ILIPOISHIA
Alitoka nje na kumkuta Keti mlangoni
"Kuna nini Zaki?"
"Hamna kitu Keti"
"Kuwa na amani sawa?"
"Sawa nipo na amani"
*****************************
Zaki alirudi kwa Moni aliyekuwa amefunikwa tayari na kuchuchumaa karibu yake
"Moni kwanini ulifanya hivyo, kwanini ulijiua, ungeniambia tu, umechukua uamuzi mgumu sana nashindwa nimlaumu nani"
"Zaki" Sauti ya Mzuka Feria ilimuita
Zaki alipogeuka kutazama
"Feria, Moni amejiua mwenyewe"
"Usijari Zaki, Moni hawezi kurudi tena"
"Tafadhali kamuite niongeee naye"
"Kumbuka alijiua ina maana yeye sio miongoni mwetu sisi ni roho zisizo na hatia tuliofanyiwa unyama kwa malengo binafsi ya watu wengine ila Moni wakati wake ulifika ndio maana alijiondoa duniani, apumzike kwa amani hata mimi nina muda mchache wa kukutana naye mbaya wangu akikamatwa"
Zaki machozi yalimtoka alikumbuka alivyosaidiwa na Msichana Moni pale uwanjani lakini alishindwa kumsaidia siku hiyo aliyojiua.
"Ningekuwahi usingekufa kirahisi hivi Moni umetuacha wote nilishakuzoea sana sijui kwanini ulichukua uamuzi huu mzito, Moniiiiii"
Zaki aliendelea kunung'unika mwenyewe ndipo sauti ya mwanachuo mwenzao akiwa ana kimbia aliwahi na kuwapa taarifa..
"Jamani Mkuu wa chuo hiki amepatikana akiwa amejinyonga ofisini kwake muda huu"
"Baba!" Keti aliita jina hilo na kukimbia haraka, alikuwa wa kwanza kufika ofisini kabla ya wote
"Baba, baba, baba amka kwanini umekufa baba, kwanini umejiua baba, baba amka baba anguuuuu" Keti aliita akiwa analia sana
"Baba angu umeniacha mwenyewe, baba kwanini umenifanyia hivi, baba umeniacha kama alivyoniacha Bedo, baba kwanini umeniacha baba, naumia mimi baba" Bado Keti aliendelea kulia
Zaki alikuwa amesimama tu akisubiri hatma ya kilio cha Keti.
Keti aliendelea kulia sana pasipo kunyamaza ndipo ving'ora kwa mara nyingine viliwasiri, Askari waliingia wakiwa na machela walimchukua Moni na machela nyingine walimchukua Mkuu wa chuo.
"Baba usiniache, baba tafadhali, baba angu" Keti alimpenda sana baba yake na ndiye mtu pekee aliyebaki duniani.
Zaki alimuomba Keti aongozane naye mjini kwaajili ya mazishi ya baba yake Mkuu wa chuo hiko na cha pili alimwambia kuhusu Bedo alishahukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kuwa mmojawapo aliyehusika na kifo cha msichana Feria Cha tatu alimuomba kuishi naye hadi pale hali yake itakapokuwa sawa atarudi tena chuoni hapa.
Keti hakukataa alikubari kwa shingo upande, hakuwa na msaada mwengine zaidi ya kijana Zaki.
Naye Zaki alimtafuta Feria na kumuona kwa mbali akiwa anatabasamu sana alimuaga kwa ishara ya kumpungia mkono huku naye Feria alimjibu kwa kumpungia mkono.
"Asante sana Zaki naenda kupumzika kwa amani sasa" Feria aliongea huku alimtazama Zaki aliyeishia getini na Askari wenzake chuoni hapo.
*MWISHO*
FUNZO: HAKUNA MALIPO YA MBALI KATIKA DUNIA HII TUNALIPWA HAPAHAPA.
Tags:
CHOMBEZO