KIBUTI O1

*KIBUTI* 💔 Ni simulizi inayomhusu kijana mtanashati, handsome kabisa anaitwa Frank huyu...

 hakuwahi kutongoza kabisa huyu jamaa ye ndo alkuwa anatongozwa na madem tangu akiwa primary hadi inafikia pisi zinapigana kisa yeye 🙆🏼‍♂️

Frank hajui shida anatokea Ushuani... ile huku na huku mara anajikuta anapenda pisi moja kali (nayo ya Ushuani) ila inamtolea nje... anajaribu kila namna ila wapi tu 😃

Oyaa fanya ufatilie kisanga hiki hope utapata kitu

@hadithikali 



Story by JAPHET LUHENDE 
  0675 373 713
  @HadithiKali

Kuna daktari mmoja alikuwa anasoma SUA(Vet), jina lake ni Frank. Kwa mujibu wa wanawake waliomuona live au kwenye picha wanasema ni bonge la handsome. mimi kwangu alikuwa ni mshikaji sana, mcheshi na mtoa support kwa wana.
Frank alikulia mazingira ya kishua flani. Primary, O’level na Advance jamaa alikuwa. akishobokewa sana na warembo hadi kufikia hatua wana wanamchukia. Frank hakujali maana hawezi kucontrol hiyo hali, na pia yeye anafuatwa si anakuwa mkarimu tu(warembo waliliwa wengi tu). Sasa alipofika chuo ndo mambo yakawa HOT🔥. Mwaka wa kwanza sem1, jamaa anakanyaga chuo tu hata wiki bado warembo wanashoboka. akanipigia mwanae like “oya mwanangu, SUA kuzuri kinoma”, mi nikahisi anamaanisha mazingira. Nika-support mada na story zikaendelea kiaina then akaaga. class lake lina-wadada 10 tu, afu kawaida tu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post