KIBUTI 02💃

Sasa kuna mrembo mmoja wa kuitwa Nurat alikuwa mwaka wa kwanza pia kozi tofauti na ya Frank. Jamaa alimuona mara ya kwanza pale utawala sijui alifuata nini mshikaji maana sio pigo zake(ye akishalipa ada, hataki kung’aa pande hizo). Frank akapishana na toto la hatari mzeeee🍑

Akasimama kwanza na kuvunja shingo, akaduwaa, akapiga picha afu akasepa zake. Akarudi room kwake akamuuliza mshikaji, “oya unamsoma huyu mtoto”, jamaa akamwambia hapana. Frank akaumia moyo ila akasema ipo siku atamkuta tena. 
Punde si Punde akakutana nae tena, this time ni cafe.

Jamaa akapiga nae story 2/3 pale, akachukua digits then akasepa room. Frank alifurahi na hakutegemea kama zoezi gumu lingekuwa jepesi vile. Kosa alilofanya Frank ni kumtafuta yule demu siku ileile na ilikuwa night.
Fra: mambo?
Nur: poa.
Fra: naitwa Fra
Nur: aha, mbona saa hizi?

Fra: nimeona nikusalimie.
Nur: kwani ungengoja hadi kesho ungekufa?
Jamaa moyo ukapasuka na kufokewa kule, akaaga akalala zake😀.
maisha yakaendelea huku akiendelea kupiga sound kwa mtoto na kugalagazwa vizuri tu. yule mtoto alitolewa macho na kila mwanaume pale SUA. 

Post a Comment

Previous Post Next Post