KIBUTI 03💃

Sasa unaweza pata picha kwamba Frank anashobokewa na wanawake kibao ila hawataki kwa muda huo, anamtaka Nurat. Nurat anashobokewa na wanaume kibao, ila hawataki wote. Frank akafuatilia info za Nurat, akaja kujua kuwa na yeye ni wa kishua sana, tena zaidi yake. Frank hakufa moyo. 

Frank akasema hapa kuhonga hakufai, outing za kawaida nitaumbuka. Siku ya siku Frank alijipanga kumuomba Nurat watoke kwenda sehemu flani, which aliamini atakataliwa tu. Akiwa njiani kwenda kwa Nurat, kuna Prado nyeusi ikampita kama upepo na kumuachia vumbi ikielekea anapoenda. 

Frank akatukana kimoyomoyo(fala nini, utafilisika tu), akafika zake Hostel akapanda gorofani. Wakakutana uso kwa uso na Nurat akitoka, akamsalimia Frank na kumwambia mi natoka na mume wangu mtarajiwa, labda uje kesho maana sirudi leo. Frank moyo paaaaaaa, na akaishiwa nguvu😏.

Akamcheck mtoto akishuka, akafika kwenye ile Prado jamaa akashuka(kipande), akampa wet kiss refu tu. mtoto akaingia kwenye ndinga wakasepa wakiacha vumbi machoni mwa Frank. Hakuwahi kupenda mwanamke kama hivi, aliangusha chozi. Frank akajisemea “Karma is doing her dirty work”. 

1 Comments

Previous Post Next Post