SIRI ZA HOSTELI 19

ILIPOISHIA

Moni alimkuta Zaki akiwa amemkumbatia Keti huku akimtamkia neno la mwisho alilolisikia.

Hakutaka kukaa tena hapo badala yake alikimbia kuelekea ndani huku alijisemea kwenye Moyo wake "Siwezi kuvumilia kukuona na mwengine bora nimfate rafiki yangu kipenzi Feria"
**********************

Moni aliwahi kuingia ndani na kutafuta kamba ya kujinyonga hakufanikiwa kuipata alipekua madawa kama angepata lakini wapi alikosa na akili pekee iliyomjia ni kujitupa kupitia dirishani.

Alichukua karatasi na kuandika ujumbe wake wa mwisho kisha alifungua dirisha na kutoka nje hakutaka kusubiri tena alikaa hatua ya mwisho huku moyoni mwake alisema

"Naondoka Zaki nitakukumbuka sana" 

Moni alijiangusha kutoka ghorofa ya 4 hadi chini hakuna aliyetulia kitendo cha kuanguka Keti alikiona alimshtua Zaki atazame, alipotazama tu walitoka ndani na kukimbilia nje haraka 

"Moni, Moni mama kwanini umejiua" Zaki aliwahi kumshika kabla hajafa. Moni aliongea kwa shida 

"Za...k...i" alibaki kuita na mkono wake alinyoosha juu ghorofa ya 4.

Zaki hakutaka kuchelewa alikimbia juu huku mawazo yake akifikiri huenda kuna mtu amemuangusha aliwahi kuingia haraka na kufungua mlango.

Alitazama tazama na kugundua kulikuwa na karatasi kwenye kitanda, Zaki alisogelea karatasi lile lililoandikwa....

"Zaki nilikupenda tangu siku ya kwanza nilivyokusaidia kwenye viwanja vya Mpira uchezaji wako niliupenda sana kwasababu nilipenda sana kucheza Mpira na kuangalia pia, nilishindwa kukwambia ila ile siku uliyoniona nimeshika picha ya Feria nilikuwa naongea naye kumwambia Nimekupenda wewe kwasababu kipindi cha uhai wake hakuwahi kuniona na mwanaume yeyote hata kusikia na mimi nilikuwa nikimwambia siku nikipenda nitakwambia tu basi siku ile nilimwambia na wewe ulitokea hali iliyosababisha nitoke machozi nilipokuona wewe ukiwa mbele yangu. Hakika nilikupenda ila leo nilipokuja chumbani nilikukuta ukiwa na Keti mmekumbatiana huku ukimwambia maneno ya upendo iliniuma nikaona isiwe sababu ya kuendelea kuishi ikiwa nimemkumbuka rafiki yangu Feria. Ni mimi Moni" 

Zaki aliweka ujumbe ule kwenye mfuko wake na kuchukua simu yake ya kipolisi kupiga kwaajili ya kuchukua maiti. 

Alitoka nje na kumkuta Keti mlangoni 

"Kuna nini Zaki?"

"Hamna kitu Keti"

"Kuwa na amani sawa?"

"Sawa nipo na amani"

Usikose sehemu ya mwisho ya 20. 

Post a Comment

Previous Post Next Post