SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA: 23

Nikamwambia,,,francy asante sana kwa maisha tuliyoishi,,asante kwa kunipenda tangu siku ya kwanza,,asante kwa kunipa heshima kwetu maana ulikua mwanaume wa kwanza kwenda kujitambulisha na kufata taratibu zote zinazohitajika asante sanaaa,,,ila naomba nikwambie kitu, mimi na wewe hatutawezana,,mimi si mwanamke ninaekustahiri, naomba tuachane,,,alishtuka akakaa vizuri,,,unasema!!! Aliuliza kwa mshangao,,,nami nikamjibu tena,,,naomba tuachane,kama utahitaji kurudishiwa gharama za mahari nitazirudisha mwenyewe wala usihangaike kumdai mama yangu,,,,akacheka kisha akasema winie unanitania umeshapata bwana mwingine anakuchanganya??? Nikamjibu,wala hakuna mtu wa kunichanganya ila maisha ndo yananichanganya hivyo naomba tu tuachane kwa amani, alilalamika usiku kucha ila sikumsikiliza na sikumwambia lini naondoka mi nililala zangu,,,asubuhi aliamka mapema akatoka nikajua huyu anaenda kwa shangazi yake,,nami sikulemba nikaamka nikajiandaa haraka nikapaki nguo zangu zote kwenye begi nikavua pete yake ya uchumba nikamuwekea mezani maana alinivishaga pete ya uchumba, nikamuachia na ujumbe kwenye karatasi,,,NAENDA SEHEMU SALAMA USINITAFUTE KUA NA AMANI NAKUTAKILA KILA LA KHERI,,MAMA YANGU HAJUI CHOCHOTE USIMUINGIZE WENYE HILI,,,kisha nikaita bodaboda ikanipeleka bandarini nikachukua boti ya saa tatu safari zanzibar kuanza maisha mapya,,,baada ya masaa mawili nilifika zanzibar nikapokelewa na mfanyakazi mwenzangu akanipeleka kwenye nyumba nitakayokua nakaa,,kisha tukaenda offisini nikakabidhiwa kila kitu pamoja na mkataba wangu,,,kisha nikarudi nyumbani kupumzika,,,nyumba waliyonichukulia nilikua nakaa mwenyew na offisi ndo ilikua inalipia ilikua ina kula kitu ndani sikua na haja ya kununua chochote,, francy alipiga simu kama kichaa lakini sikupokea,,shangazi yake ndo usiseme pia sikupokea,alituma msg za lawama na vitisho lakini hazikuniumiza nilijua wanatapatapa tu,,,nilimpigia simu wazazi wa francy kijijini niliongea nao vizuri na kuwaeleza kwa ufupi yaliyotokea na kuwaambia kua nimeondoka kwa mtoto wao na sitorudi tena,walihuzunika sanaa lakini ndo nilishafanya maamuzi,,,baada ya hapo nikaivunja laini nikaitupa, nikatengeneza nyingine kisha nikamtafuta mama nikamwambia nilipo na kumuomba asimpe mtu yeyote no yangu hadi mambo yakikaa sawa,,,alifurahi sana kuona nimepata kazi akanipa na baraka zoote,,,,
   Nilifanya kazi kwa muda wa miaka mitatu nashukuru mungu maisha yangu yalibadirika kwa kiasi kikubwa,,,nilifanya kazi kwa bidiii maboss zangu walinipenda sana,hata wafanyakazi wenzangu,,,nikafanikiwa kujenga nyumba dar esaalam namshukuru mungu kwa hilo 🙏🙏 nyumba kubwa tu ya kisasa ya gorofa moja,,chini anaishi mama yangu maana ameshastaafu hivyo ameamia dar ndo anaishi hapo,,na juu nimeweka chumba kimoja masta na kuna kila kitu yaani jiko,dinning, sebure ndogo na sehemu ya kupumzikia kwa nje ukiwa hukohuko juu, huko juu hua nikienda dar esaalam hua nafikia mimi ila mama kwake chini hua sipendi kumbana, nyumba nimejenga madare... Kipindi nikiwa kazini nilikua napata fursa za kusafiri nchi mbalimbali na nikakutana na mtu mwingine ambae sasa ndo mume wangu halali wa ndoa🥰😘😘 ila yeye ni mkenya kabila mluya,,,aliweza kunisahaulisha kero zote nilizopitia,,,ni mwanaume wa ndoto zangu naweza kusema hivyo maana anapenda na kujali mpaka basi,,,tunaishi kwa amani, upenda na furaha sanaa,,tuna miaka mitatu sasa hatujawahi kukosana hata kwa bahati mbaya nisiwafiche kiufupi ni mwelewa na anaelewa jinsi ya kuishi na mke najivunia kua nae,,,nilimweleza matatizo yangu ya uzazi na ilo si shida kwake wala kwa ndugu zake,,,kiufupi wananipenda mnooo na kama mnavyojua watz tunavyojua kunyenyekea na kumdekeza mume hasa ukimpata anaekuthamini,,hicho ndicho kinachoifanya ndoa yetu iwe na amani sanaaa,,,anaijali furaha yangu na amani yangu ya moyo namshukuru mungu kwa hilo,,,tulienda baadhi ya hospitali nikapima nikaambiwa kizazi ninacho, na mayai yapo ila mrija mmoja ulijikunja,,ikabidi nifanyiwe operation kwa maelezo ya madaktari wakasema uko sawa lakini bado sijafanikiwa kupata mtoto hadi muda huu.....
 ITAENDELEA...... 

Post a Comment

Previous Post Next Post