SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA...FINAL. 24 MWISHOOOO

Kwa sasa naishi nairobi kenya,,,na kazi zanzibar niliacha ila huku kuna biashara naisimamia ya haohao maboss zangu,,baada ya kuona nimeolewa hawakutaka tupotezane hivyo wakafungua duka la simu kubwa sanaa na mimi ndo nalisimamia japo nina vibiashara vyangu mwenyew pia navifanya maana pale dukani nasimamia tu muuzaji yupo hivyo hapanibani sanaaaa hua naenda kukagua na kufunga mahesabu,,,Tanzania nikienda hua nafikia madare na mara nyingi hua naenda na mme wangu na ndo maana nikajenga nyumba ya design hiyo ili tusimnyime mama uhuru tukiwa Tanzania...sina taarifa zozote kuhusu francy maana sikutaka kumfatilia na hela yake ya mahari nilimtumiaga mama akamrudishia nusu maana alikua anamsumbua sana mama,,,sikumpa yote maana nami alinipotezea muda wanguuu,,pia nilirudi chuo nikachukua vyeti vyangu nikamlipa mtu mzima hovyo hela zake alizokua ananidai,ila sikuendelea na masomo nilichukua tu vyeti,,kiufupi aliona aibu sana siku nilipoenda,,lakini tabia yake ya kutembea na wanafunzi hajaachaga hadi hivi leo ndo zake,,na kila akioa mke anakaa miaka michache anakufa anaoa tena yaani ndo maisha yake,,,

NAOMBENI USHAURI WENU
Naomba mnisaidie ama kunielekeza dawa ambayo itanisaidia kupata mtoto hii hali inanitesa sanaa,,najua nilifanya kosa ila sikua na namna kwa kipindi hicho na najutia sanaa kwa hilo,,na ni hiyo mimba moja tu sikuwahi toa nyingine wala kupata nyingine,na sijawahi kutumia dawa yoyote ya kuzuia mimba, na hata kwa mliokua kenya pia nahitaji msaada wenu maana najua mnajua dawa nzuri au njia ya kufanya kutatua tatizo hili,nina miaka 31 sasa umri unaniacha.. nafatilia comment wapendwa,,,asanteni woote mlioifatilia story yangu na comment zenu zimenijenga sana mungu awabariki hadi mshangae...
    Nawashauri pia kwa wanawake wanaopitia changamoto kwenye ndoa, si kila kitu unavumilia mengine unajikosesha rizki,,ukiona mahusiano hayaeleweki yana maumivu na mateso ni vyema ukaachana nayo Mungu atakupeleka sehemu sahihi na kwa mtu sahihi,,,
   Pia kwa mabinti msipende kukurupika,,shida nyingine ni za kujitakia,,jitahidini kushindana na mihemko la sivyo utajikuta unaingia pabaya...wazazi pia muwe karibu na mabinti zenu,,ukari muda mwingine hausaidii bali humfanya mtoto ashindwe kukuweka wazi matatizo anayopitia...
  Nawapenda sanaa,, asante Paulin mpenzi kwa kunipostia story yangu mungu akuweke kwaajili yetu
LOVE YOU ALL 😍😘😘😘❤ 

Post a Comment

Previous Post Next Post