SIRI ZA HOSTELI 17

ILIPOISHIA

"Keti nakuomba nilikuheshimu na sihitaji kuvunja heshima yako kaa mbali na kesi hii nzito ya Msichana Feria"

Keti alibaki kushangaa hasijue wala kuelewa kwanini walifunga mlango walitaka kufanya nini.
************************

Bedo aliangushwa chini kiasi kilichosababisha kuumia zaidi na Feria alianza kumpiga kipigo kisichoonekana huku Zaki akimlazimisha kukiri makosa yake.

"Naumia sana tafadhali"

"Sema ukweli nakwambia" Zaki bado aliendelea kumuuliza huku Bedo akichezea kichapo kutoka kwa msichana Feria

"Nasema nasema nasema tafadhali usiniumize"

Bedo alihisi maumivu makali sana akiwa yupo hoi taabani alianza kuongea ukweli wake wote..

"Tuliamshwa usiku sana na Mkuu wa chuo akidai alituhitaji kumfanyia kazi ya haraka sana tuliitika bila kusita na kukubaliana naye lakini tulikuja kushangaa kazi aliyotupatia ni kumuua msichana Feria hali iliyosababisha wengi wetu kukataa lakini alitulaghai kwa pesa na vitisho vya kutuua kama tungekataa kufanya kazi yake, nimekosa kweli nilimbaka Feria hali iliyopelekea mauaji yake mbele yangu nisamehe sana Keti sikuwahi kusema haya hata nilipokuwa nawe nisamehe sana"

Bedo aliongea kwa tabu sana machozi yalimtoka pasipo kukata alijiona mkosaji mno. 

Zaki alichukua rekodi yote na kuiweka kwenye mfuko wake kisha alimsogelea kwa mara nyingine Bedo.

"Aliwapa pesa ngapi mkuu mlipofanya kazi yake"

"Alitupa Mil.10 kila mmoja na kutupa ofa ya kusoma bure hapa chuoni hadi tutakapomaliza"

"Sawa"

Kipindi chote cha maswali msichana Keti alikuwa akilia kama mtoto mdogo na kukaa chini macho yake yote yalimtazama kijana Bedo aliyekuwa hoi taabani 

"Keti nyanyuka hapo chini" Zaki alimsogelea na kumnyanyua taratibu

"Utakuwa sawa Keti" Zaki aliendelea kumpa Moyo

"Zaki kwanini baba yangu aliyafanya yote haya?" Keti aliuliza kama mtu aliyepagawa

"Ni tamaa tu usijari sawa kila mwanadamu anapitia haya"

"Naumia sana Zaki tena zaidi ya neno sana naumia mimi"

Keti aliangusha kilio tena cha nguvu 

"Kwanini mimi, mbona hukuwahi kuniambia Bedo kama ulimuua msichana hasiye na hatia Feria, kwanini ulifanya hivyo"  

Keti alilalamika huku alimfata Bedo nakuanza kumpiga mateke maeneo ya tumboni. 

"Nakuchukia sana nilikupenda nakukuamini ila sasa imani yangu umeivunja yote nakuchukia mno siwezi kukupenda tena"

Alimpiga kwa hasira huku alilalamika sana

"Umepoteza nuru yangu ya upendo juu yako umepoteza thamani ya upendo natamani Feria angekuulia mbali sijui kwanini upo hai hadi sasa sijui kwanini alikuacha"

Ilifikia hatua Bedo alianza kucheua damu mdomoni mwake alitoa damu kila alivyozidi kupigwa mateke na msichana Keti.

Keti aliendelea kumpiga hadi hamu ilipomuishia na kukaa tena chini kuanza kulia.

Wakiwa ndani zilisikika kelele nje za ving'ora vya polisi zikilia kumaanisha tayari walishafika chuoni hapo 

"Zaki ni Askari?" Keti alijisemea akilini mwake huku alishangaa sana

Bedo naye hakuwa nyuma kushangaa kuhusu kijana Zaki kumbe alikuwa Askari.

KETI AMEGUNDUA UKWELI KUHUSU BEDO NA ZAKI. Usikose sehemu ya 18 

Post a Comment

Previous Post Next Post