ILIPOISHIA
Keti alikuwa bado na mawazo ilifikia wakati hata chakula hakupata na kuwadanganya wenzake kuwa atarudi anaenda chooni mara moja. Keti aliwaacha na kuondoka zake mahali hapo.
Keti alipotoka tu alijitamkia maneno moyoni mwake...
"Lazima nijue wameelekea wapi"
********************
Aliendelea kufatilia pasipo kuwaona ila akili yake bado ilicheza maeneo ya hosteli tu,
"Hawawezi kwenda sehemu tofauti na Hosteli itakuwa wameelekea huko" Keti aliendelea kujisemea moyoni mwake huku aliendelea kuwatafuta,
Kwa mbali aliwashuhudia kwa juu ghorofa ya nne wakitembea kuelekea vyumbani.
"Wanaenda kufanya nini wenyewe ikiwa watu wote tupo huku"
Keti alitumia nafasi ya kuwahi hosteli kujua nini kiliendelea Kati yao. Alifika na kupandisha haraka ghorofa ya nne hakutaka kuchelewa hata kidogo alivyofika alisimama mlangoni kusikiliza nini kilijiri.
Lahaullah! Bahati nzuri au mbaya ya kijana Zaki alimuita Moni kujua taarifa sahihi ya mzuka Feria nia na madhumuni yake ni kurekodi kupitia Moni kwasababu Feria hakuwa mwanadamu wa kawaida ilikuwa ngumu sana kurekodi sauti na wengine wakasikia isingewezekana, kijana Zaki aligundua mapema na kutumia fursa ya kumrekodi Moni.
Waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha ndio kilichotokea kipindi Keti alipokuwa mlangoni alipata kusikia yote Zaki alipomwambia kuhusu kuonana na Feria, uwezo wa kumuona na kusikia na alivyomwambia kila kitu kuhusu kifo chake na waliohusika basi Zaki alimuomba Moni ahadithie alichokijua kuhusu Feria. Naye Moni alianza kuhadithia vilevile ambavyo Feria alisimulia hadi hao waliomfanyia tukio la kumbaka aliwataja hakiwemo kijana Bedo ndiye pekee alibakia kuishi na mkuu wa chuo. Kitendo kile Keti kilimfanya hashindwe kuvumilia na kupiga kelele kiasi kilichosababisha Zaki na Moni kusikia.
Keti alikimbia kuondoka mahali hapo hili wasimuone, alikimbia haraka hakutaka kurudi darasani alijua wangemuona upande wa juu na kugundua alikuwa yeye. Alishuka ngazi na kurudi chumba chao cha kulala ambapo alimkuta Bedo akiwa juu kaning'inizwa hasijue nani aliye mning'iniza na alifikaje, kwanini hasishuke.
"Nisaidie Keti kuna mtu kanikaba shingoni kwangu naumia sana nisaidie tafadhali" Bedo alilalamika huku akiugulia maumivu makali. Ndipo Zaki anaingia akiwa na Moni nakuona hali ya Bedo hakiwa taabani.
"Nisaidieni tafadhali"
Zaki alimuona Feria aliyekuwa amemkaba Bedo kwa nguvu sana
"Feria tafadhali muachie utamuua kabla ya kutimiza lengo letu" Zaki aliongea kwa huzuni huku kila mmoja aligundua kuwa aliyemkaba kumbe alikuwa Feria...
"Feria tafadhali muache mpenzi wangu nakuomba" Keti alimjua sana Feria enzi za uhai wake alimsaidia sana ila kwasasa alishindwa kumuona, kumsikia wala kumshika
"Zaki mwambie hakiri yale aliyotenda kwangu mbele yako huku ukichukua rekodi yake" Feria alimwambia Zaki kwakuwa ndiye mtu pekee aliyemuona na kumsikia.
Zaki alimtazama na kumsogelea Bedo aliyekuwa juu juu kama nguo iliyo kambani.
"Bedo tafadhali epuka hayo maumivu kwa kusema ukweli juu ya kifo cha Feria" Zaki alianza kuhoji..
"Sijui lolote mimi" Bedo alikataa
"Huwezi kutoka hapo pasipo kifo chako embu kiri kuwa ulimuua Feria hili hurudi kwenye hali yako ya kawaida"
"Naombeni mniache mimi sijui lolote wala si muhusika tafadhali mimi sijui lolote"
Bado Bedo alikataa kabisa. Feria aliomba mlango ufungwe..
"Zaki funga mlango huo"
Zaki aligeuka na kufunga mlango tena kwa nguvu zote hali iliyosababisha Keti kumsogelea na kuuliza kwa mshangao mkubwa
"Unataka kufanya nini Zaki mbona mnamlazimisha kuongea uongo hali ya kuwa si muhusika hajui lolote kuhusu mauaji ya Feria"
"Unajua kuwa hata baba yako ambaye ndiye mkuu wa chuo hiki pia ni muhusika wa mauaji ya Feria?"
"Hapana haiwezekani Zaki wanamsingizia Bedo na Baba yangu hawawezi kumuua Feria wakati baba aliyajua matatizo yote yaliyomkumba Feria hapa chuoni na ndiye aliyekuwa kipaumbele kumsaidia"
"Nikisema alikuwa anatumia Fursa ya kumtaka kimapenzi?"
"Hapana hapana Zaki"
"Keti nakuomba nilikuheshimu na sihitaji kuvunja heshima yako kaa mbali na kesi hii nzito ya Msichana Feria"
Keti alibaki kushangaa hasijue wala kuelewa kwanini walifunga mlango walitaka kufanya nini.
FERIA ANAHITAJI KUFANYA NINI UNAZANI BEDO ATASEMA? Usikose sehemu ya 17
Tags:
CHOMBEZO