikuwa sauti za marafiki zake wapendwa waliyependa kuwa naye muda wote
"Apana apana"
"Aaah sawa basi twendeni tukapate chakula"
Walinyanyuka kwenda kupata chakula huku Keti bado akili yake ilikuwa kwa Zaki alienda wapi na Moni.
Walipokuwa mgahawani sehemu ambapo wanachuo wote walipata chakula cha asubuhi, mchana na jioni chuoni hapo.
Keti alikuwa bado na mawazo ilifikia wakati hata chakula hakupata na kuwadanganya wenzake kuwa atarudi anaenda chooni mara moja. Keti aliwaacha na kuondoka zake mahali hapo.
Keti alipotoka tu alijitamkia maneno moyoni mwake...
"Lazima nijue wameelekea wapi"
ATAWAPATA? NA WAMEENDA KUFANYA NINI? Usikose sehemu ya 16
Tags:
CHOMBEZO