SIRI ZA HOSTELI 18

ILIPOISHIA

Wakiwa ndani zilisikika kelele nje za ving'ora vya polisi zikilia kumaanisha tayari walishafika chuoni hapo 

"Zaki ni Askari?" Keti alijisemea akilini mwake huku alishangaa sana

Bedo naye hakuwa nyuma kushangaa kuhusu kijana Zaki kumbe alikuwa Askari.
********************

"Hakuna muda wa kupoteza maongezi zaidi yatasimuliwa jijini Dar Es Salaam" Zaki aliyasema maneno hayo ya ujasiri na kumnyanyua Bedo aliyekuwa hoi taabani. 

Keti alikuwa mpenzi mtazamaji tu hasielewe akionacho ni kweli au alikuwa ndotoni. 

Upande wa Moni alifurahi sana akiwemo mzimu Feria uliokuwa unashuhudia tukio lote lililoendelea mahali hapo.

Bedo aliwekwa kwenye gari na Zaki alipanda pia kwaajili ya kuondoka, ila alipokuwa garini alikumbuka hakuna mahali pa kutoka kama ukiingia na mtu pekee wa kufungua ni Feria.

Alishuka kumtafuta huku akimuita kwa kutumia hisia hili amsikie ila Feria hakuwa mbali sana na eneo hata Zaki alipomsogelea alimwambia..

"Usijari Zaki mlango upo wazi wa wewe kuondoka na wenzako ila mmemsahau mtu mmoja ambaye Mkuu wa chuo hiki"

"Ni kweli nazani kabaki yeye tu ila hayuko mbali na chuo hiki japokuwa kikubwa ila leo nitamtafuta hadi nimpate na kesho nitaondoka naye"

Zaki aliachana na Feria na kuwakimbilia wenzake kuwaruhusu waondoke zao bado muharifu mmoja aliyehusika na mauaji ya Feria ajapatikana kwahiyo Zaki hawezi kuondoka siku hiyo chuoni hapo ila aliwaomba wamuachie bastola kama angeleta ubishi ampige nayo.

Walimuaga Zaki kwa kumpa heshima kubwa na wao wakatokomea. 

Zaki alivyoachwa aligeuka nyuma kurudi Hosteli ambapo Keti alikaa mwenyewe kufikiria mengi yaliyojiri siku hiyo.

"Keti bado haupo sawa?" Zaki alimuuliza alivyoingia ndani

Keti alisimama nakumkumbatia huku bado aliendelea kulia 

"Najiona mkosefu sana Zaki nimekukosea"

"Hakuna kosa lolote ulilolifanya Keti kuwa huru wewe ni mtu mwema sana hata Feria aliniambia ulivyomtendea wema kipindi cha uhai wake"

"Naumia sana Zaki"

"Usiseme hivyo kuhusu Bedo atarudi tu muda ukifika"

"Atarudi ndio lakini atakuta upendo bado upo?"

"Upendo haufi wakati wa matatizo bali hudumu milele katika maisha yetu"

"Baba yangu sitamuona tena nani nitakuwa naye ikiwa mama yangu alishafariki"

"Hapana usiseme hivyo Keti mimi nipo kwaajili yako"

Kauli ya mwisho ya "Hapana usiseme hivyo Keti mimi nipo kwaajili yako". Msichana Moni aliisikia aliyekuja kumtafuta Zaki ndani ya chumba chake

"Zaki tayari ushampenda Keti mimi nilishakupenda tangu siku ya kwanza nilivyokusaidia viwanja vya Mpira wa miguu"

Moni alimkuta Zaki akiwa amemkumbatia Keti huku akimtamkia neno la mwisho alilolisikia.

Hakutaka kukaa tena hapo badala yake alikimbia kuelekea ndani huku alijisemea kwenye Moyo wake "Siwezi kuvumilia kukuona na mwengine bora nimfate rafiki yangu kipenzi Feria"

MONI ANAENDA KUJIUA ITAKUAJE? Usikose sehemu ya 19 

Post a Comment

Previous Post Next Post